Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Somo kubwa hili
Umejifunza nini hapo? Yani solution ni kula matunda na kuzurura? Wtf is wrong with you people? Mkisikia mnachokipenda kusikia masikioni mwenu, basi mnarukia na kumfurahia mtu bila ya kushughulisha ubongo wako kuhusiana na alichokiandika!

Hii siyo caliber ya kula matango pori. Huna source ya unachozungumiza na wakati ni scientific? Mambo hayaendi hivyo! Ndo maana mnaulizwa hizo phd mlivyozipata!
 
Mkuu kwanza tuweke baadhi ya mambo sawa

Herd immunity inapatikana pale population kwa kiwango fulani inapojenga immunity
1. Kupitia vaccination, kwamba, 80% kama sikosei ikiwa na immunity, 20% inalindwa
2. Pale ugonjwa unapokuwa na tabia ya kutengeneza ''immunity'' na hasa viral infections

Hakuna vaccination ya ugonjwa COVID-19
Hakuna ushahidi kwamba COVID-19 mtu akipata hatapata tena, ironically, kuna matukio ya kujirudia

Hapa inatueleza mambo kadhaa kuhusu viongozi. Kwamba, wanataka watu washangilie bila hoja ya kisayansi.

Kushangilia ni katika kufunika kile kinachoendelea na kuaminisha umma na dunia hakuna Corona Tz

Hilo linafanyika sambamba na kutotoa takwimu ili kujenga mazingira siku ikifika kwamba tumeshinda.

Mathalani, utasema vipi tuna korona ikiwa huna takwimu? na utasema vipi haipo ukiwa huna takwimu?

Jibu lolote lile ni sahihi kwasababu hakuna msingi wa kupinga au kukubali kwa maana ya takwimu.

suala la umri, hali ya hewa ya joto n.k. ni vitu tusivyoweza kufanyia tathmini kwasababu havisimami vyenyewe bila kuwa na nguzo nyingine.

Katika mambo yanayonishangaza ni pamoja na kuingiza masuala ya dini katika shughuli za serikali.
Kwamba watu wanataka imani zao ziwe imani za Taifa, nadhani hatutendi haki kwa wengine na wasioamini

Serikali haina dini, kazi hiyo iachwe kwa watu binafsi.
Mambo ya maombi si ya kitaifa, Tanzania ina watu wa imani tofauti na wasioamini .

JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu hapo kwenye percentage kwenye covid-19 ili kuweza ku achieve immunity through herd immunity ni asilimia 70.
 
Ndio raha ya kuwa na rais msomi wa daraja la juu mwenye utaalamu wa kemia

Corona haitaamini kama imedhibitiwa na Bingwa wa Kemia.

Kipindi serikali inapanga kuwapa msaada watu wa Jamhuri ya China katika mapambano dhidi ya Corona kuna wanaccm walimbeza Magufuli
Duuuuh,[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kwenye hayo makundi Na asilimia zake wenye magonjwa hatarishi kama kisukar, UKIMWI, High na Lowa Blood pressure, Pumu n.k ni wangapi? Mana tumeambiwa corona si tishio sana Bali inapokutana na watu wenye matatizo ya namna hiyo pamoja na kinga ndogo ya mwili kupona inakuwa ni bahati na ndio ukweli pia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ukweli kabisa kuwa walioko kwenye makundi hayo, ndo wale tunaotakiwa kuwalinda il wasipatwe na gonjwa hili. Wakiwa wachache inakuwa ni rahisi zaidi, lakini hadi usawa huu bado sijaona jitihada za msingi kwenye hilo.
 
Kalamu

JPM hakuweka rehani, aliamua

1.corona haiishi leo hata kesho
2.corona can be controlled na wahusika wa eneo husika kwa njia zao

3.kesho kikitokea kirusi kingine utakimbilia ndani?

4.maisha ya watu na kula yao inategemea kazi ya siku wangeishije? Na jibu utakalotoa mpaka lini?

5.mbona lockdown dunia nzima imeshindwa watu wanarudi mtaani na watapata tena na tena

6.Nani alikuwa na solution sahihi??

