Hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu.
Samson aliendelea kuwa mnadhiri wa Mungu hata baada ya kuzini na malaya. Nadhiri yake iliondoka baada ya kutaja asili ya nguvu zake.
Ni mke wa uzinzi wa Daud (siyo wake zake wa mwanzo) ndiye aliyemzaa Suleman.
Ni mke wa kurithi (siyo wake zake wa mwanzo) wa Boaz ndiye aliyemzaa Yese Baba yake Daud.
Suleman aliomba hekima ya kuwaongoza watu wake kwa haki. Naye Mungu akamjalia hekima, na utajiri pamoja na wake na watoto wengi (je, wake wengi ni baraka au zawadi?).
Wale wasimamao madhabahuni na milangoni mwa hekalu, wao na watoto wao, hawaruhusiwi kufanya ukahaba (je, wengine wanaruhusiwa?).
Ndoa haikuzungumziwa ktk agano jipya bali la kale. Katika agano la kale kuna ndoa tatu kwa kadiri ya torati:
1) Mke mmoja mme mmoja
2) Mme mmoja wake wengi
3) Ndoa ya kubaka. Ukimbaka msichana, mwanaume unaadhibiwa halafu uliyembaka anakuwa mke wako
Kwa kadiri ya biblia, ndoa ni nini? Ni tendo la ndoa, ni hati ya makubaliano au kiapo?
Mwisho wa yote, kumbukeni Mungu hupendezwa na wanyenyekevu kuliko wanaojihesabia haki hata kama matendo yao ni mema. Ndoa ni muhimu lakini siyo hitajio la kuingia mbinguni.
Mitume waliacha wake zao, wakaenda kulitangaza neno la Mungu. Kama ndoa ilikuwa ni muhimu kiasi tudhaniavyo, kwa nini Mungu aliruhusu mitume waache wake zao? Ndoa ni hitajio la Dunia, katika ufalme wa Mungu hakuna ndoa kati ya mwanadamu na mwanadamu bali kati ya Mungu na wanadamu.
Sent using
Jamii Forums mobile app