Kwenu Wanaume mnaozaa na michepuko

Kwenu Wanaume mnaozaa na michepuko

Waungwana na wasio waungwana nawasalimu.
Ninaandika haya nikiwa na masikitiko mengi sana...
Niko kwenye tukio moja la kifamilia ambapo imelazimu watoto wote wa mji husika kuwepo.
Ni tukio kubwa kiasi kwamba hata sisi tusio ndugu tumeshiriki.
Nimeumia kuona katoto ka nje ambako kwa makadirio kalizaliwa wakati baba mwenye mji akiwa tayari ndani ya ndoa kakiwa kwenye mazingira ya uchafu kuanzia mwili hadi mavazi. Mwili umesheheni mapunye ambayo inaonekana kabisa yamekuwa hapo kwa muda mrefu bila huduma. Nywele hazijanyolewa ni kama yule kiumbe wa Gods must be crazy.... nimeumia sana.

Baba na mama wa mji huu wana uwezo mkubwa sana na watoto wengine wapo vizuri kiafya na mengineyo.

Nikawaza ukute mama wa mtoto hajui mazingira haka katoto kanayoishi kwakuwa tu baba mtoto amelazimisha aishi na mwanae kwa sababu za kibinafsi...na sasa mtoto anaishi maisha ya kunyanyapaliwa.

Lakini pia nimeumia kuona mwanamke I mean huyu mama wa kambo kuruhusu huyu mtoto kusafiri umbali mrefu na hali ya uchafu ule huku watoto wake wakiwa smart. Kwa nini ambague ? Hajui kwamba hata yeye anaweza kufa wanae wakalelewa na mama wa kambo? Hata kama amesalitiwa lakini huyu mtoto hana kosa lolote.

Wanaume kabla hamjazaa na michepuko yenu jipimeni na muwe na uhakika kama ki akili mko wazima kiasi cha kuweza kusimama na hawa watoto. Lakini pia punguzeni ubinafsi na kuwatoa hawa watoto kwa mama zao kwa kukwepa gharama za mara kwa mara atakazotaka mama mtoto. Hii ni gharama ambayo lazima muilipe kwa kupambana na matokeo ya starehe zenu.
Mje na matusi mapya

Picha haihusiani na uzi wangu
View attachment 2551083
Asee hii dhambi itamtafuna mtu hapa mtu ameficha haki ya mtu , alafu mtu unakuwa na majanga kibao unaanza kukuuliza nmekosea wapi kumbe umehide haki ya mtu
 
Ndugu yangu na umalaya wake anakwambia kamwe hawezi zaa nje ya ndoa. Maana hatoweza kumsupport mtoto financially wala physically.

Anawaambia wasichana zake kabisa ukija kwangu siku hatari kunitega nikupe mimba utalea mwenyewe.
Muda mwingine ni wanawake tunachemka unafikiri ukibeba mimba ndio utamteka mume wa mtu kumbe unajitafutia ugumu wa maisha ya mtoto wako
💯.
 
Kuna kubadilisha mbegu. Unao mtoto mkali, anazaa watoto wote ni vilaza tu. Hapo unaona unazika vipaji vyako, unaenda nje utafute wa kunusuru uzao wako
Una uhakika gani kwenye ukoo wenu hamna vilaza😂 unakuta wewe ndo chimbuko la vilaza na unaenda kuwaongeza tena huko nje.
Mtoto akiwa na akili ni wa baba ila kilaza ni wa mama au sio😂
 
Hapa tatizo ni umaskini.
Mtoa Mada apambane kuondoa umasikini Mimi Nimelelewa na Mama tu lakini kula kuvaa kusoma shule za maana Ilikuwa uhakika so Umasikini ndo unaondoa Akili yaani nashangaa Sana hapa Tz Mtu anashindwa kulea mtoto mmoja au wawili ambao hata hawana Matatizo yoyote ya kiafya hi nchi yetu masikini kila kitu
 
Sio wote wako irresponsible Kwa watoto wao , wengine wamezaa nje na mtoto wa nje anakuwa treated the Same ni Bora uchukue mtoto kutoka Kwa mama yake akiwa KATIKA umri wa kuanza la kwanza yaan6-7 years na likizo unampeleka Kwa mama yake mwezi mzima inakuwa Haina TATIZO ,ila ukimchukua akiwa 2-5years hapo ndio shida hutokea mara nyingi
 
Ndugu yangu na umalaya wake anakwambia kamwe hawezi zaa nje ya ndoa. Maana hatoweza kumsupport mtoto financially wala physically.

