Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Nimekumbuka hadithi ya zamani ambapo waliamua kuwaua wazee wote; lakini sungura kwa ujanja wake alimficha baba yake. Baada ya muda mfalme akapata shida , akiwa amelala ameacha mdomo wazi, nyoka akaingia moja kwa moja hadi tumboni.
Ikawa nyoka atoleweje kwenye tumbo la mfalme! Mfalme akaahidi kuwa atakayeweza atamkabidhi ufalme wa nchi ile,,,,,,
 
Vipi kwenye hayo makundi Na asilimia zake wenye magonjwa hatarishi kama kisukar, UKIMWI, High na Lowa Blood pressure, Pumu n.k ni wangapi? Mana tumeambiwa corona si tishio sana Bali inapokutana na watu wenye matatizo ya namna hiyo pamoja na kinga ndogo ya mwili kupona inakuwa ni bahati na ndio ukweli pia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hapo kwenye HIV, ni kundi lipi limeathiriwa nayo
 
Wataalam wanasema njia kuu ya kuongeza immunity ni "stay active"...lakini vilevile wanasema sababu kuu inayopunguza immunity ni "hofu"...Viva JPM
Unaongelea "virus" ambae ni "DNA" corona ni "RNA" immunity yake huwezi ipata kwa "vaccines" kama vile ambavyo HIV hana "vaccines" mpaka sasa, zimeshindikana kwa kuwa nae pia ni RNA.

RNA ni "mutant" (anajibadili badili), ukitaka usitake ni lazima ujenge kinga ya mwili wako inayojitengeneza "naturally" na inayopatikana "naturally" kwa kui "boost natural immune system" kupitia kujipatia "natural boosters" za "vitamins" kwa wingi kwa kujipatia matunda na mboga mboga vile vile kuota jua la asubuhi na kufanya mazoezi kwa wingi na kuingiliana na kukutana na watu aina nyingi, kama tunavyoishi kikawaida nje ya "lockdowns".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi, nimeona nianze kwanza na hako kakipande hapo juu ili niweze kwenda kwenye hoja yangu moja kwa moja!

Kwanza niseme nimekuwa nikisumbuka sana na hali inavyoendele nchini, kana kwamba kiongozi mkuu na wasaidizi wake kuna jambo wao wanalifahamu lakini sisi hatulifahamu!

Hata hivyo, juhudi zote za kujiuliza na kijifikirisha, zimepelekea mimi kuja na wazo hili. Kwasababu ni wazi tumetofautiana wengi wetu na kama Taifa kuhusiana na namna serikali yetu inadeal na hii world pandemic!

Scenario ninayodhani inachukuliwa Tanzania.

Kama data zinavyoonyesha, ni kwamba Tanzania ina idadi ya vijana ambao ni asilimia 90 ya Watanzania wote. Wazee wenye miaka 64 na kuendelea, ni asilimia 3.1 tu ya wananchi wa Tanzania. Ina maana tuna risk ndogo sana inapokuja kwenye corona. Na wengi wenye magonjwa sugu wanaangukia kwenye group la wazee.

Sasa kuna aina mbili za immune ambazo zinafahamika na kukubalika duniani kote, nazo ni...

I)kupitia chanjo(vaccine)

II)Kupitia “herd immunity” ama kinga inayopatikana baada ya kupona gonjwa hilo.

Kila gonjwa, huwa linapewa asilimia zake za kufikia kutokana na jinsi ambavyo lina kasi katika maambukizi, mfano ugonjwa huu wa covid-19, wataalam wanasema kutokana na kasi yake ya maambukizi, basi ni lazima asilimia 70 ya wananchi wote wapate corona ndipo tunaweza kusema Tanzania tuna kinga kupitia “herd immunity”. Hapo ikiwa ina maana asilimia 30 iliyobakia inaweza kulindwa mfano wazee, wenye magonjwa sugu nk. Lakini kwasababu tuna vijana asilimia 90, basi ina maana hatutapata shida hata kidogo kuzipata hizo asilimia 70 zinazohitajika na WHO.

Kwasababu vijana hawaathiriwi sana na corona, ina maana tuna faida inapokuja kwenye “herd immunity”, ama huu mfumo unaotumika sasa nchini kwasababu kama tuna vijana asilimia 90, hatuwezi kukosa asilimia 70 za kutuwezesha kupata herd immunity na kuishinda corona.

Lakini hata hivyo data ni muhimu kufahamu tulipofikia. Pengine viongozi wameliona hilo kwasababu wao ndo wenye kuziona data, na ndiyo maana wanakuwa optimistic na kutangaza kuwa tumeishinda corona.

hata hivyo, pia ukifuatilia kauli zao na matendo, ni kama vile wanataka wananchi wengi kadri iwezekanvyo, waupate ili tufikie ile asilimia 70 inayotakiwa.

