Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ndugu kwani wewe hofu yako ni ipi ilihali unasema UP haina madhara yeyote kwa chama chenu?
Wapi nimeonyesha hofu kwenye maandishi yangu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu kwani wewe hofu yako ni ipi ilihali unasema UP haina madhara yeyote kwa chama chenu?
Dhalimu ndio aliboresha matendo ya utekaji hapa nchini.Na hii nayo watamlaumu JPM au mama anaupiga mwingi sasa?
Ata ACT Wazalendo cha akina Zitto wakat huo akina nape wanasubiria hatima YaoPokeeni pongezi zangu za dhati kwanza kwa kuwaza na kuamua kutengeneza chama chenye mlengo na falsafa anuia za Hayati na Kipenzi chetu Dr. Magufuli. Hakika mmefanya jambo kubwa nala kutukuka sana.
Pamoja na pongezi zangu nyingi napenda kuwatahadharisha na kuwaasa kuwa makini sana kwa kila hatua mnayoiendea kwa maana dhamana na imani ya watanzania inakwenda kuwekwa juu yenu. Ni ombi langu kwenu kuwa na dhamiri ile ile ya upendo kwa Tanzania na watu wake huku mkijibidiisha kwa kila namna kuhakikisha Tanzania inapata viongozi wenye kiu na dhamira ya kweli kufikia maono makubwa ya kipenzi chetu Magufuli.
Ni vizuri kufahamu ya kuwa Tanzania ya sasa haina upungufu wa vyama vya siasa au sera nzuri za uendeshaji wa nchi. Hivyo ni budi kwenu kuyasoma na kuyapatia ufumbuzi yote ambayo ni maidhafu ya vyama vya siasa vilivyopo sasa ambavyo vimeshindwa kuonesha dira ya kweli ya Taifa letu kwa miaka 50 hadi 100 ijayo. Magufuli aliipenda Tanzania na kuchukizwa kabisa kwa maneno na vitendo na hali mbaya ya umaskini, ufisadi na dharau ya watawala/mabwenyenye waliojimilikisha nchi dhidi ya tabaka kubwa la watanzania wanyonge.
Ni ombi langu kwenu kutanguliza uzalendo na elimu ya kisiasa kwa watanzania wote wapate kufahamu dira, muelekeo na falsafa za chama. Katika hatua hizi za mwanzo ni muhimu sana kuhakikisha mnatengeneza misingi imara ya kitaasisi kwanza kwa kuhubiri na tena kuonesha kwa vitendo ili watanzania wayaamini hayo mnayapeleka kwao. Pasiwepo na hila midomoni mwenu tena Amani, Upendo,Haki na Mshikamano visipungue katika majukwaa yenu. Njoo na majibu ya namna ambavyo Tanzania itaweza kuendelea kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ni muhimu sana kuzisema changamoto zote na kuueleza uma watanzania ni kwa njia gani tutafikia maendeleo ya kweli. Watafuteni wazee wazalendo wawapatie hekima zao, wapongezeni wanaostahili pongezi, wakemeeni wanastahili makaripio.
Karibuni kwenye ulingo wa siasa za Tanzania, karibuni kwenye figisu za CCM, karibuni kwenye hila za CHADEMA, karibuni kwenye kichaka cha wahuni na watakatishaji wa udhalimu.
Umoja ni nguvu, Umoja ni Ushindi, Umoja ni Maendeleo.
Nyinyi wanazi wa dikteta mwendazake mnafurahia uhuru wa kutoa maonj na kufanya siasa ambao mama yetu kipenzi ametupatia. Raisi anayejiamini na anayejitambua umetupatia watanzania.Umoja party, walipo tupo!!
Huku ndio kuzikwa pembeni mwa JPM, zitto aipate hii
Maandishi yako yamejaa hofu na uoga mkubwa kwa kitu usichokifahamu hilo liko wazi sana. Mpaka sasa UP haijaweka manifesto yake wazi wala safu yake ya uongozi lakini unakuwa mstari wa mbele kuitabiria vibaya.Wapi nimeonyesha hofu kwenye maandishi yangu?
[emoji106]Kile kingine, utafiti wa TWAWEZA ulionesha kinaungwa mkono zaidi na watu wajinga, hiki huenda itakuja kufahamika baadaye kuwa kinaungwa mkono zaidi na maharamia wanaopenda kuua, kuteka, kupoteza watu. Hiki kitakuwa ni chama cha kishetani kwaajili ya kusimamia na kuendeleza matendo ya ibilisi.
Maandishi yako yamejaa hofu na uoga mkubwa kwa kitu usichokifahamu hilo liko wazi sana. Mpaka sasa UP haijaweka manifesto yake wazi wala safu yake ya uongozi lakini unakuwa mstari wa mbele kuitabiria vibaya.
