Kweli nawaambia, ili nchi hii iendelee inahitaji Rais Shupavu, Smart, Mwenye Uchungu na Nchi na Mapenzi kwa watu wake

Kweli nawaambia, ili nchi hii iendelee inahitaji Rais Shupavu, Smart, Mwenye Uchungu na Nchi na Mapenzi kwa watu wake

Demokrasia maana yake aliyeko madarakani akivurunda kuwe rais kumwajibisha. Sasa Kama jpm alivyokuwa anafukuza wawekezaji kungekuwa na demokrasia nzuri angewajibishwa mana uchumi ulikuwa unaelekea shimoni akashtuka baadae akaanza kuwabembeleza akina rostam ili wasiondoke.
Demokrasia bila kazi ni ujinga. Hauwezi kulinganisha marekani na Tz.Wao hawahangaiki tena na madawati na vyumba vya madarasa

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Tumefikia kuyawaza haya tena?!
Nilidhani mama anaupiga mwingi na haya matozo na mfumuko huu wa bei. Wacha tuisome number ili uchaguzi unaokuja tuwajaze wapinzani bungeni na ile nafasi kuu itajulikana tu. Time will tell
 
Raisi chuma ulete!😅😅 Naona sifa hii kama anayo hivi! Alafu unakuwa na anayeongozwa na watu, hapo lazima nchi ikwame
 
Tanzania haiji endelea hata siku moja kwa kuwa na Rais Legelege, mpiga porojo,chuma ulete,mpenda starehe,mdekezaji,mwivi,fisadi,asiyejiamini, anayeendeshwa na watu kadhaa.

Nchi italiwa, itafisaidiwa kodi na mikopo. Wezi watakumbatiwa na kutamba kwenye korido za Ikulu. Maskini wana maskinika, watanyanyaswa na kukamuliwa.

Nchi italala mafisadi wataota pembe na wanasiasa uchwara watafanya ujasiliasiasa. Hawa watakuwa wakipewa kiziba mdomo na kuendelea kuacha Serikali kama hiyo ijikite kuota mizizi. Utaona watakavyopishana ikulu na kutoa matamko ya kuunga mkono juhudi.

Maskini watatumika kupangwa kama ngazi ili wanasiasa njaa wafikie sehemu za juu za utukufu. Maisha yatabaki yale yale. Asiye nacho hata kile kidogo alichodhani anacho atanyang'anywa na kitapelekwa kwa aliye nacho. Huyo ataongezewa.

Masheikh,Mapadre,Wachungaji,Maaskofu,Maulamaa,Maimam hawa watakuwa na posho yao nao watajiunga katika kusifu na kuabudu. Nchi itakuwa gizani. Kila mtu ata Chukua Chake Mapema. Maana atakula kwa urefu wa Kamba yake.

Na akimaliza majani yaliyo kwenye urefu wa kamba yake atahamia maeneo ambayo ni ya wenzie. Atakata na kamba awe huru zaidi katika kula.

Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.
Kama nani? Kwani Nchi haiendelei? Tafrisi ya kuendelea ni ipi?

Tusipopata Katiba mpya sasa tuendako tunaweza pata makatili na mataahira wengine kama Mwendazake,Kim,Putin,Xi Jiping na takataka zingine kama hizo.
 
Tanzania haiji endelea hata siku moja kwa kuwa na Rais Legelege, mpiga porojo,chuma ulete,mpenda starehe,mdekezaji,mwivi,fisadi,asiyejiamini, anayeendeshwa na watu kadhaa.

Nchi italiwa, itafisaidiwa kodi na mikopo. Wezi watakumbatiwa na kutamba kwenye korido za Ikulu. Maskini wana maskinika, watanyanyaswa na kukamuliwa.

Nchi italala mafisadi wataota pembe na wanasiasa uchwara watafanya ujasiliasiasa. Hawa watakuwa wakipewa kiziba mdomo na kuendelea kuacha Serikali kama hiyo ijikite kuota mizizi. Utaona watakavyopishana ikulu na kutoa matamko ya kuunga mkono juhudi.

Maskini watatumika kupangwa kama ngazi ili wanasiasa njaa wafikie sehemu za juu za utukufu. Maisha yatabaki yale yale. Asiye nacho hata kile kidogo alichodhani anacho atanyang'anywa na kitapelekwa kwa aliye nacho. Huyo ataongezewa.

Masheikh,Mapadre,Wachungaji,Maaskofu,Maulamaa,Maimam hawa watakuwa na posho yao nao watajiunga katika kusifu na kuabudu. Nchi itakuwa gizani. Kila mtu ata Chukua Chake Mapema. Maana atakula kwa urefu wa Kamba yake.

Na akimaliza majani yaliyo kwenye urefu wa kamba yake atahamia maeneo ambayo ni ya wenzie. Atakata na kamba awe huru zaidi katika kula.

Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.
HUYO RAIS LABDA ASITOKE CCM
 
Ili nchi iendelee inahitaji demokrasia tu Mambo mengine yanakuja demokrasia ikiwa strong. Angalia marekani na uraya. Hapa kwetu jpm alitaka kuizika nchi mchana kweupe
Nchi gani ya Ulaya ina demokrasia?
Demokrasia ipo Marekani na labda India, Australia kufuatua kidogo.
Ulaya ni kingdoms zenye demokrasia zenye utata.
 
Nani kakwambia democracy ndio maendeleo? Ujinga wa wazungu uo. Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi dikteta kama Magufuli.

Mbona Magufuli aliharibu nchi sasa ndani ya miaka mitano hakuna ajira, hakuna nyingeza ya mishahara, wawekezaji wanazidi kuikimbia, mahoteli yanazidi kufungasha virago, gdp inazidi kushuka. Akabaki tegemeo lake kuu la mapato ni wizi kwa kuvamia na kuchukua pesa kwenye account za watu moja kwa moja na kutengeneza machinga nchi nzima ikawa ni vurugu. Watu wenye maduka makubwa wakawa wanalipa Kila siku na kutaka kuhamisha biashara zao nchi za jirani. Machina wakawa wanaweka viulembo vyao mlangoni kabisa kwa mwenye duka na mabarabara yote hayapitiki ukiwa na gari lako unawahi kazini I abidi ulipaki uchukue angalau bodabod.
 
Nchi gani ya Ulaya ina demokrasia?
Demokrasia ipo Marekani na labda India, Australia kufuatua kidogo.
Ulaya ni kingdoms zenye demokrasia zenye utata.
Tanzania sasa Ina demokrasia? Angalau kidogo kipindi hiki Cha Samia. Jpm alikuwa anasigina waziwazi katiba na ya nchi na akaenda mbali kutaka kuwa life president wakati Kila kitu kimehalibika
 
Ili nchi iendelee inahitaji wananchi smart na wachapakazi hodari, ili wamsaidie Rais.
Rais ni mhamadishaji tu, awepo asiwepo nchi na wenye nchi wataendelea kuwepo.
Mabadiliko ya fikra ni muhimu sana kwa wananchi kujua kwamba Rais anawategemea wananchi kuendeleza nchi, kila mmoja (Rais na wananchi) ana wajibu na nafasi yake katika kuendeleza nchi.
Viongozi wawepo au wasiwepo, nchi na wananchi watabaki.
Katikati ya Wananchi na Rais ni LAZIMA UWE NA MIFUMO IMARA ya uogozi wa Taifa ambayo itaweka mambo yote sawa (check and balance) bila mifumo hii ni sawa na mziki usio na mpangilio mzuri wa vyombo inakuwa ni fujo.

Wananchi ------> Check and Balances <-----------President

Checks and Balances
= Principle of government under which separate branches are empowered to prevent actions by other branches and are induced to share power. Checks and balances are applied primarily in constitutional governments.
 
Mifumo huundwa na wananchi, hivyo wananchi imara vivyo hivyo mifumo.
Tatizo kubwa ni raia kufikiria kuwa kuna watu wa kuwajengea nchi yao.
 
Nchi imepata marais 6 tangu ipate uhuru, mbona bado tuko hovyo? Ina maana kati ya marais 6 hakuna aliyekuwa na sifa hizo ulizotaja?
Huko nchi fulani mimi sijui hata ni wapi nasikia alitokea mmoja, ila inasemekana wakamuua. Na wenzie wawili waliofanana nae kiitikadi na kiimani pia 'wamekufa'. Ila hao legelege, wavivu na mafisadi bado wako hai, cha kushangaza ni wote wanatokea pwani ya nchi hiyo, na kwa imani wote ni wavaa kanzu! Labda ni coincidence tu!!
 
Unafikirisha Sana we jamaa!!

Unataka nianze kuona aibu kuvaa kanzu!!kama ni hivyo na hao waliobaki hawapaswi kuishi!!

Nimeumia
 
Tutagundua HATA BAADA YA KUMALIZA KUNYWA MTORI CHINI KUNA MIFUPA TU.
Nimekusoma vizuri sana mkuu 'Komeo Lachuma'.
Na huu mstari mmoja ulioamua kuutumia kuhitimisha mada yako ukanifikirisha.
Ni akina nani hawa watakaokutana na "mifupa tupu" huko chini?

Hivi kuna watakaokutana na "maminofu" huko chini?

Pengine hawa wa kundi la pili nao utawasikia hivi karibuni, kama huwasikii kila siku wakiimba nyimbo zao kupitia kwenye kumbi hizi na kwingineko!

Naomba uniunganishe kwa hilo kundi la "wala mifupa".
Kuna watu husema mifupa ndiyo yenye supu kali!

Lakini naomba nieleweke: sitaki kulialia. Nitauma meno na kutazama mbele kwa matumaini ya Tanzania yetu yenye neema kwa waTanzania wote.

Hawa wanaokula kwa urefu wa kamba zao, kuna siku kamba zitageuka na kuwa minyororo shingoni mwao wasiyoweza kuikata.
 
Back
Top Bottom