To be continued...

Tanzania Population 2020 (Demographics, Maps, Graphs)

Nguruvi3 Kalamu1 JokaKuu imhotep
BAK
Sky Eclat denooJ Pythagoras The Boss Lucas Mobutu
Pascal Mayalla
Erythrocyte Salary Slip Magonjwa Mtambuka Bia yetu kipara kipya johnthebaptist
Chakaza G Sam Influenza
YEHODAYA Tabutupu Daudi Mchambuzi Victoire FaizaFoxy
 
Mkuu Kama taifa ni kweli tuna idadi kubwa ya vijana? But do we know their health status kiasi Cha kujiamini kwamba watakuwa safe_ Jana tumezika rafiki yangu pale dodoma,he was under 40.second.Hao vijana ni productive kwa kiasi gani? Uchumi wa nchi hii umeshikiliwa na watu wachache mostlu who are above 40.Tatu hao vijana wako trained kwa kiasi gani na wanauzoefu wa kiasi gani kushika majukumu ya kina Ndugai na wengine baada ya hao over 40s kufyekelewa mbali na corona
 
Unaongelea "virus" ambae ni "DNA" corona ni "RNA" immunity yake huwezi ipata kwa "vaccines" kama vile ambavyo HIV hana "vaccines" mpaka sasa, zimeshindikana kwa kuwa nae pia ni RNA.

RNA ni "mutant" (anajibadili badili), ukitaka usitake ni lazima ujenge kinga ya mwili wako inayojitengeneza "naturally" na inayopatikana "naturally" kwa kui "boost natural immune system" kupitia kujipatia "natural boosters" za "vitamins" kwa wingi kwa kujipatia matunda na mboga mboga vile vile kuota jua la asubuhi na kufanya mazoezi kwa wingi na kuingiliana na kukutana na watu aina nyingi, kama tunavyoishi kikawaida nje ya "lockdowns".

Somo kubwa hili
 
Mkuu Kama taifa ni kweli tuna idadi kubwa ya vijana? But do we know their health status kiasi Cha kujiamini kwamba watakuwa safe_ Jana tumezika rafiki yangu pale dodoma,he was under 40.second.Hao vijana ni productive kwa kiasi gani? Uchumi wa nchi hii umeshikiliwa na watu wachache mostlu who are above 40.Tatu hao vijana wako trained kwa kiasi gani na wanauzoefu wa kiasi gani kushika majukumu ya kina Ndugai na wengine baada ya hao over 40s kufyekelewa mbali na corona
Maswali mazuri sana.

Nazungumzia wale wanaosemekana hawawezi kuishi bila kutoka, hapo ina maana ni vibarua. Sasa kama ni hao, wengi wao ni vijana wadogo kabisa. Fanya kautafiti kadogo utagundua. Hata hao madereva wanaozuiliwa huko mipakani ni watoto ama vijana wadogo kabisa. Nazungumzia through experience.

Hao kina Ndugai sasa wako kwenye asilimia kama 10 au chini ya hapo. Hapa pia nazingatia median age yetu watanzania.
 
Somo kubwa hili
Acha uongo. Eti somo kubwa. Ameweka reference? Si tuna macho ya kusoma na uwezo wa kuelewa? Maana ya JF kama una uelewa wa kutosha utafahamu nini cha kufanya.
 
Kinachotuangusha watanzania wengi kwenye kwenye hili suala la corona virus ni lack of scientific information about the whole thing. Naomba sana kabla sijatoa mchango wangu unipe maoni yako kuhusu hili suala: Wewe unafikiri ni kwa nini nchi nyingi zimechukuwa hatua ya lockdown*? (lockdown*: sipendi sana kulitumia hili neno kwani watanzania wengi wakiongozwa na rais either wanapotosha maana yake makusudi au hawaelewi maana yake kabisa)
Karibu sana kiongozi, wewe pia ni mmojawapo nilisahau kuwatag.

Lack of scientific information is is a huge disadvantage to us. Na hilo lemesababisha uwepo wa “lack of knowledge” when it comes to the viruses.

Ni kweli kabisa kuwa rais na watanzania, wamekuwa wakiongea kwa kurudia rudia mambo ambayo ni disinformation. Kwasababu nimeliona hata kwa Trump, ikanifanya niamini kwamba kuna jambo nyuma yake, na jambo hilo ni uchaguzi mkuu unaokuja mwishoni mwa mwaka huu.

