Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,319
Mwenye upendo wote na uwezo wote anaachia anaowapenda wapatwe na mabaya au haachii?
Kwa nini mwanadamu aweze hata kufikiri kwamba hili ni baya, hapa nimeonewa, sijatendewa haki etc.
Hilo wazo tu lilitakiwa lisiwepo kama mungu mwenye uwezo wote na upendo wote yupo kweli.
Umeelezwa juu ya "fallacy of definition " kuwa ndiyo msingi Mkuu kwenye hoja zako zinazokosa uhusiano wa kimantiki huku ukiwa umeng'ang'ana na mwenye upendo wote,uwezo wote pasipo kujua uwezo wote na upendo wote ni kitu gani.
Wewe umekariri kwamba upendo wote na uwezo wote unakomea pale kariri zako zilipoishia...
Hoja kuu ni kuweka hoja ya kimantiki inayokufanya upate nguvu kuandika na kuonyesha kuwa MUNGU HAYUPO KWA VILE KARIRI ZAKO ZINAONA MAMBO AMBAYO YANAFANYA ASIWEPO, MAMBO YENYEWE NI MAOVU AU MABAYA YANAYOWEZEKANA KUTOKEA.
ELEZA KANUNI ULIYOTUMIA AMBAYO IMEKUWEZESHA KUHUSIANISHA KUWEPO KWA MAOVU DUNIA NA KUTOKUWEPO KWA Mungu.
Usilete kariri zako na kuweka maswali kana kwamba hayo maswali ndiyo kanuni ya kimantiki.
Atheism is totally a blind faith...
Ujanja ya kujibanza kwenye sayansi kuficha dini yenu umeonekana siku nyingi Sana ni kwa kuwa hamjitambui wataalam wa kukariri pasio kureason...
Kauli zenu sio kauli za kisayansi , sayansi na Atheism ni Kama usiku na mchana havikutani.
Angalau Mimi nikisoma .... Hapo mwanzo Mungu aliumba...
Sayansi imegundua uwepo wa mwanzo wa ulimwengu...
Angalau biblia imeitangulia sayansi kwenye ujuzi wa ulimwengu kuwa na mwanzo na hata nyakati kuwa na mwanzo.
Tofauti ni malengo na maudhui tu lakini Atheism ni imani/dini isiyo na mahusiano na sayansi kimtazamo lakini waumini wake hujibanza kwenye sayansi ili kujikinga na mvua ya hoja zinazotakiwa wazijibu.