Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Wewe ushawahi uliwa na paka
 
Usithubutu
 
Hata paka inaweza mdhibiti black mamba.
Black mamba anadhibitiwa kwa namna nyingi. Ila sisi wabongo tunamtukuza na kuona kwamba ni nyoka asiedhibitika, wakati kiuhalisia kuna njia nyingi za kumdhibiti na kuuwawa kwake.
 
Nakuomba uingie google uandike "who is a king of snakes in the world" alafu uone utapata jibu gani.

Dunia nzima nyoka anaeuwa na kumeza nyoka wenzake ni mmoja tu ambae ni King Cobra. King Cobra ni nyoka anaeuwa na kumeza nyoka wa aina yoyote katika dunia hii. Kasoro Chatu tu tena awe mkubwa kuliko saizi ya King Cobra, ndo hawezi kumwezwa. Lakini wengine wote akiwemo huyo black mamba wako, ni chakula chake popote atapokutana nae na sumu yake haimfanyi lolote King Cobra.
 

Attachments

  • images (4).jpeg
    24.9 KB · Views: 6
  • images (5).jpeg
    30.9 KB · Views: 6
  • images (7).jpeg
    35.8 KB · Views: 6
Nakuomba uingie google uandike "who is a king of snakes in the world" alafu uone utapata jibu gani.

Dunia nzima nyoka anaeuwa na kumeza nyoka wenzake ni mmoja tu ambae ni King Cobra. King Cobra ni nyoka anaeuwa na kumeza nyoka wa aina yoyote katika dunia hii. Kasoro Chatu tu tena ndo hawezi kumwezwa. Lakini wengine wote akiwemo huyo black mamba wako, ni chakula chake popote atapokutana nae na sumu yake haimfanyi lolote King Cobra.
 
lengo langu nataka kuanzia mradi wa ufugaji nyuki mkuu na kama ujuavyo lazima uende kuangalia kila mara
Hakuna shida mkuu, nyoka kwake ni porini na huko ndo maskani yake na ukitaka kum-disturb ndo utaangamia. Yaani mpaka umefika hapo kwenye msitu wako umewapita nyoka kibao sema Kwa kuwa hujawashitukia unaamini huko kwenye mashamba mengine hakuna nyoka.

Nyoka Kwa binadamu ni mwoga na akimwona binadamu huwa akiwa kwenye position nzuri huwa anatoka nduki hasa akiwa chini kwenye nyasi ila akiwa juu ya mti huwa hana option ya kufanya na mara nyingi huwa anapiga kimya (unamuona katulia tu na ulimi wake) na huwa ana assume hujamuona. Na hapo sasa bahati mbaya za kugongwa na nyoka hutokea ukipita karibu yake ana assume kama unamfuata lakini napo hakugongi tu mpaka uwe karibu sana kiasi kwamba anahisi una jambo unataka kujifanya

Wewe endelea na shughuli zako yaani hapo akiona Kila siku mpo hapo atatafuta sehemu nyingine ya kujistiri
 
Mkuu kwa paka sina uhakika, fuatilia kile kipindi cha snake city.
Mara nyingi sana paka anakuwa target kwa hayo madude. Black mamba ni mkubwa na ana kasi kwa paka ni ngoma nzito.

Nipe ushahidi kulingana na experience yako niendelee kujifunza mkuu.
Katika kila jambo exceptional zipo, unaeza kuta paka amelala akagongwa, fuatilia google is free, paka ana kasi mara 2 ya black mamba, usimchukulie poa kabisa.
Wanasema paka anaua king cobra hadi black mamba.
 
Kuna miti Fulani huwa mvua ikinyesha hutoa harufu Fulani inayofukuza nyoka... jila LA hiyo miti nimesahau.

Ila ukienda kwa wataalam watakupa maelekezo, hiyo miti ni uzio mzuri wa nyoka.
Dah! Hebu kumbuka aisee umsaaidie mdau. Ingekuwa ni wale nyoka wanaoingia ndani angelitumia mti wa mwitanjoka (Mkunde pori) (Kwa kuuchoma ndani ya nyumba) au kuchoma asali ya nyuki.
Mti unaotoa harufu mvua ikinyesha labda ni mvunja genge?
 
Dah! Hebu kumbuka aisee umsaaidie mdau. Ingekuwa ni wale nyoka wanaoingia ndani angelitumia mti wa mwitanjoka (Mkunde pori) (Kwa kuuchoma ndani ya nyumba) au kuchoma asali ya nyuki.
Mti unaotoa harufu mvua ikinyesha labda ni mvunja genge?
Nitatafuta nipost humu, nimewahi kuishi porini katikati ya mlima sikuwahi kuona nyoka sehemu ya makazi ya Watu, Lakini kwenye mlima kila siku Tulikuwa tunapishana nao.

Hadi wenyeji waliponiambia Siri ya miti iliyopandwa kuzunguka Eneo letu la kuishi
 
Huyu kiumbe ni hatari sana hasa anapokuwa na hasira ana mbio na uwezo wa kuruka , japo huwa sio mkubwa kivile wengine humpamba kwa uhatari wake.

Kwanini usiwaruhusu wanakijiji wamuue au nao hawataki kusikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…