Kwenu Viongozi wa Umoja Party

Mbona huwasisitizii kuendeleza uharamia wa marehemu wa kuteka, kutesa, kuwapoteza na kuwabambikia kesi wale wote watakaowakosoa.

Kwa watu wengi wenye kuthamini utu wa mwanadamu, neno Magufuli ni dhihaka dhidi ya ubinadamu. Waende na jina hilo hilo kila mahali, watayapata majibu.
 
Kiuhalisia hayati Magufuli alikua ni kiongozi jasiri na shupavu kweli, lakini hakua na sifa za kuwa Rais.Nafasi ya juu kimamlaka kwa mtu kama yule ilikua ni uwaziri mkuu tu.Yaani juu yake inapaswa kuwa na mtu aliepevuka kwa hekima na maono ya kuvumilia kupishana maono na watu na kukubali kushaurika.

Lakini kiongozi aina ya Magufuli ni mtu mwenye kutumia maguvu mengi hata mahala pasipohitaji maguvu, mwisho wa siku mnaibomoa nchi badala ya kuijenga.Mungu amlaze pema huko alipo maana ametuachia somo kama taifa!!!
 
Bahati mbaya sana Mimi mwenyewe natamani kupata kadi hata leo na sijui ninaipatia wapi.
Kile kingine, utafiti wa TWAWEZA ulionesha kinaungwa mkono zaidi na watu wajinga, hiki huenda itakuja kufahamika baadaye kuwa kinaungwa mkono zaidi na maharamia wanaopenda kuua, kuteka, kupoteza watu. Hiki kitakuwa ni chama cha kishetani kwaajili ya kusimamia na kuendeleza matendo ya ibilisi.
 
Mawazo hayapigwi rungu sikupingi ndugu. Lakini hatuwezi kukihukumu chama ilihali bado hakijaanza kufanya kazi. Fear of unknown ni changamoto kwa wengi hivyo ni kazi ya viongozi kuhakikisha falsafa, itikadi na sera za chama zinaeleweka vyema.
Nakumbuka Mzee Mangula akisema waliteuliwa vijana 75 kuhubiri falsafa ya azimio la Arusha. Vivyo hivyo ni muhimu kwa Umoja party kutumia mbinu hiyo.
 
Siyo jbo la ajabu hata kidogo. Kuna watu wanamkumbuka Dictator Id Amin mpaka leo. Kuna watu, Ujerumani wanamtukuza Hitler mpaka leo.

Shetani yupo, kwa sababu hajawahi kupungukiwa wa kumsujudia.
Ni mtazamo wako lakini ukikaa ukawa huru utagundua kulikuwa na kitu cha ziada kwa JPM
 
Mtaeneza vipi Chama chenu wakati hakuna mikutano?
Kiongozi shupavu anapimwa wakati wa dhiki na mashaka. Uwezo wa kusimamisha chama wakati huu mgumu ni mtihani wa kwanza mgumu na muhimu tuwe mashuhuda
 
Ahsante mkuu,
 
Mwisho wa ccm umekaribia,mwisho wa dhuruma na uporaji umekaribia,
 
Aliyeua demokrasia, kuzuia mikutano ni Magufuli. Labda kabla ya kufariki kwake aliwaachia wosia kuwaambia kuwa amefungulia demokrasia.

Samia kama ataamua amuenzi marehemu, hamtafanya hata kikao cha sebuleni.
Hiki Chama na wafuasi wake ni contradictions tupu

Magufuli aliziba kabisa space ya kisiasa iliyokuwepo Tanzania, na kusema CCM itatawala milele

Licha ya kuzuia mikutano ya vyama, Magufuli alianzisha uhuni mwingi ambao haukuwahi kuwepo kwenye siasa za Tanzania, kuteua makada wa CCM Kama wakurugenzi, kuengua watu kwa vigezo kuwa hawajui kusoma, kutekwa watu wakati wa kurudisha fomu

Sasa kwa Chama chochote Cha upinzani hakiwezi kusema kinamuenzi Magufuli sababu uwepo wake tu tayari una contradict aliyoamini na kuyafanya Magufuli
 
Naona Giza linaenda kutoweka kwenye macho yangu kwa ujio wa UP
 
Kiongozi shupavu anapimwa wakati wa dhiki na mashaka. Uwezo wa kusimamisha chama wakati huu mgumu ni mtihani wa kwanza mgumu na muhimu tuwe mashuhuda
Huu sio wakati mgumu, wakati mgumu ilikuwa 2016-2020 viongozi wa upinzani walivyokuwa wakitekwa na kuuawa
 
Sema kipenzi chako na familia yako.
 
Ndugu,
Ukiamua kuwa huru na mawazo yako utamuona Magufuli katika picha nyingi sana. Kimoja ambacho wote tunakubaliana ni kuwa Magufuli alikua mzalendo na mwenye upendo wa dhati kwa Tanzania. Alihubiri Tanzania yenye maendeleo na aliamini katika watanzania hivyo alipandikiza mbegu ya ujasiri na uzalendo kwetu wote. Sisi tuliobaki tumejifunza mengi na tunaanzia hapo kuhakikisha kweli tunaisimamisha Tanzania ya mfano na mkombozi wa bara la Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…