Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

TTu
Hapa kunaufisqdi... Magufuli kanunua ndge 11 kwa trillion 1.2 harafu hizi ndegenne kwa trioni 1.7...na kwanini wasingesubiri hizo alzinunua magufuri ziendelee kufanya biashara kwanza?
Tumekubaliana tuendeleze kazi za Hayati
 
Freighter ndiyo ya muhimu hapo,hayo mapesa mengine Kwa nini wasifungulie bank Kwa ajili ya kuwezesha watanzania wanaotaka kulima mashamba zikatumika kukusanya vijana katika makundi ya vijana 50,lengo kutengeneza ajira kutengeneza mazingira bora ya kuvutia vijana kubakia vijijini kukaribisha wawekezaji wa kununua mazao Kwa viwanda vyao
Vijana wote wamesoma hamna anaetaka kuchafuka shamban.
 
..737 Max si ndio zilizokuwa zinaanguka mpaka ikapelekea zikafungiwa?
Hizo ndio zitakuwa ndege za kuendeshwa kwa faida kuliko aina nyinginezo. Nchi nyingi duniani zilisharuhusu hii aina na jana hapo China imeruhusu. Lile tatizo lilikuwa kwenye mfumo wa kompyuta na Boeing wamerekebisha, orders zake zishakuwa nyingi.
 
Unatumia $726m kununua ndege halafu unaenda kukopa $937 IMF ya kujenga madarasa na matundu ya choo.

Ubongo wa waafrika huenda uko tofauti na binadamu wa mabara mengine
Kuna agenda nyingine mkuu, siamini kama watu wote hawalioni hili. Watu waliopewa dhamana wana agenda ya siri, si kwa maslahi ya wananchi ila kunufaisha kikundi cha watu flani. Ccm ni ile ile, haijabadilika.
 
Agenda gani hiyo mkuu ?
Hainingii akilini unatumia $726m kununua ndege halafu unaenda kukopa $937m ujenge madarasa na vyoo.
 
Uamuzi wa kulifufua shirika la ndege uliishafanyika na mchakato wake huwa hauishii kwenye kununua ndege moja au mbili, ni mchakato unaohusisha kutambua "Hub" ya shirika, kutambua "Routes" kuziomba na mwisho kuanza ununuzi wa ndege kulingana na makisio ya idadi ya abiria kwenye "Route" zilizoombwa na shirika.

Serekali kununua ndege zaidi ni kitu kilichotarajiwa na bado watalazimika kununua nyingine nyingi tu siku za usoni.

Kununua Boeing 787-8 na 767 freighter ni sahihi kabisa, Ila Boeing 737 Max tena mbili!!???... nadhani wangefikiria mara mbili chaguo hilo maana kuna ndege nyingi za aina hizo ziko "grounded" sababu ya ajali mbili maarufu zilizohusisha ndege hizo.

Kama ningeulizwa nifanyeje kwenye hali kama hii ambapo Tr. 1.7 inahusika hizo Max ningezipiga chini na kuchukua Boeing 777 mbili badala yake au Boeing 787-9 mbili.
Hizo zote kama zikinunuliwa zinabaki kuwa "Assets" za Serikali kama yalivyo madaraja..... Narudia Boeing 737- Max ni sawa na COVID-19....Serikali msiuvae mkenge!!.
Waliozifungia 737 Max ndio hao hao wanezifungua. Achana na mamlaka za anga za Marekani na Ulaya zenyewe ndio kila kitu kwenye usafirishaji wa ndege duniani. Wakizuia ndege ndio wewe utakuja jua ina shida, wakifungua ndege ndio utaweza jua inafaa kwa matumizi.

Boeing nao sio wapumbavu kuharibu shares zao kwenye masoko ya hisa wazirudishe ndege hizi bila kufanyia marekebisho hizo softwares zilizoleta shida. Hizi ndege watu wanazikimbilia uko na orders zake zimeielemea Boeing wewe unasema ni mbovu. Mpaka sasa sijaona ni ndege gani itakuwa na orders nyingi zaidi ya hii aina, maonesho yanaisha keshokutwa
 
..mna uhakika gani na hizo watakazotuletea?
Mimi si mnunuzi ila serikali. So kwanza nitoea hapo kwenye "mna" wkt sihusiki na manunuzi yoyote.
Pili hiz ndege zilikuwa grounded march 10, 2019 baada ya kupata matatizo ya mfumo wake. Boeing wamefanya marekebisho badala. May 23 2020 ziliruhusiwa kuruka tena.

