Sasa cha ajabu nini?? Ni wapi uliona mwanamke anamweka mume kama mrithi my friend. Mimi ni mtumishi sijawahi kuona.. Hata uwaaulize au kuwashauri huwezi kubadirisha hiyo mitazamo yao..
So why ukae uumize kichwa kwa vitu none sense. Unajua wazi kwa nini huwa wanafanya hivyo. Kwa hiyo usiumize kichwa. Au una uhakika atatangulia kufa yeye? If not why bother?
Wote ndio Hali hiyo hiyo na maisha ya naendelea tena kwa furaha na Amani.
Kwani akitangulia wewe utashindwa kutunza watoto mpaka uwe concern na nini aliandika?
Baada ya kifo wanaotesekaga ni wajane (Wanawake) na sio wagane.
Mwanamke anaamini yeye akifa utaoa mke mwingine ambaye ndiye atakayekuja kula vyote alivyochuma au mlivyochuma pamoja na atawanyanyasa watoto wake aliowaacha.... Na wanaona mifano hai kila siku na ni kweli.
Sasa utatumia mbinu ipi kumwaminisha kuwa kwako haitakuwa hivyo?
Kumbuka mwanaume ndio mwenye maamuzi ya kuoa au kuto oa.. Tofauti na mwanamke akifiwa kuolewa ni ngumu sana Maana Hana maamuzi juu ya mwanaume. Labda achukue viserengeti. Ingawa wapo wachache wanao olewa tena.
So relax chapa kazi, lea familia achana na hivyo vitu vidogo kama you're machured enough kwenye ndoa.
Jenga future bora ya familia yako hata usipo kuwepo una uhakika hakuna kikaragosi kutoka kwenye ndugu zako atakae ingilia future na rasilimali ulizoacha vinginevyo usipoteze muda na akili.
Wanaume ndio tunaopaswa kujenga Mifumo ya kuaminika na wenzi wetu vinginevyo mtaishia kuharibu ndoa.
Njia ya kwanza ni kudhihirisha kwa vitendo kuwa huna na huhitaji chochote chake(isipokuwa responsibilities za kawaida kwenye family, mahitaji, maendeleo, Ada etc.) lakini Mali no no.. Jinsi ambayo utakuwa huonyeshi interest kwenye maeneo hayo ndivyo atakavyo kuamini na kukabidhi mwenyewe Mali na mirathi.
Kadiri unavyoonesha interest kwenye vitu hivyo ikiwemo mirathi uliyo Sema ndivyo atazidi kuikimbiza mbali nawe Maana ni Ishara ya kutoaminika.
Be Gentle man my friend utaishi kwa raha, Amani na furaha na mkeo.