eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Wewe huna elimu ndio sababu ukaandika uliyo andika!
Ohh mimi mkiristo kabisa!
Kwanza hapo tu! Ni nani aliyekuambia wewe "uwe mkiristo"? Hio si mmebuni tu nyie!
Cha pili ulitegemea huo MFUMO KRISTO UWE NA OFISI HAPO DAR NDIO UUJUE KUWA UPO?
Unajisifu kuwa umesoma halafu unaongea utumbo namna hii!
Eti.mi SIDHANI...bla..bla...bla..!
We kwa akili yako watu wanaishi KWA KUDHANI??
Nyie ndio maana yule MNAFIKI PAULO hakupata tabu kuwa Convince kuwa japo yeye aliuwa mamilioni ya WAKRISTO WA KWELI eti alioteshwa kuwa yeye ni Nabii!
Na nyie mambulula wooote mkamkubali
We kaa na elimu yako ya kata!
Watanzania wengine wenye busara na elimu watafahamh nini kinaongelewa hapa.
Mimi sijakuja hapa JF kutukanana wala kukejeliana...kutoa maoni kwa uhuru. nimekuja kujifunza na kundisha wengine..... ikitokea hukubaliani na maoni yangu bora ukapuuzia tu..... maana kunitukana na hata bila kuelimisha kwa njia inayoeleweka....... haitanifanya nibadili mtazamo na maoni yangu kuhusiana na kitu hicho cha kufikirika ukiitacho eti mfumo kristo..... mara nyingi watu wanakuuliza jinsi mfumo huo ulivyo na unavyofanya kazi..... wewe unaishia kutukana tu ...... tunashindwa kuelewa lengo lako ni nini sasa.
Pia nakumbuka niliwahi kukuambia kuwa lete ushahidi wa kuonesha jinsi Nyerere baba wa Taifa alivyokuwa akiwapendelea wakristo na kuwachukia waislam na kuifanya nchi kuwa ya kikristo... wewe unajibu kwa matusi...
Nilikuambia kuwa nitaleta ushahidi kuonesha Nyerere alipigania nchi kuwa isiyo na dini...secular country... ukatoa kejeli.....
lingine ni kuwa unapenda sana kutoa kejeli kuhusiana na shule za kata.... siyo jambo jema.. kwa maana huo ni mwanzo mzuri wa kuelimisha watanzania...... licha ya changamoto zake...lakini kuna kitu kimefanyika...... mimi kijiji ninachotoka kuna kijana ambaye alisoma shule ya kata sasa anafanya masters pale Ujerumani....... hivyo si vyema kuzibeza...ni mwanzo mzuri, kwani sasa hatuongelei kujenga madarasa....bali kuongeza waalimu.... cha msingi ni kushauri namna ya kuziboresha......
Mwisho ni kuwa dharau, jazba na kejeli hazijengi... na pia Mwenyezi Mungu nina uhakika hafurahishwi nayo.... mbali na yote ukatae usikatae sisi wote ni watanzania tuna shida zile zile.... kama ni magonjwa, ufisadi, ambazo haziangalii imani tulizonazo... cha msingi tupendane woote.... na penye tofauti au matatizo tuzungumze.... kwa hakuna jambo lisilo zungumzika...