Walipata permission from FAA,ICAO. Ndege yoyote haiwez kutoka kiwandani na kuruka au kutumika na mteja bila vibali vya hao watu. Na kuna regulation bodies nyingi tu huko. So ni ndege zote ziko regulated
 
Unatumia $726m kununua ndege halafu unaenda kukopa $937 IMF ya kujenga madarasa na matundu ya choo.

Ubongo wa waafrika huenda uko tofauti na binadamu wa mabara mengine
Watakuja kulaumu mabeberu hawawapendi. Mabeberu wanataka kuwahujumu. Kumbe tunajihujum wenyewe
 
..tatizo shirika la ndege ni biashara kichaa?

..atcl ina mzigo mkubwa sana wa madeni.

..pia atcl imekuwa ikiingiza hasara mwaka hadi mwaka.

..kwanini hayo matrillion yasielekezwe kwenye sekta zinazogusa Watz wengi mfano kilimo, mifugo, badala yake tunaenda kununua midege toka kwa MABEBERU?
Mkuu CCM ni wagonjwa wa akili, unadhani hilo Boya litakuelewa?
 
Waliozifungia 737 Max ndio hao hao wanezifungua. Achana na mamlaka za anga za Marekani na Ulaya zenyewe ndio kila kitu kwenye usafirishaji wa ndege duniani. Wakizuia ndege ndio wewe utakuja jua ina shida, wakifungua ndege ndio utaweza jua inafaa kwa matumizi.

Boeing nao sio wapumbavu kuharibu shares zao kwenye masokobya hisa wazirudishe ndege hizi bila kufanyia marekebisho hizo softwares zilizoleta shida. Hizi ndege wetu wanazikimbilia uko na orders zake zimeielemea Boeing wewe unasema ni mbovu. Mpaka sasa sijaona ni ndege gani itakuwa na orders nyingi zaidi ya hili aina, maonesho yanaisha keshokutwa
Mimi sijasema popote kuwa ni mbovu na wala sina mamlaka wala msingi wa ubovu wake, kilicho wazi na cha uhakika ni kwamba hizo ndege ziko grounded, na Boeing wanahaha kuzirudisha kwenye chati. Mashirika mengi ya ndege yanachagua kuchukua 737 NG hizo Max bado hata wanahisa wana wasi wasi nazo!
Kama tunanunua, hatupewi bure mimi kama mlipakodi na mdau kwenye usafiri wa ndege nina haki ya kutoa angalizo kwa shirika letu la ndege, kuwa wawe makini kwenye hili..... Naamini kuna kipengere cha marekebisho kwenye mkataba wa manunuzi.
 
Waliozifungia 737 Max ndio hao hao wanezifungua. Achana na mamlaka za anga za Marekani na Ulaya zenyewe ndio kila kitu kwenye usafirishaji wa ndege duniani. Wakizuia ndege ndio wewe utakuja jua ina shida, wakifungua ndege ndio utaweza jua inafaa kwa matumizi.

Boeing nao sio wapumbavu kuharibu shares zao kwenye masokobya hisa wazirudishe ndege hizi bila kufanyia marekebisho hizo softwares zilizoleta shida. Hizi ndege wetu wanazikimbilia uko na orders zake zimeielemea Boeing wewe unasema ni mbovu. Mpaka sasa sijaona ni ndege gani itakuwa na orders nyingi zaidi ya hili aina, maonesho yanaisha keshokutwa
Taarifa za kuruhusiwa hizo ndege zilipokelewa kwa tahadhari kubwa na kama zipo chache zilizoanza kuruka zitakuwa kwenye mashirika ya ndege ya Marekani. Kwa mashirika nje ya Marekani bado wateja wanazitilia shaka.... Sasa sisi ndio tununue mbuzi kwenye gunia?

Ushauri wangu, kama ikiwezekana wanunue hiyo B787 na B767 freighter. Hizo Max zisubiri.. mbona tuna Airbus nne?.
 
Mimi si mnunuzi ila serikali. So kwanza nitoea hapo kwenye "mna" wkt sihusiki na manunuzi yoyote.
Pili hiz ndege zilikuwa grounded march 10, 2019 baada ya kupata matatizo ya mfumo wake. Boeing wamefanya marekebisho badala. May 23 2020 ziliruhusiwa kuruka tena.

Walipata permission from FAA,ICAO. Ndege yoyote haiwez kutoka kiwandani na kuruka au kutumika na mteja bila vibali vya hao watu. Na kuna regulation bodies nyingi tu huko. So ni ndege zote ziko regulated

..je, serikali ya Tz ina uhakika kwamba 737 max tutakazoletewa ni salama?
 
Back
Top Bottom