Hakuna chochote ambacho rais angeamua bila kupata upinzani wa aidha nyie mnaojifanya wasomi au wananchi kupinga

Lockdown hata JPM angeamua, wananchi wangeingia mitaani

Nyie mnaishi mikocheni nyumba za kurithi na kupokea kodi kila mwezi, mimi natoka home asbh sijui familia yangu itakula nini...you cant lock me down, never

Acheni upuuzi wa kujiona mna akili na soon mtaaibika

Mpaka leo hauoni trend ya dunia inarudi kwenye solution za sweden na Tanzania?

Viongozi wa sweden unawaitaje???
Na wewe ni moja ya wale makasuku ambao hawalewi kabisa lengo la lockdown. Mazee soma angalau historia ya virus wanaosambaa kwa njia ya hewa kama ile Spanish Flu ili ujiongezee maarifa. Nchi zote zilizoweka lockdown lengo halikuwa ni kumaliza virus au watu wakae nadani mpaka itakapotangazwa kuwa virus wameisha, la hasha. Lockdown zinawekwa ili kufanya watu wengi wasiugue kwa wakati mmoja na hospital zikaelemewa. Na nina uhakika unajua kuwa kama siyo hizo hatua za lockdown walizochokuwa mambo yalikuwa yawe mabaya sana. Na pia unajua kuwa sasa hivi wanaondoa lock down baada ya maambukizi kupungua na hawatasita kurudisha tena lockdown kama yataongezeka tena. Na pia nikujulishe kama hujui, kuwa lengo jingine la lockdown ni kuvuta muda ili tuwajue kwa undani hawa virus na ikiwezekana tujue dawa zinazoweza kupunguza makali yake au tupate sindano za kinga. Tanzania tumepoteza watu wengi sana ambao kama tungechukuwa hatua sahihi (siyo total lockdown) wangekuwa hai mpaka sasa. Vifo vimetokea mpaka rais akaamua kuingilia upimaji na utoaji wa takwimu ili kuficha uzembe wake. Atawadanganya watu wengi lakini hawezi kuwadanganya watu wote na kwa muda wote.
 
Nimeipenda hii
You can fool some people sometimes but you cant fool all people all the time
Bob Marley wise words in the song War
 
Na wewe ni moja ya wale makasuku ambao hawalewi kabisa lengo la lockdown. Mazee soma angalau historia ya virus wanaosambaa kwa njia ya hewa kama ile Spanish Flu ili ujiongezee maarifa. Nchi zote zilizoweka lockdown lengo halikuwa ni kumaliza virus au watu wakae nadani mpaka itakapotangazwa kuwa virus wameisha, la hasha. Lockdown zinawekwa ili kufanya watu wengi wasiugue kwa wakati mmoja na hospital zikaelemewa. Na nina uhakika unajua kuwa kama siyo hizo hatua za lockdown walizochokuwa mambo yalikuwa yawe mabaya sana. Na pia unajua kuwa sasa hivi wanaondoa lock down baada ya maambukizi kupungua na hawatasita kurudisha tena lockdown kama yataongezeka tena. Na pia nikujulishe kama hujui, kuwa lengo jingine la lockdown ni kuvuta muda ili tuwajue kwa undani hawa virus na ikiwezekana tujue dawa zinazoweza kupunguza makali yake au tupate sindano za kinga. Tanzania tumepoteza watu wengi sana ambao kama tungechukuwa hatua sahihi (siyo total lockdown) wangekuwa hai mpaka sasa. Vifo vimetokea mpaka rais akaamua kuingilia upimaji na utoaji wa takwimu ili kuficha uzembe wake. Atawadanganya watu wengi lakini hawezi kuwadanganya watu wote na kwa muda wote.
Maneno mengi lakini ukweli utabaki pale pale. Hakuna binadamu anaeweza zuia kifo cha binadamu mwenzake kama muda umefika.

Lawama zako zote ni utapoteza nguvu zako bure. Ukitaka lawama zako ziwe na mashiko weka takwimu za vifo vya corona hapa Tanzania. Tofauti na hapo ni kelele tu kama zilivyo kelele nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba corona virus amejengwa na RNA na si DNA.

Kwamba RNA huwa na tabia ya kumutate

Kwamba hakuwezi patikana vaccine

Sent using Jamii Forums mobile app
Weka reference ya unachosema. Hata mimi ninayoyasema nilikuwa nayafahamu, lakini umeona nimeandika bila reference?

