Kwenye haya Maisha kuna watu ni untouchable , hii nimejifunza kwa njia ngumu.

Kwenye haya Maisha kuna watu ni untouchable , hii nimejifunza kwa njia ngumu.

Na kama wewe pia umeumiza wengi, kuna madhara yoyote yaliyokukuta
Hakuna mkamilifu, nakosea na huwa naomba samahani nikijua nimekosea mimi. Kuna mazuri na mabaya maishani. Ila huwa naogopa kumfanya mtu aumie sana na kulia. Sababu najua maumivu yake, mimi mtu nikimfanya ajisikie wa thamani, mwenye furaha ndiyo kitu napenda. Ila usivuke Red line.
 
Nilichojifunza sio kila mtu anagusika .

Kuna jirani yetu ukimjaribu basi lazima mpoteane .

Nilimfata na kumuuliza inakuaje kila anayetaka kukufanyia ubaya au anayekufanyia anapoteana

Alinijibu kuwa hiyo hata yeye hajui na wamezikwa watu wengi na kupoteana tangia zamani.

Mimi mwenyewe najiuliza hii ni nguvu ya aina gani? Kila anayekujaribu anapoteana?.
Meneja masoko wa mganga wa kienyeji hapa anatafuta wateja.
 
Hee usiombe kinarudi kwa mtu anayempenda kwenye familia au kwake. Mmoja alilia na kupiga magoti kwa aliyotenda. Maana dada yake ndiyo alitendewa vilevile. Nilimsamaehe na yakaisha pia kwao.
Maybe
 
Mimi ukiniibia nikakusamehe umeisha.
Maisha yako yataharibika sana au utakufa kabisa.
Bora nisikusamehe.

Wapo waliishia jela kwa wizi, familia kuvurugika au kuishia jela kwa kuuwa. Kuna walio kufa ghafla, n.k.
 
Baba angu mzazi ( R. I. P) alikuwa na hiyo nguvu pia.
Sisi kwenye ukoo wetu huwa hatuibiwi, haturogwi wala kudhulumiwa.
 
Kuna wakati, nikiwa kijana kabisa, nikiwa nimetoka kumaliza masomo ya chuo kikuu, na ikumbukwe kabla ya kumaliza chuo nikiwa nimetoka likizo, nilisurika kwenye ajali mbaya kabisa ya basi lililogongana na lorry na kisha kushika moto, na watu wengi kupoteza maisha. Baada ya kumaliza masomo, nilipata kazi, nikaenda fieldwork vijijini ndani kabisa huko Dodoma nikiwa na gari na hema.

Nilikosa nyumba ya kupanga na hapakuwa hata na guest house. Nikaupata mti mmoja, mbuyu mkubwa sana wenye kivuli kikubwa, na chini hakuna nyasi kabisa, nikaweka hema langu chini ya huo mti. Kama ilivyo kawaida yangu, kila siku kabla ya kulala, nilipiga magoti kumshukuru Mungu na kuomba mwongozo wake. Niliishi bila kuona kitu chochote kisicho cha kawaida.


Siku moja, mtu mmoja akaja akiniomba nimsaidie kwa sababu mke wake amerogwa, alisema mengi. Kwa kweli nilichukia, kwa nini afikirie kuwa mimi naweza kumsaidia kwenye mambo ya kurogwa, nami sijawahi kujishirikisha katika ushirikina katika maisha yangu yote? Nilipomkatalia, aliendela kunibembeleza. Alipoona nimechukia na nazidi kumwuliza kwa nini anafikiria mimi naweza kumsaidia kwenye ushirikina?
Akasema kuwa pale kwenye mbuyu mkubwa nilipoweka hema, wachawi wote wa kanda ile ndipo huwa wanakutanikia, lakini tangu nimeweka hema langu, hakuna anayeweza hata kusogea. Akadai kuwa kuna mchawi kiongozi wa eneo hilo, yeye alilazimisha kusogelea lakini nilimpiga na kitu cha ajabu, na tangu siku hiyo ni mgonjwa, hajaweza hata kuamka kitandani. Akasema kuwa hapo kijijini pao, kwenye vilabu vyao vya pombe, hiyo imekuwa habari kubwa inayozungumzwa, na watu wamekuwa wakisema kuwa mwamba huyo wa uchawi amekutana na kiboko yake, wakimaanisha ni mimi!