Kuna taarifa ambayo nimeiweka humu, ambapo wanasema kuwa kama Trump angechukuwa hatua mapema badala ya kusubiri hadi March, wamarekani 36,000 wasingepoteza maisha yao.
Lockdown mainly ni kulinda maisha ya wananchi wako. Ndo maana mimi nilishangaa nakujiuliza inakuwaje? Mbona kama vile hawajali maisha yetu?
 
Ukitaka herd immunity lazima ukubali kutoa kafara wananchi wako.

Ni kweli lazima watu 70% lazima wapate maambukizi ndio mpate herd immunity.Lakini kumbuka 1% ya hao 70% lazima watakufa.Iwapo tupo watu milioni 55 je watafariki wangapi kabla hatujapata heed immunity?
Ni kweli kabisa mkuu. Herd immunity pia yenyewe haiendi tu bila tahadhari! Ina maana kwamba hata kama ni herd immunity, haina maana kwamba ndo fungulia mbwa yani maisha kama kawaida! Nooo!
 
Mahesabu ni haya;-
Hakuna fedha za kuhudumia wanannchi dhidi ya huu ugonjwa.
Amri iliyopo ni " songa mbele" atakae dondoka rip , mzima endelea kusonga mbele.. hatuwezi kufa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha! Mfano nchi ingekuwa na wazee wengi kama USA na Italy ndo ungesema haya!

Population yetu ingekuwa na wazee wengi kama hao wenzetu, halafu utaratibu ndo ukawa kama unavyosema, tungekuwa tunatafutana.
 
Yaani serikali inataka wengi waupate ugonjwa wa corona??? Uko serious?
Ukiwaambia watu wakusanyike kwenda kuomba dhidi ya gonjwa linalosambaa kutokana na mikusanyiko ndo utakuwa serious?
 
Mimi nafikiri hakuna hesabu iliyofanyika, ni uwezo mdogo wa kushughulikia majanga, kiongozi wetu hajawahi kuwa mstari wa mbele kwenye maswala haya, ni kama ana alergy, na mifano ni mingi.

Maswala ya majanga yanahitaji strategies, logistics, planning, budgeting na fikra za haraka. Pia mikutano ya mara kwa mara ambapo soft skills zinahitajika sana.

Bahati mbaya hatuna viongozi wenye hizo soft skills, ndio maana inabidi uyaache mambo yajiendee atakayepona apone atakaeondoka aondoke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa, hata mimi sikuona strategy yoyote na ni kweli kuwa serikali hii ya sasa haijisumbui na majanga! Hilo ni la ukweli kabisa. Hata kule Bukoba yaliwapata kule mto ngono na sokoni katerero!
 
FaizaFoxy yuko sahihi.

Mtoto anapozaliwa huwa hana kinga ya mwili lakini anaijenga kwa kushika shika vitu vyenye pathogens na kuweka mdomoni, puani, machoni na kila sehemu ya mwili wake. Kadri umri wa mtoto unapoongezeka na akili kukua ndivyo kinga inavyoongezeaka na hapo mtoto hupunguza kuweka vitu mdomoni.

Ni intelligence ya Mola wetu au kwa wale "vichaa" watasema ni evolutionary, kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Yaani, mtoto kujifunza kwa kudadisi na kushika shika vitu, wakati huo huo akijenga kinga ya mwili.

Pia ni kweli kuwa mutation ya RNA ni zaidi ya mara milioni ya ile ya DNA. Mama Faiza (naelewa kuna wakati anazingua) yuko sawa kabisa kusema njia pekee ya kujikinga ni kuuwezesha mwili wenyewe kujikinga.

Mwili wa binadamu unauwezo wa kujifunza jinsi ya kupambana na kirusi kilicho mutate, dawa za maabara haziwezi. Hii ndiyo sababu nchi zenye baridi, kila mwaka huwa kunakuwa na flu shot mpya, kwasababu ya RNA mutation.
Sasa maana ya herd immunity ni nini? Au lazima aseme FaizaFoxy ndo uelewe?

Pia hapa tunaenda na sources kama watu walioenda shule wakaelimika. Siyo blah blah!

Hata kama wewe ni professor, lazima uje na credible source of information. No abstract!
 
Mkuu kwanza tuweke baadhi ya mambo sawa

Herd immunity inapatikana pale population kwa kiwango fulani inapojenga immunity
1. Kupitia vaccination, kwamba, 80% kama sikosei ikiwa na immunity, 20% inalindwa
2. Pale ugonjwa unapokuwa na tabia ya kutengeneza ''immunity'' na hasa viral infections

Hakuna vaccination ya ugonjwa COVID-19
Hakuna ushahidi kwamba COVID-19 mtu akipata hatapata tena, ironically, kuna matukio ya kujirudia

Hapa inatueleza mambo kadhaa kuhusu viongozi. Kwamba, wanataka watu washangilie bila hoja ya kisayansi.

