Embu anza kuangalia kwenye namna unavyojimililisha vitu, utaona ni kama kuna Mimi ambayo iko nyuma ya Kila Mimi.
Ukiulizwa jina, utasema naitwa fulani, utasema mwili wangu, utasema mkono wangu, utasema moyo wangu na kadhalika.
Kwenye Kila umiliki hapo utaona ni kama imekaa hivi… mkono wangu mimi lakini sio Mimi, mwili wangu mimi lakini sio Mimi, ni moyo wangu mimi lakini sio mimi na ndio maana ukipata ajali na ukakatwa mguu utasema mguu wangu ulikatwa, au mkono wangu ulikatwa ila sio Mimi, au utaskia mwili wake umepalalaizi (ni mwili wake ila sio yeye).
Hata kwenye habari, utaskia alikutwa amefariki kando ya barabara na mwili wake (yeye ambayo ndio ile Mimi sasa) umehifadhiwa kwenye hospital fulani. Je, huyo yeye (ambae ndio Mimi) ni nani na yuko wapi wakati mwili wake upo monchwari?
Lakini hapo hapo ukirudi kwenye matendo mengi, utakuja kugundua hapo huwa Mimi anahusika moja kwa moja.
Kwamfano nani ambae amechora ubaoni, utaskia sio Mimi au ni Mimi, nani ambae amaua ni Mimi au sio Mimi, nani ambae ameiba ni Mimi au sio Mimi.
Kwahiyo kwenye hali ya umiliki, Mimi huwa hana chake ila kwenye matendo Mimi huwa ndio producer.
Sasa, ikiwa Mimi si mwili, si mkono, si moyo, si mawazo, si hisia, na si jina lakini ndiye anayejipa umiliki na ndiye tunayemhusisha na matendo, je, Mimi ni nini?