Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

Kwenye msitu wangu kuna black mamba/ koboko natafuta njia za kumwangamiza bila kuleta madhara kwenye jamii

We una uhakika gani wako wawili tu? Cha msingi temana nao nyoka hawana shida na mtu labda utake kuwadhuru
Nakutanaga nao sana huko simanjiro Kila mmoja anaenda na hamsini zake
Binafisi na amini wapo wengi lakini kwa mashuhuda wamewahi onekana wawili na huenda huwa huwa wanaona wengine wao wanajua ni haohao wawili. yahitaji moyo sana sema madogo mle mle ndo huenda chungia mbuzi
 
King Cobra chakula chake rasmi ni nyoka wenzake.
Na nyoka wote wenye sumu kali wanaliwa vizuri tu na Cobra.
Tatizo ni kwamba Koboko huwa wanarefuka sana kumzidi king Cobra.
Akiwa mrefu na mnene kuliko na Cobra kesi inakuwa ngumu kwake.
Hii sikuijua na kuna mdau mwingine nimembishia kwa sababu cobra wamo japo sio wengi
 
wewe utakua tabora vijijini uko igombe igombe flani back to the point fuga bundi koboko ndio chakula akipendacho
na ukifuga bundi jiandae kuchomwa moto na wanakijiji kwa tuhuma za uchawi
chagua kuuawa na koboko au wananzengo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ha
wewe utakua tabora vijijini uko igombe igombe flani back to the point fuga bundi koboko ndio chakula akipendacho
na ukifuga bundi jiandae kuchomwa moto na wanakijiji kwa tuhuma za uchawi
chagua kuuawa na koboko au wananzengo
Itabidi akae na wananzengo wajadili isiwe sio badae
 
Jf salaam🙏

Ni muda sasa tangu aanze kuonekana huyu nyoka hatari koboko na inasemekana wapo wawili.

Taarifa zilianza kunifikia kutoka Kwa wazee wangu maana huo msitu ukweli sio wangu ni wa mzee ila kaniruhusu kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.

Mara kadhaa amekuwa akionekana na muda wa usiku kupiga kelele flani Hivi.

Nakumbuka baada ya kupata mapumziko mafupi nilienda kijijni kwa wazee wetu. Nikafika na nikaenda mlimani(msituni) lengo nikufanya research kwa kina Ili niwekeze ufugaji wa nyuki (asali).

Nilimchukua dogo mmoja ambae Huwa anachunga mbuzi wangu tukaenda naye huku akinifotoa picha za kila aina na Kila Rangi.

Mwisho tukafika kwenye mti mzuri wenye kijani kibichi wenye matawi mazuri akanipigia picha za kutosha pale.

Baada ya hapo tukakaa chini ya mti huo kwenye jiwe huku nikipitia picha nilizopigwa na kufuta zile sikuzipenda

Tukiwa hapo tunapiga story ghafla tukasikia kelele za ndenge flani juu ya mti Mimi kelele zile nazijua huwa ni Alert ya hatari fulani wameiona wale ndege.

Kuinua macho juu sikuamini nilichokiona ni yeye koboko mtesa ametulia tulii Wala hatikisikii kama amekufa.

Dogo(muha) kumuona akapanic akaanza mbio nikamwambia simama hapohapo akasimama huku nami nikitoka eneo la tukio hadi kwa dogo.

Nyoka ni mkubwa na anaogopesha na kwa mazingira yale huwezi mshambulia kwa kutumia njia zetu hizi za asili(fimbo)

Maana ni mstuni vinginevyo anakuua ndani ya muda mfupi tu hakuna sehemu ya ku escape asikudhuru.

KUMBUKUMBU ZANGU

Miaka ya nyuma tukiwa wadogo nilishuhudia maiti za Watoto wenzetu watu na ng'ombe 7 zikiwa zimelala Chali (kufa).

Ni baada ya Hawa Watoto kuona huyo nyoka aina ya koboko na kumshambulia ndipo alipowageuka na kuwauma wote wawili na ng'ombe zao zote Saba na zilikufa hapohapo!

Nakumbuka kipindi hicho hicho nikiwa primary mtoto mwingine darasa letu Moja akiwa anaenda kuokota maembe kwenye mti wa mwembe akamuona koboko Kasimama wima naye pasina kujua alianza kumshambulia.

Hapo hapo alimgonga na kufa mama yake alisikia kelele za mwanae akilia Kwa uchungu Kwa sababu ilikuwa mbali na mwembe na mara zote walikuwa wanaenda Watoto kadhaa kuokota maembe pale. ile anatoka akamsaidie alimkuta tiyari kashafariki na nyoka amepanda juu ya mtu flani mfupi.

Ndipo alipo piga yowe kuomba msaada na walifanikiwa kumuua.

Inavyosemekana na Mimi naweza kuwa shahidi wa hili ni kwamba....

Nyoka aina ya black mamba ni wapole kupita kiasi pale anapokuwa katika Hali yake ya kawaida.

Pia anasikia kuliko kawaida anaupeo mkubwa wa kuhisi hatari na hata harufu na hivyo kujiweka tiyari Kwa ajiri ya mapambano.

Akiona mazingira aliyopo sio salama kwakwe kufanya shambulio hujiondokea kabla hujamfikia Wala kumuona.

Lakini pale ukimuona wewe jua kakusubiri na amejiandaa Kwa muda mrefu sana amegojea tu ulianzishe upate unachostahili.

Kwa matukio hayo mawili ambayo siyo ya kusimuliwa na hili langu Mimi mwenyew Tena mwezi 2 tu mwka huu nakubaliana na hili kuwa Hawa nyoka ni wapole na ni hatari.

Tukio la wale watoto wawili na ng'ombe wao. Sisi ndo tulikuwa wa kwanza kumuona yule nyoka na ilikuwa Hivi.....