Kushangilia ni katika kufunika kile kinachoendelea na kuaminisha umma na dunia hakuna Corona Tz

Hilo linafanyika sambamba na kutotoa takwimu ili kujenga mazingira siku ikifika kwamba tumeshinda.

Mathalani, utasema vipi tuna korona ikiwa huna takwimu? na utasema vipi haipo ukiwa huna takwimu?

Jibu lolote lile ni sahihi kwasababu hakuna msingi wa kupinga au kukubali kwa maana ya takwimu.

suala la umri, hali ya hewa ya joto n.k. ni vitu tusivyoweza kufanyia tathmini kwasababu havisimami vyenyewe bila kuwa na nguzo nyingine.

Katika mambo yanayonishangaza ni pamoja na kuingiza masuala ya dini katika shughuli za serikali.
Kwamba watu wanataka imani zao ziwe imani za Taifa, nadhani hatutendi haki kwa wengine na wasioamini

Serikali haina dini, kazi hiyo iachwe kwa watu binafsi.
Mambo ya maombi si ya kitaifa, Tanzania ina watu wa imani tofauti na wasioamini .

JokaKuu Pascal Mayalla
Kama kawaida yako! Nashukuru sana kwa mchango muruwa kabisa!
 
I am more than your so called "credible sources". You either take it and regard me as the "source" of what I wrote or you don't. Your "credible sources" is none of my business, it's your problem.
GTFOH
 
Karibu sana kiongozi, wewe pia ni mmojawapo nilisahau kuwatag.

Lack of scientific information is is a huge disadvantage to us. Na hilo lemesababisha uwepo wa “lack of knowledge” when it comes to the viruses.

Ni kweli kabisa kuwa rais na watanzania, wamekuwa wakiongea kwa kurudia rudia mambo ambayo ni disinformation. Kwasababu nimeliona hata kwa Trump, ikanifanya niamini kwamba kuna jambo nyuma yake, na jambo hilo ni uchaguzi mkuu unaokuja mwishoni mwa mwaka huu.

Kuna taarifa ambayo nimeiweka humu, ambapo wanasema kuwa kama Trump angechukuwa hatua mapema badala ya kusubiri hadi March, wamarekani 36,000 wasingepoteza maisha yao.
Lockdown mainly ni kulinda maisha ya wananchi wako. Ndo maana mimi nilishangaa nakujiuliza inakuwaje? Mbona kama vile hawajali maisha yetu?
Asante sana mkuu. Hata mimi nakubali kabisa. Magufuli anachopania hapa ni uchaguzi tu. Anajua kabisa wananchi wengi wanaamini kuwa lockdown ni kuwanyima watu kutoka nje ya nyumba zao kabisa kwa muda fulani. Amechukuwa hili neno ili kuwatisha watu huku akiwahakikishia kuwa yeye anawapenda na kuwajali sana ndiyo maana hataki lockdown. Ni mnafiki mkubwa. Mkuu mpaka sasa wamekufa watu wengi sana kwa corona ila idadi imefichwa. Maabara ya kupimia imeingiliwa na sababu za vifo vingi hazionyeshi tena kama watu wamefariki kwa corona hata kama ndiyo sababu ya kifo. Hii yote ni kuwa anajaribu kukwepa ushahidi siku zijazo kwa sababu kama watakuja kufuatilia kuna uwezekano mkubwa wa kujua idadi kamili. This guy is just a killer by nature na hataki ushauri wowote tofauti na anavyotaka yeye. Hata wizara ya afya ameondoa wale wote waliokuwa angalau wanaonyesha utaalam na kubakisha wale manyumbu. In fact nchi nyingi sana zimekiri kuwa lengo la lockdown siyo kumaliza tatizo bali ni kuokoa maisha ya wananchi kwa kufanya watu wengi wasiugue kwa wakati mmoja na hospital zikaelemewa. Hata kwa wale wanaotaka ''herd immunity'' ni kuwa wanasema ni lazima kuwa na namna ya ku-control wingi wa watu wanaougua kwa wakati mmoja ili hospital ziweze kuhudumia wale ambao watazidiwa. Kinachonishangaza ni kuwa Magufuli anakasirika na kubeza anapoona watu wamevaa maski au wanachukuwa tahadhari nyingine za kibinafsi ambazo haziingiliani na ujenzi wa Taifa hata kidogo. Narudia tena mpaka sasa ni watanzania wengi wameshafariki kwa korona, na hivi vifo vingeweza kuzuilika kabisa. Iko siko mambo yatajulikana tu kwani sasa hivi namna madaraka yamelevya watu mpaka kujiona watadumu hapo walipo milele.
 
Back
Top Bottom