Kwenye kila Mimi ni kama huwa kuna Mimi nyingine nyuma ya hiyo Mimi, je Mimi ni nani?

Thecoder

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
2,620
Reaction score
6,780
Embu anza kuangalia kwenye namna unavyojimililisha vitu, utaona ni kama kuna Mimi ambayo iko nyuma ya Kila Mimi.

Ukiulizwa jina, utasema naitwa fulani, utasema mwili wangu, utasema mkono wangu, utasema moyo wangu na kadhalika.

Kwenye Kila umiliki hapo utaona ni kama imekaa hivi… mkono wangu mimi lakini sio Mimi, mwili wangu mimi lakini sio Mimi, ni moyo wangu mimi lakini sio mimi na ndio maana ukipata ajali na ukakatwa mguu utasema mguu wangu ulikatwa, au mkono wangu ulikatwa ila sio Mimi, au utaskia mwili wake umepalalaizi (ni mwili wake ila sio yeye).

Hata kwenye habari, utaskia alikutwa amefariki kando ya barabara na mwili wake (yeye ambayo ndio ile Mimi sasa) umehifadhiwa kwenye hospital fulani. Je, huyo yeye (ambae ndio Mimi) ni nani na yuko wapi wakati mwili wake upo monchwari?

Lakini hapo hapo ukirudi kwenye matendo mengi, utakuja kugundua hapo huwa Mimi anahusika moja kwa moja.

Kwamfano nani ambae amechora ubaoni, utaskia sio Mimi au ni Mimi, nani ambae amaua ni Mimi au sio Mimi, nani ambae ameiba ni Mimi au sio Mimi.

Kwahiyo kwenye hali ya umiliki, Mimi huwa hana chake ila kwenye matendo Mimi huwa ndio producer.

Sasa, ikiwa Mimi si mwili, si mkono, si moyo, si mawazo, si hisia, na si jina lakini ndiye anayejipa umiliki na ndiye tunayemhusisha na matendo, je, Mimi ni nini?
 
Fumbo hili la mimi ni kama kutafuta kitunguu. Unaona kitunguu kila ukitoa ganda la juu linakuja lingine na unaweza maliza kutoa maganda yote swali linabaki kitunguu kiko wapi.
The most profound question human beings to ask themselves is WHO AM I?
 
Inakua ni infinity loop... Na kwanini unahisi inakua hivi?
 
kwan haujui kama kuna mwili nafsi na roho,, mwili ni muunganiko wa viungo mfano mkono, kichwa, miguu nk, nafsi ndo huyo wew ambae ni mimi alf roho ndo iyo inayo ifashauriana na nafsi kuu-umiza mwili, kwa matendo ya kikuda

ndo maana utaskia, "nafsi au roho yangu imegoma kufanya jambo flani",, nafsi na roho vikikoma kufanya kazi, mwili unabaki bure kama pambo
 
Umesema kuna mwili, nafsi na roho pia ukasema roho yangu, mwili wangu, nafsi yangu. Kama ukijisikiliza vizuri kuna mmiliki wa vyote hivyo roho, mwili na nafsi. Swali mmiliki ni nani?
 
Huenda “Mimi” si kitu kilichopo nyuma ya kila kitu; huenda “Mimi” ni jina tunalolipa mfumo mzima unaopitia uzoefu, unaokumbuka, unaamua na kutenda.
 
Back
Top Bottom