Kama ni scientific, yeye FaizaFoxy ndo amegunduwa hilo?

Umesoma mpaka la ngapi dada?
 
Sasa maana ya herd immunity ni nini? Au lazima aseme FaizaFoxy ndo uelewe?
Sasa herd immunity utaipataje kama watu watajificha?
Pia hapa tunaenda na sources kama watu walioenda shule wakaelimika. Siyo blah blah!

Hata kama wewe ni professor, lazima uje na credible source of information. No abstract!

Why are RNA virus mutation rates so damn high
The immunocalibration hypothesis
Discovery of immune cells able to defend against mutating viruses could transform vaccine development
Immunity and immunopathology to viruses:
 
Tatizo kuifikia hiyo 'herd immunity' kuna gharama kubwa sana ya kulipa ambayo ni usalama wa afya na uhai wa wananchi walio wengi maana sio wazee tu wenye Kinga hafifu hata hao vijana unaowalenga wapo ambao Kinga yao ya miili haitaweza kuhimili hivi virusi, hivyo hii njia bado ni hatari.
Takwimu zinaonyesha level ya maambukizi na kasi ya maambukizi ni ndogo sana kwa nchi za Afrika. Ukiangalia graph ya kiasi cha maambukizi yote Vs Muda, katika nchi zilizoathirika sana kama hispania na uingereza utaona kuwa miezi miwili ya kwanza ongezeko la maambukizi ni dogo sana. Lakini kuanzia mwezi wa tatu wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu maambukizi hupanda sana kiasi cha kutisha. Ndio maana kwa kutazamia trend hiyo, wazungu walitegemea kuanza kuona miili ya watu mitaani huku Afrika hususan Tanzania kuanzia tarehe 15/05/2020. Hilo halijatokea. Kumbuka ugonjwa uliingia Tanzania tarehe 15/03/2020. Hivyo tarehe 15/05/2020 ni miezi miwili kamili na baada ya hapo walitegemea maambukizi na vifo vipande sana. Mpaka sasa halijatokea.
Ina maana tukiingia mwezi wa sita bila mlipuko mkubwa huo ni uthibitisho kuwa trend ya ugonjwa kwetu haifuati trend kama ya ulaya. Ndiyo maana anga na vyuo vitafunguliwa wakati huo. Very scientific!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka reference ya unachosema. Hata mimi ninayoyasema nilikuwa nayafahamu, lakini umeona nimeandika bila reference?

Kama ni scientific, yeye FaizaFoxy ndo amegunduwa hilo?

Umesoma mpaka la ngapi dada?
Weeee nae

Nimeandika nimejifunza toka kwa Faizafoxy

Unasema niweke reference, unakeraa

Nimesoma mpaka la saba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafahamu chanjo inavyopatikana?

Kama hauna chanjo ndo uendelee kuzurura, na kula matunda ili kuudhibiti? Hivyo ndivyo unawatangazia wananchi?

Maelekezo ya wataalam wa wapi?

Generally inafahamika kwamba matunda yana vitamin c ambayo ni muhimu kwenye kujilinda na hayo magonjwa. Na mazoezi pia, lakini siyo kusema kwamba ndiyo njia muafaka ya kuudhibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi.

Labda kama hamjafahamu maudhui ya thread hii.

Hatahivyo kwenye herd immunity, ni sahihi kuhimiza tabia zinazoimarisha kinga za mwili huku hatua stahiki zikichukuliwa kupunguza maambukizi ya kasi.
 
Weeee nae

Nimeandika nimejifunza toka kwa Faizafoxy

Unasema niweke reference, unakeraa

Nimesoma mpaka la saba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa utajuaje kama umelishwa matango pori? Hata maprofesa wenyewe wanaulizwa reference.

Labda kanisani au miskitini ndo unaamini watu bila maswali.
 
Tatizo kuifikia hiyo 'herd immunity' kuna gharama kubwa sana ya kulipa ambayo ni usalama wa afya na uhai wa wananchi walio wengi maana sio wazee tu wenye Kinga hafifu hata hao vijana unaowalenga wapo ambao Kinga yao ya miili haitaweza kuhimili hivi virusi, hivyo hii njia bado ni hatari.
Magufuli ni changer kwenye kila eneo.