Nilipuuza na kuona hiyo habari nzima ni ujinga, upuuzi na uwongo mkubwa.

Ilikuwa ni kawaida yangu, nikitoka kwenye shughuli zangu, mara nyingi kwenda kanisani, nakutana na paroko kwa mazungumzo ya kawaida, maana ndiyo kampani ambayo niliweza kuendana nayo. Safari hii nilipoenda, nikamweleza juu ya habari hiyo niliyoambiwa, nikimsisitizia kuwa fikra za kishirikina zimeifanya ile jamii ya pale kuwa wajinga. Paroko alinishangaza aliposema kuwa eti hicho wanachoongea huenda ni kweli. Nikamkatalia kuwa ni uwongo kwa sababu mimi sina kabisa hizo nguvu za giza. Lakini Paroko akaniambia, siyo wewe bali kuna watu Mungu huwalinda, nguvu za giza haziwezi kuwasogelea. Nikasema kuwa kama ni kwa mantiki hiyo, siwezi kukataa.

Pia nilipokuwa huko usukumani vijijini nikitimiza wajibu wangu, niliposhinda mgogoro uliokuwepo, wakatamka hadharani kuwa wameshindwa kwenye sheria lakini hawawezi kushindwa katika nguvu zao za kishirikina, nikawaambia waniroge hata muda huo huo, na hakukuwahi kutokea chochote.

Nilipokuwa Sekondari, kuna mganga wa kienyeji alipanda juu ya boneti ya gari ya rafiki yangu, nikamshusha kwa nguvu kwa kumvuta. Akaanza kupiga kelele kuwa, umenivuta mimi, tutaona, nisilaumiwe. Sikujali. Baadhi ya watu waliokuwepo pale, watu wazima wakaja kunisihi, nikamwombe msamaha yule mzee maana ni mchawi sana, mimi nikawaambia kuwa kama ni kufa kwaajili ya haki yangu, basi wacha nife. Hakuna chochote kilichotokea.

Kuna wakati tukiwa porini tunafanya kazi maeneo ya Ngula, mkoani Geita, tukafika kijiji fulani, na vijana walikuwa na mizigo iliyowaelemea, nikawaambia tuombe tuhifadhi kwenye nyumba iliyokuwa ikionekana maeneo ya karibu. Wale wafanyakazi waligoma kabisa wakisema kuwa hiyo nyumba ni kwa mganga wa kienyeji. Nikawaambia sisi tunaweka tu mizigo, uganga ni wa kwake. Wakanifuata kwa nyumva, kwa woga. Ilikuwa majira ya saa 4 asubuhi. Kufika pale nikawakuta watu wengi wametengeneza duara kama la nusu kipenyo cha meta 10. Mipaka ya lile duara ni unga/majivu. Na hakuna aliyeugusa ule unga/majivu. Watu wote waliolizunguka duara wameshika mioto inawaka. Katikati ya duara alikuwa huyo mganga, amevaa mashang na nguo nyeusi ya kujifunga. Mbele yake kulikuwa na mkuki ambao nchi yake ipo juu, na mpini haujashindiliwa kwenye ardhi, na juu ya ncha ya mkuki kulikuwa na chungu kikubwa, lakini hakianguki.

