Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

Wastaafu hawapati stahiki zao kutokana na 'watu hawa' kuhujumu fedha zao kununulia mindege isio na faida kwao.
Wanafunzi wanakosa madarasa na madawati kwa matumizi ya hovyo kabisa kama haya!
Cha kusikitisha tunapewa mkopo na WB shs 1.3 trilioni, tunafurahia na kushangilia bila aibu 😵
 
Mkuu hizo ndege zinachagiza ukuaji wa uchumi kwa njia ambayo mimi na wewe hatuioni. Ni rahisi kulalama humu jukwaani lakini kivitendo ndege zinahitajika sana haswa kwenye sekta nzima ya utalii.

Kuna mkataba wa kibiashara umetiwa saini kati ya Ubelgiji na Tanzania. Watalii watafuatwa moja kwa moja Brussels na kuletwa bongo. Kuna mikataba kama hiyo iliingiwa na Tanzania enzi zile za hayati JPM, muda sio mrefu itaanza kufanya kazi.

Ndege zinaifungua Tanzania kuliko aina nyingine ya usafiri. Kumbuka Mama anapigia debe uwekezaji uweze kukua, nchi inavyofunguka ndivyo mzunguko wa pesa unavyozidi kuimarika.
 

..nakuheshimu sana, but I disagree.

..you can not convince me ukizingatia HASARA ambayo Atcl inaliingizia taifa kila mwaka.

..pia hakukuwa na shida kwa watalii kufika Tz kiasi cha kulazimisha tununue ndege zetu wenyewe.

..kama ni suala la kuifungua nchi ningependelea sekta za kilimo na viwanda zipewe kipaumbele kupitia uwekezaji na uwezeshaji mkubwa wa serikali kama huu uliofanyika ktk ununuzi wa ndege.
 
Dah alaf mbona bei kibwa kiasi iko wakati kwa 1.7 unaweza ukapata jumbo jet Airbus 380 za double deck tena mbili na chenchi inabaki
Kama unafikiri zinanunuliwa kwa faida ya nchi na siyo dili la watu wanaozinunua endelea kushangaa.

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
MAX wamesharekebisha ndege zao?? Si ndo hizi ndege walisema software mbovu rubani akibofya POWER ON yenyewe inaenda SLEEPING MODE?
Kaka umeongeza chumvi aisee [emoji846][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Yes walirekebisha na majaribio wakafanya
 
Kaka umeongeza chumvi aisee [emoji846][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Yes walirekebisha na majaribio wakafanya
Chief hizi ndege haziaminiki mkuu. Naambiwa ikiwa juu pilot aki command autopilot yenyewe inaitikia stop engine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…