Hatimaye ametokomeza Corona Tanzania nzima

Watanzania tunamhitaji kwa miaka 50 ijayo

Wapinzani wote say yeeeeiiiiyeeeee
 
Huwezi kusema hivyo acha uongo. Umetumia vigezo gani kusema hivyo?
Kigezo ni jinsi watu wanavyoongea huku mitaani mpaka Kyle ambapo ilikuwa ni ngome ya chadema kama Arusha na Moshi. Jana alikuwa kwenye mkoa wa Lisu, mwenyewe uliona jinsi watu wanavyomkubali Magufuli. Hata Mbowe mwenyewe ataunga juhudi mapema tu, labda Tundu ndo anaweza kujivuta vuta kidogo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu kama Maghufuli alifikiria hivyo toka awali, sina uhakika, ndo maana nikasema nilijaribu sana kufikiria kwamba nia yake ni ipi?
Mbona hili kalielezea Jumapili iliyopita kanisani.

"Msukumo wa aliyoamua ulilenga kulinda uchumi"; pamoja na kwamba madhara ya ugonjwa huu mpya yalalikuwa hayajulikani kwa yeyote.

Anyways, kuna hiki kipengele kuhusu research iliyofanyika kule Wuhan China.
Hicho kipengele ulichochomeka hapo hakiwezi kuwa ndio iwe nguzo ya maamuzi mazito juu ya kukabiliana na ugonjwa ambao ni mpya.

Wachina kubwaga chini kila kitu na kusimamia kuzuia maenezi ya ugonjwa usiojulikana, wao hawakuwa wajinga.

Sisi tukabahatisha, na kwa bahati yetu nzuri, huenda tumesalimika, kama wanavyosalimika Burundi na kwingineko.

Kote huko tutasema viongozi hao walikuwa na maono juu ya hatma ya ugonjwa huu nchini mwao?
 
Unafahamu chanjo inavyopatikana?

Kama hauna chanjo ndo uendelee kuzurura, na kula matunda ili kuudhibiti? Hivyo ndivyo unawatangazia wananchi?

Maelekezo ya wataalam wa wapi?

Chanjo hakuna na itachukua muda mrefu kupatikana, kwa hiyo watu wajifungie tuu ndani, kisa chanjo?
Generally inafahamika kwamba matunda yana vitamin c ambayo ni muhimu kwenye kujilinda na hayo magonjwa. Na mazoezi pia, lakini siyo kusema kwamba ndiyo njia muafaka ya kuudhibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi.

Labda kama hamjafahamu maudhui ya thread hii.

Hatahivyo kwenye herd immunity, ni sahihi kuhimiza tabia zinazoimarisha kinga za mwili huku hatua stahiki zikichukuliwa kupunguza maambukizi ya kasi.
Hatua stahiki ni pamoja na watu kupata vitamin C, virutubisho muhimu vya mwili (organic), jua, kunawa/kutakasa mikono na kutumia barakoa. Vyote hivyo vimefanyika.

Ni ujinga kwa nchi za Afrika kutumia njia zile zile zilizotumika nchi za magharibi kwasababu wao wako kwenye latitudo tofauti na sisi. Jua wakati wa winter kwao lipo kwenye nyuzi 45 hivi, wakati sisi linacheza kwenye nyuzi 90 karibia mwaka mzima. Hivyo sisi tunapata UV kwa wingi sana na hivyo kusaidia kupunguza maambukizi ya covid-19 kuliko kaskazini.
 
Chanjo hakuna na itachukua muda mrefu kupatikana, kwa hiyo watu wajifungie tuu ndani, kisa chanjo?

Hatua stahiki ni pamoja na watu kupata vitamin C, virutubisho muhimu vya mwili (organic), jua, kunawa/kutakasa mikono na kutumia barakoa. Vyote hivyo vimefanyika.

Ni ujinga kwa nchi za Afrika kutumia njia zile zile zilizotumika nchi za magharibi kwasababu wao wako kwenye latitudo tofauti na sisi. Jua wakati wa winter kwao lipo kwenye nyuzi 45 hivi, wakati sisi linacheza kwenye nyuzi 90 karibia mwaka mzima. Hivyo sisi tunapata UV kwa wingi sana na hivyo kusaidia kupunguza maambukizi ya covid-19 kuliko kaskazini.
Chanjo inapatikana endapo kuna antibodies.
 
Back
Top Bottom