Kweli maisha ya sasa, ndoa inatafutwa kwa lazima

Kweli maisha ya sasa, ndoa inatafutwa kwa lazima

Kazi sio kigezo pekee cha ndoa.

Kuna muonekano wake, tabia zake, familia yake anayotoka, asili yake, kuna factor nyingi zinamfanya mwanamke aolewe. Kazi sio kigezo pekee
Ndio wakipata mtu mwenye muelekeo, wanajisogeza kabisa
 
Kutokana na changamoto za kiuchumi pamoja na uhaba wa wanaume wenye sifa za uoaji kupungua; mabinti wakileo wameanzisha utaratibu wa kujisogeza kwa mwanaume na kuanza naye maisha, bila kufuata taratibu za ndoa.

Kuna binti mmoja amemaliza chuo, na kukaa mwaka mmoja nyumbani bila kazi, akaona haya maisha hayaeleweki, akabeba nguo zake akajisogeza kwa baharia (mchumba wake), sasa hivi wanaishi nyumba moja, pika nipakue.

Wengine wako chuo wanasema, kazi nikose, na mume pia nikose? Kwa hiyo wanahitimu chuo, na baada ya hapo wanajisogeza kwa wachumba zao na kuanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Wengine wako mtaani, wakiona wapenzi wao wana muelekeo fulani wa kimaisha, wanahisi wanaweza kuja kutelekezwa; kinachofanyika ni mabinti kubeba vitu vyao na kuamia kwa wapenzi wao bila utaratibu ule wa zamani wa kusubiri ndoa.

Ama kweli si mwanamke wala si mwanaume; nyakati hizi wote ni mabaharia.

Kweli maisha ya sasa, ndoa inatafutwa kwa lazima.​
Waoe uone Sasa balaa lao 😃😃😃


Wanawake wanatafuta Sana ndoa ila wakizipata huwa wanazichezea
 
Kuna mwengine anakukoleza kitandani anakuvuruga na midawa ya kwa babu, lazima utamuoa tuu.

Ila kuna wengine mpaka wanahonga wanaume, mimi kula hela ya mwanamke sijui na onaje na sijawahi kula hela ya mwanamke.

Kuna mwanangu yy michepuko yake yote ni mabinti wenye hela na wote kawapata kwa kuingia na gear ya kuwaoa.
 
Back
Top Bottom