Kwenu Viongozi wa Umoja Party

Ata ACT Wazalendo cha akina Zitto wakat huo akina nape wanasubiria hatima Yao
 
Umoja party, walipo tupo!!

Huku ndio kuzikwa pembeni mwa JPM, zitto aipate hii
Nyinyi wanazi wa dikteta mwendazake mnafurahia uhuru wa kutoa maonj na kufanya siasa ambao mama yetu kipenzi ametupatia. Raisi anayejiamini na anayejitambua umetupatia watanzania.

Kumbukeni dikteta wenu alizuia wengine kufanya siasa na kutoa maoni...akabaki yeye tu.
 
Wapi nimeonyesha hofu kwenye maandishi yangu?
Maandishi yako yamejaa hofu na uoga mkubwa kwa kitu usichokifahamu hilo liko wazi sana. Mpaka sasa UP haijaweka manifesto yake wazi wala safu yake ya uongozi lakini unakuwa mstari wa mbele kuitabiria vibaya.
Tukubaliane jambo moja CCM wameshindwa kuliongoza taifa na tena kuna ombwe kubwa sana la kiuongozi Tanzania. Bahati mbaya zaidi kuna Kuta nene sana kupenyeza mawazo huru kwenye vyama vya siasa vyenye muelekeo wa kushika Dola. Hivyo ni lazima kwa manufaa ya Tanzania ya leo na kesho kuwa na msingi mpya wenye muelekeo wa maendeleo ya kisasa na fikra za kujitegemea kama ilivyo shauku ya watanzania wote.
Wamemaliza kazi ya kulisimamisha taifa (CCM) Sasa ni muda wa UP kuleta maendeleo ya kweli kwa watanzania wote.
Pamoja kwenye Umoja Bwana Tindo
Amani iwe nawe
 
[emoji106]
 

Nimecheka kwa nguvu, eti nina hofu, hofu niipate toka kwa hilo tawi la ccm. Bado mnaamini mnaweza kuvuta watu kwa mitazamo na mipango ya kiccm? Ngoja muingie uwanjani ndio mtajua kizazi kimeshabadilika.
 
Wew hujui kitu hata sifa za kiongozi huzijui unazungumzia siasa za uongo uongo yule alikuwa reformist
 
Mmeichoka ccm Wakati ndio imewaanzisha, au unadhani tutapotea maboya kirahisi hivyo? Hii mbinu ya kuanzisha chama na kuja na gia hizo ccm ilifanikiwa zamani, kwa sasa tunawachora tu.
Chadema haitakuja kuaminika tena kamwe
 
Ni mjinga anayeweza kuamini kuwa mrengo wa mawazo ya Magufuli yangelifikisha Taifa hili mbali. Endeleeni kujifurahisha!
Yanaweza kulipeleka taifa mbele kwa speed ya mara 10 zaidi ya ilivyo sasa just kukiwa na check and balances!

Mnakimbilia kudhoofisha alichofanya Magufuli kwa sababu alikuwa kiongozi wa chuma kwa ku sabotage mazuri yake yote kwa mabaya machache.

Ndio alikuwa bold ila tukumbuke maendeleo yoyote hayaji kirahisi hata maendeleo binafsi hata hao matajiri unaowaona walipitia session za ukatili sana kufikia hapo walipo leo. Ndio iko hivyo sababu maisha ni vita mkuu.

Hata wewe ili kufika ulipo kuna watu ilikuwa lazma uwashinde ama kwa juhudi au kwa hila ili uonekane bora na upate nafasi zaidi. You can not escape from that reality. Sasa ni nini kinakufanya umuone Magufuli ni monster wakati unaishi katika uhalisia huo huo
 
Ni mtazamo wako lakini ukikaa ukawa huru utagundua kulikuwa na kitu cha ziada kwa JPM
Hivi ni kitu gani cha ziada kinakuwepo katika kuua au kupoteza watu, au kuwashambulia wanaokukosoa. Au hata kuwagunga watu kwa kuwaonea?

Muuaji, hata afanye nini, siamini kama huyo anaweza kuwa mtu mzuri kwa kipimo chochote kile.

Hicho chama, kama kweli kitaenda kwa wananchi kuwa kipo akwaajili ya kuenzi yale maovu ya marehemu, hakika kuna maeneo kitatemewa hata mate.
 
Ni mjinga anayeweza kuamini kuwa mrengo wa mawazo ya Magufuli yangelifikisha Taifa hili mbali. Endeleeni kujifurahisha!
Ni wato wenye upeo mdogo ndio wanaoamini kiwa sera za marehemu zingetufikisha popote. Kama anageishi zaidi, watu wanaochelewa kuelewa ndiyo wangetambua uhovyo wa sera zake ambazo zingezidi kulididimiza Taifa katika kila nyanja ya maendeleo.
 
Upo sahihi sana. Ndiyo maana naamini kuwa waanzilishi wa hiki chama, ama watakuwa ni wanafiki sana, au wana upeo mdogo sana.

Huwezi kufanya kitu ambacho unasema unamuenzi mtu ambaye yeye hakukitaka kabisa.
 
Uharamia na ukatili siyo sehemu ya uzalendo.

Alichokuwa anakifanya Magufuli, hakina tofauti na kile alichokifanya fashisti Stallin, aliyekuwa Rais wa Urusi, ambaye alikuwa kiongozi muuaji aliyekuwa akiimba kila siku kuwa anayepingana naye, amekosa uzalendo.

Madikteta wengi, hujificha kwenye neno uzalendo. Anaua watu kwa kisingizio kuwa eti wale wanaomkosoa wamekosa uzalendo. Anafungia vyombo vya habari kwa kudai vyombo hivyo vimekosa uzalendo.

Magufuli, bila ya kumtaja kama mtu aliyekuwa katili, dikteta, mwongo aliyehubiri tofauti na kilichopo moyoni mwake na anayetenda, na sisi tutakuwa ni wanafiki. Magufuli hata apambwe vipi, kuna siku ambayo uovu wake wote utawekwa wazi, na watu watabakia midomo wazi, na jina hilo litakuwa likitajwa kwa ubaya zaidi kuliko kwa mema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…