Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

..tatizo shirika la ndege ni biashara kichaa?

..atcl ina mzigo mkubwa sana wa madeni.

..pia atcl imekuwa ikiingiza hasara mwaka hadi mwaka.

..kwanini hayo matrillion yasielekezwe kwenye sekta zinazogusa Watz wengi mfano kilimo, mifugo, badala yake tunaenda kununua midege toka kwa MABEBERU?
Inawezekana ni moja ya masharti ya kuwa nchi ya uchumi wa chini wa kati.
 
Kuna siku nilisema hapa hii nchi si-ya kuangaika nayo sana, inatia hasira sana,yaani hata ufanye lipi wasio kupenda watakupinga na kutukana wanaokupenda watakushangilia hata ufanye mambo ya kipumbavu.

Magu alinunua ndege 11 akasimangwa kama mbuzi mwenye mapengo kwa wasiompenda, haya na huyu anaendeleza manunuzi hayahaya waleeee watashangilia..ahahahah na wa Magu watapinga ahahahah

Aisee hii nchi bora kula bia, kitimoto, choma nyingi,masamaki kibao bila kusahau mademu tu basi.

Maana Magu alifikia hatua akawa halali kisa mafile yamejazana kitandani kumbe wahuni wanamlia timing ahahahah...

Leo wamekuja na tundege tunne eti kwa 1.7T(what a hell)!!!

Dah! sjui hii viongozi wanafanya maksudiii au huwa wanalazimishwa? Hivi ukitia tilion 1.7 kwenye kilimo si utaleta mabadiliko makubwa sana ya maisha ya watu tena kwa mkupuo? Eti ndege!!! '..stupid cattle, the cattle of Africa by Mampala mng'aiza!
 
Yaani serikali yetu inatumia zaidi ya Trilion 1.7 (pesa taslimu) kutoka kwenye kodi za watanzania ili kununua ndege, halafu inakwenda kuomba mkopo wenye wa riba wa 1.4Trilioni kutoka IMF ili kwenda kujenga shule na hospitali.

Kuna namna viongozi ni mataahira na wamewafanya wananchi kuwa watumwa.
Daah inafikirisha sana
 
Uamuzi wa kulifufua shirika la ndege uliishafanyika na mchakato wake huwa hauishii kwenye kununua ndege moja au mbili, ni mchakato unaohusisha kutambua "Hub" ya shirika, kutambua "Routes" kuziomba na mwisho kuanza ununuzi wa ndege kulingana na makisio ya idadi ya abiria kwenye "Route" zilizoombwa na shirika.

Serekali kununua ndege zaidi ni kitu kilichotarajiwa na bado watalazimika kununua nyingine nyingi tu siku za usoni.

Kununua Boeing 787-8 na 767 freighter ni sahihi kabisa, Ila Boeing 737 Max tena mbili? nadhani wangefikiria mara mbili chaguo hilo maana kuna ndege nyingi za aina hizo ziko "grounded" sababu ya ajali mbili maarufu zilizohusisha ndege hizo.

Kama ningeulizwa nifanyeje kwenye hali kama hii ambapo Tr. 1.7 inahusika hizo Max ningezipiga chini na kuchukua Boeing 777 mbili badala yake au Boeing 787-9 mbili.

Hizo zote kama zikinunuliwa zinabaki kuwa "Assets" za Serikali kama yalivyo madaraja..... Narudia Boeing 737- Max ni sawa na COVID-19....Serikali msiuvae mkenge!!.
 
Hii hela ingejenga interchange la maana Sana pale jangwani. Hii nchi inaviongozi wa ajabu sana.
offset_771279.jpg
 
kuna taarifa kuwa tanzania inapanga kununua ndege zingine 4 aina ya boeing.

hii imekaa je wadau.

katikati ya mgao wa umeme na maji tunawaza kununua ndege?

au ndege ni bei rahisi kuliko umeme na maji?
 
Freighter ndiyo ya muhimu hapo,hayo mapesa mengine Kwa nini wasifungulie bank Kwa ajili ya kuwezesha watanzania wanaotaka kulima mashamba zikatumika kukusanya vijana katika makundi ya vijana 50.

Lengo kutengeneza ajira kutengeneza mazingira bora ya kuvutia vijana kubakia vijijini kukaribisha wawekezaji wa kununua mazao Kwa viwanda vyao
 
Magufuri alishafanya kazi ya kununua ndege 11..sasa ilitakiwa wanunue moja ya mzigo basi..sasa wamenunua max wakati yameuua watu..TunaRais wa ovyo kwa sasa
 
..tatizo shirika la ndege ni biashara kichaa?

..atcl ina mzigo mkubwa sana wa madeni...
Muda mwingine huwa mnashauri kwa kutumia akili za makaratasi/kamasi kabisa.
Trilioni zote hizo ziwekwe kwenye sekta ya kilimo wakati mnaopaswa kulima mmeenda kujazana darisalama kutwa kucha kulalamikia joto la dar.

Zinunuliwe tuu kwani aliyekwambia tuna njaa ya chakula na nyama ni Nani?

Go ahead,nisipozitumia nitaziona na inatosha kujimilikisha kwamba ni zetu.
 
Back
Top Bottom