Kwenu Viongozi wa Umoja Party

Na hii nayo watamlaumu JPM au mama anaupiga mwingi sasa?
Uovu ukipandikizwa katika nchi, huchukua muda kupotea kabisa. Tabia hizi za kinyama, marehemu alizipa nguvu sana, hata zikaota mizizi. Haziwezi kuondoka kwa siku moja.
 
Ni mjinga anayeweza kuamini kuwa mrengo wa mawazo ya Magufuli yangelifikisha Taifa hili mbali. Endeleeni kujifurahisha!
Taifa litafika mbali kwa kuendekeza KAZI NA BATA ???!!!
 
MAGUFULI ALICHUKIA "KATIBA MPYA" HIVYO HICHO CHAMA HAKITUFAI WANANCHI TUNATAKA CHAMA KINACHOPIGANIA UPATIKANAJI WA "KATIBA MPYA" ILI TUONDOKANE NA HII KATIBA YA CHAMA YA KIFALME

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana Urusi IPO hapo ilipo Leo ! Hali kadhalika kwa Mao tze Tung wa China ! Watu walikuwa wanatayarishwa wawe wazalendo wa kweli na askari hodari wa kuijenga na kulinda taifa lao !! Taifa imara haliwezi kujengwa kwa KAZI NA BATA !! Ndio maana bara la Africa lipo nyuma kimaendeleo kuliko mabara yote Ulimwenguni pamoja na rasilmali zote zilizopo !! Akili zetu tumezielekeza kwenye KAZI NA BATA !! unayajua ma Vieite wewe ???!!! Tutasubiri sana !!!
 
Maneno unayoongea mtu anaweza fikiri labda kulikuwa na vita mfano Hii ya Urusi na Ukraine, yaan unaweza kudhani kulikuwa na kitu kikuuuubwa kibaya wakati wa uongozi wa huyo
u kipenzi cha Watanzania JPM Kumbe ni katika kushughulikia wahuni, wazembe , kuondoa takataka zilizofoji vyeti kazini, kusimamia miradi ikamilike kwa ubora na gharama nafuu, kubana matumizi na kuzuia safari za kisengesenge.

Pole sana kama ulikuwa mhanga, nachojua ni kwamba hata nyumbani kwako ukiwa na mtoto mtukutu unapojaribu kumnyoosha anaweza kukimbilia mtaani akawaacha wenzake waadilifu, Hatuwezi kushangilia utepetevu kama huu unaoendelea unaowafurahisha ninyi na ndo maan UP ni suluhisho
 
Tunataka tuende njia kama ya USA na George Washington.
 
Yaani mnakinasibu kuwa kitakuwa ni chama bora kwa sababu kitakuwa na mlengo wa fikra za mtu? Hiyo ni sawa na kuweka rehani akili zenu. Kwa mtazamo wa mbali pia inaonekana kitakuwa na sura ya ukanda flani kitu ambacho si afya katika kujenga jamii yenye umojaanye.
 
Wewe ni anti-jpm lakini usije ukaona jamii ya twitter na jf ukafikiri ndiyo Tanzania.....hakuna MTU mwenye akili timamu anayeweza kumlinganisha samia na jpm....magufuli ni wa watanzania na samia ni wa wanufaika.....so if wewe ni mmoja wao endelea kulambiswa asali.
 
Pumbaf uzalendo gani wakati nchi ilikuwa inaliwa kama mchwa?

Kwa ripoti ya CAG inaonyesha kuwa hakujawahi kufanyika ufisadi kama wa awamu ya 5.

Alafu unatuletea ngonjera eti alikuwa na uzalendo na upendo.
 
Hakuna jipya hapo kama kweli mna nia ya kuanzisha chama anzisheni,lakini hiyo kauli mbiu yenu ya kusema mnaienzi au kudumisha legacy aliyoiacha hayati JPM,haitowafikisha popote,sababu ni kwamba mtanzania wa kawaida anaelewa fika kwamba Magufuli alikuwa ni kiongozi wa CCM,na nyie kama mtazinadi sera zake itapelekea kukikuza zaidi CCM,hii itakuwa ni faida kubwa sana kwa wana CCM,mtakuwa mmewapigia kampeni isiyo na malipo.
 
