Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nchi yetu inapitia kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuwepo tangu Taifa liwepo.
Japo kumewahi kuwepo malalamiko mbalimbali kuhusu usalama na haki za watu, lakini hali haijawahi kuwa mbaya kama ya awamu hii.
Kwenye awamu zilizopita, mathalani wakati wa utawala wa Kikwete, Dr Ulimboka alitekwa na kuumizwa vibaya, lakini watekaji walifanya kwa siri, kwa kujificha, walimtesa, na hawakumwua. Na wala Kikwete hakuwahi kutoa kauli kuonesha jambo hilo lilikuwa la kawaida.
Kwenye awamu hii pekee, ndipo tumeshuhudia, mtu anatekwa bila hofu, mbele ya watu wengi, mbele ya polisi, anapelekwa kuteswa, anauawa, halafu kiongozi mkuu wa nchi anatoa kauli kuwa kilichofanyika ni jambo la kawaida, na kwamba kifo ni kifo tu. Yaani Rais anataka kutuaminisha kuwa ukifa kwa malaria, Covid 19, typhoid, na ukiuawa na watekaji, vyote ni vifo tu, hatustahili kuhamaki. Hapo ndipo tulipofikia.
2) Hata awamu zilizopita, kuna watu waliwahi kuitwa vituo vya polisi, wakateswa na hata baadhi walifia vituo vya polisi au hospitalini, baada ya kipigo huko vituo vya polisi. Lakini kuna wakati polisi walipoona mtuhumiwa yupo kwenye hali ya hatari, walimkimbiza hospitali ili wao wasiwe watuhimiwa wa kumwua mtuhumiwa. Yote hayo walifanya kwa sababu walikuwa na hofu ya vitendo vibaya walivyofanya. Lakini awamu hii, mtu anaitwa kituoni polisi, anahojiwa, halafu anapotezwa moja kwa moja, huku watu wakijua kabisa kuwa mtuhumiwa alichukuliwa na polisi, na hao wanaofanya hivyo wanajua kuwa wananchi wanajua, lakini hawana hofu yoyote kwa vile wanajua hakuna wa kuwafanya chochote.
3) Wizi wa kura na vitendo vinavyokiuka misingi ya uchaguzi huru na wa haki, vimekuwepo awamu zote, lakini haijawahi kutokea mtu anatekwa na kujeruhiwa wakati wa uandikishaji wapiga kura, tena uchaguzi wa Setikali za mitaa, ni awamu hii pekee ambayo inaongozwa Samia Suluhu Hassan, tunashuhudia vitendo vya kutisha vya kuteka na kujeruhi wakala wa CHADEMA kwa vile tu mtu huyo alikuwa anazuia hujuma wakati wa uandikishaji wapiga kura. Haya yanatendeka huku Waziri wa TAMISEMI kabla zoezi halijasnza, amekwishatamka kuwa kwenye jimbo lake, kunzia wenyeviti wa vijiji na mtaa, mpaka wajumbe wa serikali, watakuwa ni CCM pekee.
4) Idadi ya wakosoaji wa Serikali na Rais, waliokwishatekwa na kupotezwa mpaka sasa kwenye awamu hii, kwa kadiri ya orodha iliyotolewa na chama cha wanasheria wa Tanganyika, TLS, ni kubwa maradufu ya watu waliowahi kupotezwa katika awamu zote zilizopita.
5) Hapo zamani, wakati wa awamu zilizopita, hata mahabusu waliokuwa wanafia vituo vya polisi, karibia wote, walikuwa watuhumiwa wa makosa ya jinai, lakini awamu hii wanaotekwa, wanaouawa na wanaopotezwa ni wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, watetezi wa uhuru wa maoni, na ama viongozi au viongozi na wanachama wa chama cha upinzani. Hii ni dhahiri kuwa uhalifu huu mkubwa dhidi ya ubinadamu, unafanywa dhidi ya wanaoihoji Serikali na uongozi wa Rais.
6) Awamu ya 5, ya Hayati Magufuli, kama umemkera na anataka kukudhibiti, iwe kwa njia halali au zisizo halali, yeye aliweka wazi kuwa amekuchukia, na wewe mkosoaji utalijua hilo. Lakini awamu hii inaongoza kwa unafiki kwa kiwango cha pekee. Viongozi wanaongelea 4Rs lakini ukija kwenye uhalisia ni kinyume kabisa. 4Rs zinatajwa, bila shaka kuwahadaa wananchi wajisahau, ili waweze kufanyiwa uovu mbaya kwa kabisa, huku wakiwa wamejisahau.
Tuzidi kumwomba Mungu. Nchi yetu ipo kwenye giza nene. Katiba kweli imefanywa ni kijitabu, hakuna mtawala anayeiogopa katiba wala sheria za nchi.
Rais Kikwete, alisema, "......... labda mambo yaharibike sana", sijui anataka yaharibike mpaka ifike hatua gani, ndipo aseme yameharibika sana!!