Siku Moja tunaenda machungani katikati ya njia kulikuwa na mti flan Hivi kama kichaka (ipo miti Ina randa na kutengeneza kichaka kizito)

Tulipitisha mifugo yetu yote salama na sisi wenyewe tukapita salama mtu wa4 ndo akatumbia oneni yule nyoka tukarudi kumtazama asee alikuwa mrefu sana na ametulia kama hajui kinachoendelea...

Tulichokifanya ni kwenda kuwambia wakubwa wetu karibu na eneo lenyewe. Na walipokuja wakamuona na kumtambua walitumbia ondoeni ng'ombe na mifugo yenu hapa tukafanya hivo.

Nao walipoona tumeondoka waliondoka pia bila kumfanya chochote.

Bahati mbaya sana Kwa wenzetu siku chache mbele wao walipo muona tu ujasiri uliwaingia na kuanza kumshambulia huo ndo ulikuwa mwisho wao na ng'ombe wao pia.

Yowe lilipigwa nyoka huyo akauliwa.

Nimekuja kuomba ama kufundishwa njia/mtego Ili nimuue bila kuathiri watu wa maeneo hayo.

Msitu huu nimepanga kufugia nyuki Kwa wingi lakni kinacho niogopesha ni uwepo wa black mamba kwenye eneo hili.

Eneo ni zuri sana Kwa nyuki kwani maji yapo si zaidi ya mita250 na nyuki ni wengi sana hasa kwenye mapango ya miti,mawe na wengine hujitengenezea asali juu ya mti tu.

Najua humu Kuna watu wa maliasili na wataalamu wa maswala haya naombeni namna ya kumuondoa huyu mdudu na nimeambiwa wapo wawili.

Wapo walio waona Kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti na usiku hupiga kelele zao Kwa kupokezana wasi wasi wangu zaidi watazaliana na kuongezeka zaidi.

Ahsanteen sana.

View attachment 2945391
Chomeni mipira ya tairi za magari chomeni mfululizo siku 7 hawatakaa tena huo msitu watahama kabisa..
Tena mkidondosha na oil chafu ndio kabisa

Tahadhari ukiwasha moto wa tairi muondoke kabisa eneo hilo maana mmeanzisha vita vya 3 vya dunia na hao nyoka..
 
Koboko huwa anagonga kichwani..Wazee walikuwa wanafanya hivi;
Wanachemsha Choroko na zikiwa zimeiva na za moto..zinawekwa kichwani zikiwa za moto kwa mtu mwenye ujasiri anaenda eneo alilokuwepo huyo Nyoka na kumchokoza...si atakuja kwa hasira na kumgonga mhusika kichwani...hapo atakuwa ameingiza kichwa chake kwenye chungu cha Choroko za moto na kufa.
Ila..yataka Moyo.
 
Nakumbuka ile story ya zamani, mtu alijitishwa jungu la uji wa moto akapita nalo msituni alipo, akajitokeza amkonge kichwani akayavaa mauji ya moto akafa.
hiyo ni kubetia maisha yako mkuu

huku kazini kuna motto wetu huwa tuna sema ZERO HARM{ KUTOKUPATA MADHARA} yaani unapotoa msaada hakikisha kwanza wewe mwenyewe upo safe
 
Binafisi na amini wapo wengi lakini kwa mashuhuda wamewahi onekana wawili na huenda huwa huwa wanaona wengine wao wanajua ni haohao wawili. yahitaji moyo sana sema madogo mle mle ndo huenda chungia mbuzi
NYoka wenye sumu Kali huwa Wana ai bu sana unaweza Kuta wanakuona Kila siku ila wanajisepea zao kujificha!

Nyoka ambaye ana hatari zaidi shambani ni puff adder na Hawa vipers mara nyingi hupendelea kutulia sehemu Moja hasa kwenye njia kuota jua hivyo ikitokea kumkanyaga imeenda iyo
Ila Hawa wa elapidae family akina koboko,boomslangs na cobra wanatimua mbio! Unless uwabane wakose namna ya kusepa ndio wataanza kujilinda kwa sumu zao
 
Chomeni mipira ya tairi za magari chomeni mfululizo siku 7 hawatakaa tena huo msitu watahama kabisa..
Tena mkidondosha na oil chafu ndio kabisa

Tahadhari ukiwasha moto wa tairi muondoke kabisa eneo hilo maana mmeanzisha vita vya 3 vya dunia na hao nyoka..
Hiko ndo nawaza nikifanye pamoja na mayai ya kuchemsha
 
NYoka wenye sumu Kali huwa Wana ai bu sana unaweza Kuta wanakuona Kila siku ila wanajisepea zao kujificha!

Nyoka ambaye ana hatari zaidi shambani ni puff adder na Hawa vipers mara nyingi hupendelea kutulia sehemu Moja hasa kwenye njia kuota jua hivyo ikitokea kumkanyaga imeenda iyo
Ila Hawa wa elapidae family akina koboko,boomslangs na cobra wanatimua mbio! Unless uwabane wakose namna ya kusepa ndio wataanza kujilinda kwa sumu zao
nakubali
 
Koboko huwa anagonga kichwani..Wazee walikuwa wanafanya hivi;
Wanachemsha Choroko na zikiwa zimeiva na za moto..zinawekwa kichwani zikiwa za moto kwa mtu mwenye ujasiri anaenda eneo alilokuwepo huyo Nyoka na kumchokoza...si atakuja kwa hasira na kumgonga mhusika kichwani...hapo atakuwa ameingiza kichwa chake kwenye chungu cha Choroko za moto na kufa.
Ila..yataka Moyo.
hapo ni kubetia maisha asee
 
Back
Top Bottom