Kweli nimeamini, ukimfadhili mwanamke usitegemee kwamba atakuja kukusaidia wakati wowote

Kweli nimeamini, ukimfadhili mwanamke usitegemee kwamba atakuja kukusaidia wakati wowote

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Huyu dada alipitia changamoto baada ya kupoteza wazazi na nikaamua kumsaidia. Tukawa na mahusiano kama mwaka mmoja hivi.

Baadae nikamwambia naona tulikutana ili nikusaidie lakini moyo wangu hauko na furaha kuendelea na uhusiano. Aliumia sana japo niliendelea kumsaidia kwa kulipa ada zake chuo.

Miaka zaidi ya saba imepita na tumekuwa tukiwasiliana kawaida kama kaka na dada. Alipomaliza chuo alipata kazi kampuni kubwa sana hapa dar na alinitumia meseji nyingi sana kushukuru.

Wiki kadhaa zilizopita nilipata changamoto kwenye biashara zangu na kuna malipo fulani yalichelewa sana kuingia na nikawa natakiwa kulipia baadhi ya huduma kwa haraka.

Kwasababu huwa tunawasiliana nikamtumia ujumbe whatsap kuomba anisaidie 400k (ninafahamu mshahara wake upo kwenye 2.5m). Alisoma ujumbe halafu hakujibu kwa wiki mbili.

Sasa amenijibu kuwa anayo majukumu mengine, nitafute alternative ingawa najua bado hajaolewa.

Nimeanza kuelewa kwanini moyo wangu ulikataa kumuoa.
 
Ulihiari mwenyewe kumsaidia. Sio lazima saana alipe ulichmfanyia. Ndio maana waswahili wakaja na Msemo Tenda wema nenda zako usingoje shukrani. Hata hivyo, kuwa earning ya 2.5 M ni kitu kimoja na kuwa cash always in hand ni kitu kingine. Ninapendekeza muendelee na urafiki n kusaidiana.
 
Sawasawa mkuu. Ila mimi ningekuwa yeye ningefanya kitu kuonesha shukrani. Tunatofautiana na hivyo naheshimu maamuzi yake.
 
Hawa mamburura mnawasaudieje?
Waacheni wateseke, ukiwasaidia wanaona ni kama walistahili.
Hiyo pesa uliyomfadhili ungemfadhili shangazi yako angeacha biashara ya vitumbua na angemiliki duka sasa ukoo ungeinuka zaidi.
Narudia tena.
Waacheni wasaidiane wao kwa wao.
Msaada ni kwa yeyote mwenye uhitaji. Awe ndugu au la.
 
Back
Top Bottom