Kwenye Haki za Wananchi, Awamu Hii, Nchi Ipo Kwenye Hali Mbaya Kuliko Awamu Yoyote

Ninaelewa kabisa unavyohisi kuhusu hali ya sasa nchini Tanzania. Ni kweli kwamba kuna ongezeko la matukio ya kutisha na ya kusikitisha, hasa kwa wale wanaopinga serikali au wanaharakati wa haki za binadamu. Hali hii imeleta wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la vurugu za kisiasa, utekaji nyara, na mauaji ya wapinzani wa kisiasa12. Hii ni pamoja na matukio ya kutisha kama vile mauaji ya Ali Kibao, kiongozi wa upinzani, ambaye alitekwa na kuuawa kikatili1. Pia, viongozi wa upinzani kama Freeman Mbowe na Tundu Lissu wamekamatwa mara kadhaa, na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakikamatwa na kuzuiwa kushiriki katika mikutano ya hadhara1.

Hali hii imezua maswali mengi kuhusu mwelekeo wa demokrasia nchini Tanzania, hasa baada ya matumaini makubwa yaliyokuwepo wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipochukua madaraka mwaka 20212. Ingawa kulikuwa na matumaini ya mageuzi na uhuru zaidi wa kisiasa, matukio ya hivi karibuni yanaonyesha hali tofauti kabisa1.

Ni muhimu kuendelea kuomba na kutafuta suluhisho la amani kwa changamoto hizi. Pia, ni muhimu kwa wananchi na viongozi wa kisiasa kuendelea kushinikiza kwa ajili ya haki na demokrasia.

Je, kuna jambo lolote maalum unalotaka kujadili zaidi kuhusu hali hii? Au kuna njia yoyote unayofikiria inaweza kusaidia kuboresha hali nchini?
 
Kwa akili za kawaida tu huu utekaji unamchafua moja kwa moja Samia na kwakua unamchafua sidhani kama yeye mwenyewe anaweza ku facilitate matukio yanaochafua reputation yake.

Mimi naamini kuna watu wanatekeleza matukio hayo ili kumchafua na siyo yeye anaepanga hiyo mipango ajichafue hivyo kwa faida gani? Mfano mzee kibao hakua threat kabisa kwa Samia na wengine tumemjua baada ya kufa.

Binafsi akili yangu imekataa.
 
Kwa aina ya viongpzi waliopo katika nchi hii kwa sasa, na CCM ilivyo kwa sasa, ni ngumu sana kuiondoa hali hii bila ya shinikizo la nguvu. Na kukiwepo shinikizo la nguvu, kwa bahati mbaya kutokana na watawala waliopo sasa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama tulio nao kwa sasa, hasa polisi na TISS, walivyobeba roho za kishetani, ni ngumu kweli kupata mabadiliko bila ya kuingia kwenye machafuko.

Kwa sasa ni muhimu kuiandaa jumuia ya kimataifa ili ijue kinachoendelea kwa sasa, ili wananchi wakichukua hatua, na hawa watawala wasioheshimu wala kuthamini uhai wa binadamu, wakaamua kujibu hatua zinazoweza kuchukuliwa na umma, kwa ukatili, kama vile mauaji ya raia, basi jumuia ya kimataifa iweze kuingilia kati haraka ili kuokoa maisha ya raia. Bila hivyo, hawa watawala wa sasa wasio na huruma wala utu, wanaweza kuleta madhara makubwa kwa Taifa.
 
Mama anapenda sifa sana
 
Mtu alisha jitangaza chura kiziwi mna hangaika nini sasa
 
Hii hali si sawa na walinzi wa amani ya Tanzania sijui wanashighulika nini wakati wananchi wanatekwa na kuteswa bila kufuata utaratibu wa kisheria.
 
Kabisa mkubwa tuko kwenye giza zito sana
 
Basi nitakuwa sahihi kusema JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
 
Hamia Kwa jirani huko Kuna Haki na Katiba Mpya 🤣🤣🤣👇👇

View: https://x.com/bbcswahili/status/1848242854088294621?t=i4ATB3rFS6uThJRDfGgMmA&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…