Unajua maana ya fikra wewe?
Dunia inaendeshwa na fikra za wafu kama ulikua ufahamu demokrasia ni zao la fikra za mfu, mpaka kesho uislamu umesimama kwa fikra za Muhammad, ukristo ni zao na muendelezo wa fikra za Yesu, uchina ni zao la fikra za mfu.
Upeo wako ni mdogo inaonekana huwezi kung'amua vitu ndio maana unaushirika na wahuni.
Sasa kaa ukifahamu kwa fikra na falsafa za Magufuli UP Itasimama hakuna wa kuizuia. Tunakwenda kulisimamisha dola ya Tanzania kwa uongozi imara na madhubutu. Tanzania ni nyota na ukombozi wa Africa.
 
Watanzania wote wanajua Magufuli alikua CCM lakini hakujinasibisha na CCM. Mlengo wake siku zote ulikua Tanzania kwanza amefanya juhudi nyingi kupitia CCM lakini hakufanikiwa kwa sababu CCM has been broken beyond repair.
Binafsi ninaona CCM kupitia kwa muasisi wake Baba wa taifa Mwl. Nyerere imefanya kazi kubwa naya kutukuka ya kusimika mizizi ya taifa na kutengeneza misingi imara ya umoja na Mshikamano.
Kwa sasa mahitaji ya taifa ni tofauti kabisa na yale ya kipindi cha ukombozi hivyo yanahitaji fikra tofauti kuvuka kwenye mkwamo uliopo Sasa.
Magufuli alitengeneza blue print na sisi kama wana UP tunakwenda kiiteleza. Jambo hili litapingwa sana na wote wanaofurahia/kunufaika na hali mbaya umaskini uliopo nchi, wala rushwa, wahujumu uchumi, wapiga madili na wenye vyeti feki, wabadhirifu na wahuni wote.
Lakini yeyote mwenye nia njema hakika hawezi acha kuunga mkono harakati za UP.

Umoja ni Nguvu, Umoja ni Upendo, Umoja ni Maendeleo.
 
Unazungumzia kitu ambacho huna uelewa wa ndani. Uchumi wa China umeshikiliwa na mataifa ya Magharibi. Tafuta kwenye orodha ya makampuni makubwa kabisa 10 ya nchini China, niambie ni mangapi yanamilikiwa na wachina/China. Unaelewa kilichofanyika nchini China miaka 2000 kilichosababisha China yenye uchumi hohe hahe mpaka kufikia ukuaji wa 12% kwa mwaka?

Hivi unajua kuwa katika real development (human development), China ni nchi ya 89, ikizidiwa na nchi kama Botswana? Usione wachina wanazurura Duniani kote, ukadhani wanapenda. Hali zao za kimaisha na duni sana, japo Serikali ina pesa nyingi.

Huko Urusi kuna makampuni zaidi ya 1000 ya nchi za Magharibi. Unafuu wa uchumi wa Urusi, ulikuja baada ya kuachana na Leninism, na kuruhusu uwekezaji wa nje na uchumi huria lakini bado kuna pengo kubwa sana la maendeleo ukilinganisha na nchi kama US, UK, Belgium, Germany, Japan, Italy, Norway, n.k.

Hakuna nchi hata moja ya kidikteta ambayo wananchi wana maendeleo halisi. Urusi ni nchi ya 52 kwenye human development.
 
Upo sahihi sana. Ndiyo maana naamini kuwa waanzilishi wa hiki chama, ama watakuwa ni wanafiki sana, au wana upeo mdogo sana.

Huwezi kufanya kitu ambacho unasema unamuenzi mtu ambaye yeye hakukitaka kabisa.
Wenzako hawawalengi wananchi wenye uelewa,la hasha wanawalenga walalahoi,wanyonge na hohehahe

Wanawalenga watu ambao hawajui kuhoji yanayoendea Tanzania

Wanawalenga watu ambao wana chuki na watumishi wa umma,matajiri na wenye nacho

Hivyo nina uhakika watapata wajinga wengi

Watawapata wanyonge wengi wa Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…