Tukubaliane jambo moja CCM wameshindwa kuliongoza taifa na tena kuna ombwe kubwa sana la kiuongozi Tanzania. Bahati mbaya zaidi kuna Kuta nene sana kupenyeza mawazo huru kwenye vyama vya siasa vyenye muelekeo wa kushika Dola. Hivyo ni lazima kwa manufaa ya Tanzania ya leo na kesho kuwa na msingi mpya wenye muelekeo wa maendeleo ya kisasa na fikra za kujitegemea kama ilivyo shauku ya watanzania wote.
Wamemaliza kazi ya kulisimamisha taifa (CCM) Sasa ni muda wa UP kuleta maendeleo ya kweli kwa watanzania wote.
Pamoja kwenye Umoja Bwana Tindo
Amani iwe nawe
Nacho kitakuwa kinateka na kuua kama mwendazake?Umoja party, walipo tupo!!
Huku ndio kuzikwa pembeni mwa JPM, zitto aipate hii
Ccm na chadema walishamkataa JPM na kazi zake zoteNadhani Yale yote mema ya JPM yataendelezwa na CCM ama Chadema ama chama chochote.Muhimu ni kuweka mifumo na taasisi imara.
Wew hujui kitu hata sifa za kiongozi huzijui unazungumzia siasa za uongo uongo yule alikuwa reformistKiuhalisia hayati Magufuli alikua ni kiongozi jasiri na shupavu kweli, lakini hakua na sifa za kuwa Rais.Nafasi ya juu kimamlaka kwa mtu kama yule ilikua ni uwaziri mkuu tu.Yaani juu yake inapaswa kuwa na mtu aliepevuka kwa hekima na maono ya kuvumilia kupishana maono na watu na kukubali kushaurika.
Lakini kiongozi aina ya Magufuli ni mtu mwenye kutumia maguvu mengi hata mahala pasipohitaji maguvu, mwisho wa siku mnaibomoa nchi badala ya kuijenga.Mungu amlaze pema huko alipo maana ametuachia somo kama taifa!!!
Magufuli hakuamini uhuni wa vyama vya upinzani lakini watu makini waliokuwa upinzani aliwateua katika nyazifa mbalimbaliWazo kuu la Magufuli hakuamini katoka vyama vingine tofauti na CCM
Chadema haitakuja kuaminika tena kamweMmeichoka ccm Wakati ndio imewaanzisha, au unadhani tutapotea maboya kirahisi hivyo? Hii mbinu ya kuanzisha chama na kuja na gia hizo ccm ilifanikiwa zamani, kwa sasa tunawachora tu.
Yanaweza kulipeleka taifa mbele kwa speed ya mara 10 zaidi ya ilivyo sasa just kukiwa na check and balances!Ni mjinga anayeweza kuamini kuwa mrengo wa mawazo ya Magufuli yangelifikisha Taifa hili mbali. Endeleeni kujifurahisha!
Chadema haitakuja kuaminika tena kamwe
Hivi ni kitu gani cha ziada kinakuwepo katika kuua au kupoteza watu, au kuwashambulia wanaokukosoa. Au hata kuwagunga watu kwa kuwaonea?Ni mtazamo wako lakini ukikaa ukawa huru utagundua kulikuwa na kitu cha ziada kwa JPM
Ni wato wenye upeo mdogo ndio wanaoamini kiwa sera za marehemu zingetufikisha popote. Kama anageishi zaidi, watu wanaochelewa kuelewa ndiyo wangetambua uhovyo wa sera zake ambazo zingezidi kulididimiza Taifa katika kila nyanja ya maendeleo.Ni mjinga anayeweza kuamini kuwa mrengo wa mawazo ya Magufuli yangelifikisha Taifa hili mbali. Endeleeni kujifurahisha!
Upo sahihi sana. Ndiyo maana naamini kuwa waanzilishi wa hiki chama, ama watakuwa ni wanafiki sana, au wana upeo mdogo sana.Hiki Chama na wafuasi wake ni contradictions tupu
Magufuli aliziba kabisa space ya kisiasa iliyokuwepo Tanzania, na kusema CCM itatawala milele
Licha ya kuzuia mikutano ya vyama, Magufuli alianzisha uhuni mwingi ambao haukuwahi kuwepo kwenye siasa za Tanzania, kuteua makada wa CCM Kama wakurugenzi, kuengua watu kwa vigezo kuwa hawajui kusoma, kutekwa watu wakati wa kurudisha fomu
Sasa kwa Chama chochote Cha upinzani hakiwezi kusema kinamuenzi Magufuli sababu uwepo wake tu tayari una contradict aliyoamini na kuyafanya Magufuli
Uharamia na ukatili siyo sehemu ya uzalendo.Ndugu,
Ukiamua kuwa huru na mawazo yako utamuona Magufuli katika picha nyingi sana. Kimoja ambacho wote tunakubaliana ni kuwa Magufuli alikua mzalendo na mwenye upendo wa dhati kwa Tanzania. Alihubiri Tanzania yenye maendeleo na aliamini katika watanzania hivyo alipandikiza mbegu ya ujasiri na uzalendo kwetu wote. Sisi tuliobaki tumejifunza mengi na tunaanzia hapo kuhakikisha kweli tunaisimamisha Tanzania ya mfano na mkombozi wa bara la Africa