Anawaambia wasichana zake kabisa ukija kwangu siku hatari kunitega nikupe mimba utalea mwenyewe.
Muda mwingine ni wanawake tunachemka unafikiri ukibeba mimba ndio utamteka mume wa mtu kumbe unajitafutia ugumu wa maisha ya mtoto wako
Mngekuwa na akili hizi muda wote dunia isingekuwa na single maza
 
Mtoa Mada apambane kuondoa umasikini Mimi Nimelelewa na Mama tu lakini kula kuvaa kusoma shule za maana Ilikuwa uhakika so Umasikini ndo unaondoa Akili yaani nashangaa Sana hapa Tz Mtu anashindwa kulea mtoto mmoja au wawili ambao hata hawana Matatizo yoyote ya kiafya hi nchi yetu masikini kila kitu
Hivi wewe mbona uko obsessed sana na whatever I post here?
Hivi huwa unasomaga kweli kinachoandikwa ? Hii ni story ya kweli inayohusu family flani na sio story yangu kama unavyolazimiza.
Uko stressed sana tafuta dawa ya tatizo lako kabla haijawa too late. Kwanza mhaya gani huna maisha?
Manyanza huyu vipi ?? Hebu mpatie nasaha za namna ya ku behave kiume.
Hii ni mental case I can't handle.
 
Sasa unarekebisha kwa mkeo unaumiza damu yako? Au kwa vile mtoto ni minor hajui kujitetea?
Na mnavyozungukwa mke anakwambia mlete tu nitalea kumbe lengo lake ni kuepuka ww kuwasiliana na mchepuko na hana Mapenzi na mwanao.

Naongelea source. Ilikuwaje mpaka ukazaa nje? Kwann usinavoid if possible?
 
Ni kweli ila wanaume wengi hutumia nguvu kuiunganisha familia wakiamini wamesolve tatizo kumbe ndio wanazidisha tatizo. Mtoto kupokelewa na mke ni rahisi ila kuishi nae kwa upendo sawa na wanae wa kuwazaa ni changamoto.

Ni kweli ni changamoto. What if linaepukika? What if usizae nje at first place?
 
Unajua wanawake wa ktz wanapenda sana kuzaa sana Yaan yeye ni kuzaa tu ilimradi Kazaa watoto riziki itakuja mbele kwa mbele watoto wanaishia kuteseka

Wengine wanazaa kuwakomoa wake za ndoa
Ndio apate mke mwenyewe hata hajali sarakasi zao mbona atatamani amle huyo mtoto[emoji23]
 
Inatokea pia wanaolewa baada ya wake kuachika ila ni bahati nasibu na kujitesaa mno
Wapo waume za watu wnaatunza watoto wao wa nje sana Ila wachache mno
Ila wanawake wa kitz wanapenda mno kuzaaa hovyo na kila mtu
 
Waungwana na wasio waungwana nawasalimu.
Ninaandika haya nikiwa na masikitiko mengi sana...
Niko kwenye tukio moja la kifamilia ambapo imelazimu watoto wote wa mji husika kuwepo.
Ni tukio kubwa kiasi kwamba hata sisi tusio ndugu tumeshiriki.
Nimeumia kuona katoto ka nje ambako kwa makadirio kalizaliwa wakati baba mwenye mji akiwa tayari ndani ya ndoa kakiwa kwenye mazingira ya uchafu kuanzia mwili hadi mavazi. Mwili umesheheni mapunye ambayo inaonekana kabisa yamekuwa hapo kwa muda mrefu bila huduma. Nywele hazijanyolewa ni kama yule kiumbe wa Gods must be crazy.... nimeumia sana.

Baba na mama wa mji huu wana uwezo mkubwa sana na watoto wengine wapo vizuri kiafya na mengineyo.

Nikawaza ukute mama wa mtoto hajui mazingira haka katoto kanayoishi kwakuwa tu baba mtoto amelazimisha aishi na mwanae kwa sababu za kibinafsi...na sasa mtoto anaishi maisha ya kunyanyapaliwa.

Lakini pia nimeumia kuona mwanamke I mean huyu mama wa kambo kuruhusu huyu mtoto kusafiri umbali mrefu na hali ya uchafu ule huku watoto wake wakiwa smart. Kwa nini ambague ? Hajui kwamba hata yeye anaweza kufa wanae wakalelewa na mama wa kambo? Hata kama amesalitiwa lakini huyu mtoto hana kosa lolote.

Wanaume kabla hamjazaa na michepuko yenu jipimeni na muwe na uhakika kama ki akili mko wazima kiasi cha kuweza kusimama na hawa watoto. Lakini pia punguzeni ubinafsi na kuwatoa hawa watoto kwa mama zao kwa kukwepa gharama za mara kwa mara atakazotaka mama mtoto. Hii ni gharama ambayo lazima muilipe kwa kupambana na matokeo ya starehe zenu.
Mje na matusi mapya

Picha haihusiani na uzi wangu
View attachment 2551083
Screenshot_20230315-113252_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom