Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Tanzania haiji endelea hata siku moja kwa kuwa na Rais Legelege, mpiga porojo,chuma ulete,mpenda starehe,mdekezaji,mwivi,fisadi,asiyejiamini, anayeendeshwa na watu kadhaa.
Nchi italiwa, itafisaidiwa kodi na mikopo. Wezi watakumbatiwa na kutamba kwenye korido za Ikulu. Maskini wana maskinika, watanyanyaswa na kukamuliwa.
Nchi italala mafisadi wataota pembe na wanasiasa uchwara watafanya ujasiliasiasa. Hawa watakuwa wakipewa kiziba mdomo na kuendelea kuacha Serikali kama hiyo ijikite kuota mizizi. Utaona watakavyopishana ikulu na kutoa matamko ya kuunga mkono juhudi.
Maskini watatumika kupangwa kama ngazi ili wanasiasa njaa wafikie sehemu za juu za utukufu. Maisha yatabaki yale yale. Asiye nacho hata kile kidogo alichodhani anacho atanyang'anywa na kitapelekwa kwa aliye nacho. Huyo ataongezewa.
Masheikh,Mapadre,Wachungaji,Maaskofu,Maulamaa,Maimam hawa watakuwa na posho yao nao watajiunga katika kusifu na kuabudu. Nchi itakuwa gizani. Kila mtu ata Chukua Chake Mapema. Maana atakula kwa urefu wa Kamba yake.
Na akimaliza majani yaliyo kwenye urefu wa kamba yake atahamia maeneo ambayo ni ya wenzie. Atakata na kamba awe huru zaidi katika kula.
Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.