Kwenye hili John Heche na Tundu Lissu wamuunge mkono Wasira

lord atkin

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
257
Reaction score
922
Hoja ya Steven Wasira kuwa kesi za jinai hazipaswi kuisha kwa busara na maridhiano ni ya kuungwa mkono na kila anayeamini katika utawala wa sheria. Kama DPP amefungua kesi kwa maslahi ya umma ili kupambana uhalifu kwanini kesi hiyo iishe kwa maridhiano kati wa mtuhumiwa na serikali?.

Hakuna kifungu chochote kwenye katiba au sheria kinachoruhusu hilo. Na kwa kuwa John Heche na Tundu Lissu ni waumini wa utawala wa sheria naamini wanafahamu hili. Kama tutaruhusu utaratibu wa kutumia maridhiano kumaliza kesi huko mbele watakuja viongozi wasiopenda haki watawapa watu kesi ili kuwalazimisha kuingia kwenye maridhiano. Pia wanaweza wakatokea wahalifu ambao watafanya makosa wakitarajia maridhiano yatawatoa.

Ninampongeza sana Mhe Wasira kwa kuliona hili na kushauri. Ninaimani Lissu na Heche wataunga mkono kauli hii. Nitashangaa sana nikisikia eti Heche na Lissu wameingia kwenye maridhiano ili kumaliza kesi. Watakuwa wamehalalisha uvunjaji wa katiba na sheria.

MWISHO: Maridhiano yanapaswa kuwa kwa ajili ya wananchi wote siyo kwa ajili ya kumaliza kesi ya mwanasiasa fulani.
 
sahihi 🤝
 
Back
Top Bottom