Mimi nilikatiza lile duara, nikaenda nikamsalimia kwa kisukuma yule mganga mkononi, na kumtania kuwa bamwona yupo kwenye maabara yake, akacheka sana. Nikamwomva kuweka mizigo yetu, akaturuhusu. Baada ya pale habari zikaenea hapo kijijini kuwa eti sisi ni wachawi kumzidi hata huyo mganga. Na sababu ya kusema hivyo, eti ule unga wa kutengeneza duara hakuna mtu anaruhusiwa kuuruka isipokuwa mganga pekee yake. Ukiuruka tu, unaanguka na kufa pale pale. Na kwa vile mimi niliuvuka bila ya kuanguka, basi mimi namzidi hata yule mganga. Lakini hilo mimi naamini huenda ni vitisho tu vya hao waganga il wawadanganye vizuri. Ila kile kitendo cha mtungi mkubwa kukaa juu ya ncha ya mkuki, ni ngumu kuielezea.

Lakini kwangu mimi mpaka leo, sijawahi kuuogopa ushirikina hata kwa kiasi kidogo kabisa. Na ninaamini ushirikina hauwezi kuishinda nguvu ya Mungu.

Tusiamini mtu ambaye hawezi kudhulumiwa, basi ana nguvu za giza. Mtegemee Mungu katika utatu wake mtakatifu, kamwe nguvu za giza hazitakukushinda.
 
Nyie ndio mliozaliwa mmetanguliza miguu, mnakuwaga na nguvu ya asili.
Mimi ukinitendea mabaya yale ya kuuma, nikalia aisee kufa hufi ila cha moto utakiona. Sikuwa najua ila wenyewe wamekuwa wanarudi kuomba msamaha, kama kuna sehemu walinikosea!!!

Nina mengi ya kueleza ila watu yanawapata hivi, na ukiuliza mbona unataka nikusamehe kuna nini? Kuna wanaoelezea yaliyowakuta baada ya kunifanyia hayo mabaya. Na kuna wanaosema tu, nimejisikia kuomba msamaha ama kuona kama kuna kitu nilikukosea!!! Kwahiyo huwa natulia tu, nikiona mtu ananichokonoa namuangalia najua kitamlamba muda si mrefu.
 
Mimi ninayo hii nguvu sijui ilitoka wapi ila ni ya asili. Ukinifanyia ubaya basi ubwela unakufuata. Ila siipendi hii nguvu, sipendi kuona watu wakidhurika kwa ubaya mdogo mdogo tu wanaonifanyia.
 
Hakuna mkamilifu, nakosea na huwa naomba samahani nikijua nimekosea mimi. Kuna mazuri na mabaya maishani. Ila huwa naogopa kumfanya mtu aumie sana na kulia. Sababu najua maumivu yake, mimi mtu nikimfanya ajisikie wa thamani, mwenye furaha ndiyo kitu napenda. Ila usivuke Red line.
Kumbe wema wapo, ubarikiwe
 
Hivyo eeh!!! Huenda kweli maana kuna mazuri pia huyapata mtu anayekaa namimi karibu na tukatendeana mema. Kuna vitu sema sitaki tu kuanika hapa, ahsante Dexta
Nilishawahi kuwa kwenye uhusiano na mwanamke wa aina yako, kiufupi hata mkiwa mmelala hiyo nguvu yako inamlinda na mpenzi/mumeo pia..

Mnamambo mengi sana mazuri.
 
Nilichojifunza sio kila mtu anagusika .

Kuna jirani yetu ukimjaribu basi lazima mpoteane .

Nilimfata na kumuuliza inakuaje kila anayetaka kukufanyia ubaya au anayekufanyia anapoteana

Alinijibu kuwa hiyo hata yeye hajui na wamezikwa watu wengi na kupoteana tangia zamani.

Mimi mwenyewe najiuliza hii ni nguvu ya aina gani? Kila anayekujaribu anapoteana?.
Ulijifunza kwa njia ngumu!! Kwahiyo na wewe ilikua bado kidogo uende na maji?
 
Back
Top Bottom