Watoto ni kundi la watu wanaoathirika zaidi na matatizo ya kuachana kwa wazazi,kupotea kwa mzazi (kufariki) au kuzaa nje ya ndoa.Mimi ni Mtu mwenye experience ya kuishi na Mama wa kambo, ninafahamu maswahibu yanayowapata watu wa aina yangu.kiufupi ni Wanawake wachache mno wataomlea mtoto wa nje ya ndoa kwa upendo kama wa kwake, wengi wataishia Katika ukatili na unyanyasaji.Pamoja na yote, Mungu amekuwa upande wangu siku zote,na Miaka yote.ila nimejifunza kitu,kimojawapo ni hiki Cha kuzaa na michepuko.Atayeathirika ni mtoto asiye na hatia.