Kweli nawaambia, ili nchi hii iendelee inahitaji Rais Shupavu, Smart, Mwenye Uchungu na Nchi na Mapenzi kwa watu wake

Tanzania haiji endelea hata siku moja kwa kuwa na Rais Legelege, mpiga porojo,chuma ulete,mpenda starehe,mdekezaji,mwivi,fisadi,asiyejiamini, anayeendeshwa na watu kadhaa.

Nchi italiwa, itafisaidiwa kodi na mikopo. Wezi watakumbatiwa na kutamba kwenye korido za Ikulu. Maskini wana maskinika, watanyanyaswa na kukamuliwa.

Nchi italala mafisadi wataota pembe na wanasiasa uchwara watafanya ujasiliasiasa. Hawa watakuwa wakipewa kiziba mdomo na kuendelea kuacha Serikali kama hiyo ijikite kuota mizizi. Utaona watakavyopishana ikulu na kutoa matamko ya kuunga mkono juhudi.

Maskini watatumika kupangwa kama ngazi ili wanasiasa njaa wafikie sehemu za juu za utukufu. Maisha yatabaki yale yale. Asiye nacho hata kile kidogo alichodhani anacho atanyang'anywa na kitapelekwa kwa aliye nacho. Huyo ataongezewa.

Masheikh,Mapadre,Wachungaji,Maaskofu,Maulamaa,Maimam hawa watakuwa na posho yao nao watajiunga katika kusifu na kuabudu. Nchi itakuwa gizani. Kila mtu ata Chukua Chake Mapema. Maana atakula kwa urefu wa Kamba yake.

Na akimaliza majani yaliyo kwenye urefu wa kamba yake atahamia maeneo ambayo ni ya wenzie. Atakata na kamba awe huru zaidi katika kula.

Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.
Tunahitaji dikteta mmoja mwenye akili na vision. Sio mtu wa kupenda cheap popularity.
 
HUYO RAIS LABDA ASITOKE CCM
CCM imebaki kasha tu la kubebea kila takataka. Akitokea mmoja wao mwenye nia hasa ya kulichoma moto hilo kasha, mambo yatanyooka vizuri tu!

Tatizo ni hilo moja la kupatikana mTanzania huyo, au kundi dogo la waTanzania wenye nia hiyo.

CCM ya siku hizi ni huyo mtu mmoja aliyeko juu, basi. Na kwa bahati mbaya sana kwa waTanzania, huyo anayekuwepo huko juu ya kasha, ni huyo huyo anayelitumia kasha kujaza uchafu zaidi kwenye kasha lenyewe..
 
Tanzania haiji endelea hata siku moja kwa kuwa na Rais Legelege, mpiga porojo,chuma ulete,mpenda starehe,mdekezaji,mwivi,fisadi,asiyejiamini, anayeendeshwa na watu kadhaa.

Nchi italiwa, itafisaidiwa kodi na mikopo. Wezi watakumbatiwa na kutamba kwenye korido za Ikulu. Maskini wana maskinika, watanyanyaswa na kukamuliwa.

Nchi italala mafisadi wataota pembe na wanasiasa uchwara watafanya ujasiliasiasa. Hawa watakuwa wakipewa kiziba mdomo na kuendelea kuacha Serikali kama hiyo ijikite kuota mizizi. Utaona watakavyopishana ikulu na kutoa matamko ya kuunga mkono juhudi.

Maskini watatumika kupangwa kama ngazi ili wanasiasa njaa wafikie sehemu za juu za utukufu. Maisha yatabaki yale yale. Asiye nacho hata kile kidogo alichodhani anacho atanyang'anywa na kitapelekwa kwa aliye nacho. Huyo ataongezewa.

Masheikh,Mapadre,Wachungaji,Maaskofu,Maulamaa,Maimam hawa watakuwa na posho yao nao watajiunga katika kusifu na kuabudu. Nchi itakuwa gizani. Kila mtu ata Chukua Chake Mapema. Maana atakula kwa urefu wa Kamba yake.

Na akimaliza majani yaliyo kwenye urefu wa kamba yake atahamia maeneo ambayo ni ya wenzie. Atakata na kamba awe huru zaidi katika kula.

Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.
Cc @ Machawaaaa wrote uvccm
 
Ili nchi iendelee inahitaji demokrasia tu Mambo mengine yanakuja demokrasia ikiwa strong. Angalia marekani na uraya. Hapa kwetu JPM alitaka kuizika nchi mchana kweupe
pumbv kwel aliekwambia democrasia inaleta maendeleo ni nan?... hebu twambie maana ya democrasia....et marekan na ulaya hujuw hata chchte,,,
 
Ulipoandika uraya tu nikakuona kiazi mbatata au kashata-pori!
 
pumbv kwel aliekwambia democrasia inaleta maendeleo ni nan?... hebu twambie maana ya democrasia....et marekan na ulaya hujuw hata chchte,,,
Madikiteta lengo lao ni kujimilikisha nchi kwa kikundi kidogo cha watawala na wanajeshi wao tu.

Maendeleo yanabaki kuwa porojo na propaganda za mitanadoni kama awamu ya tano ilivyokuwa
 
Ili nchi iendelee inahitaji demokrasia tu Mambo mengine yanakuja demokrasia ikiwa strong. Angalia marekani na uraya. Hapa kwetu JPM alitaka kuizika nchi mchana kweupe

Broo we mwongo u.s.a na ulaya magharibi wametajirika karne ya 16 kwa kupora asia na africa sema akitokea wa kuwavusha daraja mnamkata kauli.
 
pumbv kwel aliekwambia democrasia inaleta maendeleo ni nan?... hebu twambie maana ya democrasia....et marekan na ulaya hujuw hata chchte,,,
Wawekezaji wanawekeza sehemu ambayo kuna demokrasia. Ndo Mana wakati wa dictator jpm wawekezaji walikuwa wanakimbia kwa speed ya 5G aliposhtuka akaanza kuwabembeleza akina rostam but too late
 
Nchi ya viongozi wachumia tumbo, hata uwe smart vipi watakuhujumu tu...

Pakichimbika na wachache wakinusa the HAGUE kidogo tutakaa sawa...
 
Ili nchi iendelee inahitaji demokrasia tu Mambo mengine yanakuja demokrasia ikiwa strong. Angalia marekani na uraya. Hapa kwetu JPM alitaka kuizika nchi mchana kweupe
Mbona chadema haijaendelea wakati ni chama cha demokrasia na maendeleo? Kama ni umaskini basi chama kiko kwenye level ya ufukara. Au nao ni jina tu na hakuna demokrasia yoyote huko ndani chamani?
 
Demokrasia si msingi wa maendeleo. Maendeleo yanaletwa na Uthubutu, Nia njema,Ushupavu na maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom