Kweli ndoa ngumu, binti anataka kuolewa na boda boda

Kazi ya kuendesha boda boda ni kazi km zilivyo kazi nyingine, mi sioni tatizo kikubwa ni kuishi kwa amani na upendo.
 

Kipindi naanza mahusiano na mwanamke ambaye kwa sasa ni mke wangu, alinikuta namalizia chuo baadae nikawa saidia fundi kwenye site za ujenzi.

Maisha ni siri wakuu Mungu ana nguvu sana, tuheshimu watu wote bila kujali wanacho au hawana
 
Kwani kabaka? Kama wameridhiana shida yako nini? Wanaume wengine wapo na mambo yao,wewe unasikilizia maongezi ya wa wanawake! Af unayaleta JF. Hii tabia ya wanawake uswahilini,ila uzuri yanaishia huko huko hayaletwi mtandaoni.

Huyo pisi kali wakati anachagua boda boda si ulikuwepo?
 
Yote matokeo mungu ndio mtoaji, Kuna mzazi anayependa mwanae aolewe na boda boda au saidia fund, au deiwaka yoyote yule, lazima mzazi kwanza akuoji japo baadaye utaeleweka tu, na yakikushinda Maisha utaambiwa si tulikuambia.
 
Bodaboda mmoja alinichana kua ata akiamka saa sita mchana akakomaa adi saa mbili usiku hakosi 50K per day. Per month hio ni 1.5M na hapo ameamka mchana, na hapo bado hatuja jumlisha dili za hapa na pale. Tu assume anaingiza 2M per month, huo ni zaidi ya mshahara ya watu wengi sana walioajiriwa. Usione bodaboda wanapendwa sana na wanawake unabaki kujiuliza kwanini na kukuna kichwa!
 

Kuna aina ya kazi ni risk kwa Muolewaji..

Ajiandae kuwa Mjane
Ajiandae kuuguza Mume mara kwa mara..

Ni ukweli Mchungu.
Acha ukuda mkuu

Nenda viwandani ukajionee hakuna Kazi isiyo na changamoto ,kitu muhimu ni kufanya kazi kwa adabu ni jambo muhimu zaidi
 
Aiseee boda ukifanya Kwa malengo inalipa maana Kuna vijiwe mtu kuingiza 30K Kwa Siku kawaida
 
Dume suruali!, Dume Shostito!.., dume mbea mbea!

Kutwa kufatilia mambo ya umbea umbea wa kinamama!

Karibu utavishwa dera!
 
Kwanza si kweli. Lakini ni kazi kama nyingine,akitulia,anafanya mbambo yake na anapatia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…