Kwenye ndoa za kikristo uasherati pekee ndio uliruhusiwa kuvunja ndoa, kwanini wakristo huvunja ndoa kwa sababu zingine ambazo hazijaruhusiwa?

huku kuna mijitu mijinga yani inalazimisha maana sizo kwa neno uzinzi na uasherati
Uzinzi ni kwa mwanandoa aliyechepuka
Uasherati ni kwa watu waliojamiiana na hawana ndoa

ngoja niwagoogle ie ili muelewe maana nyie ni vizazi vya google Ni tofauti gani kati ya uasherati na uzinzi?
Kama hamjaelewa na hapo basi.

Ila ndoa ya KIKRISTO nadhani ningependa kuzungumzia za Katoliki hata kama mke au mumeo kalala mara mia mbili ndoa haiwezi kuvunjwa hata siku moja. Ndoa inayovunjwa kirahisi ni ndoa ambayo haknashiriki tendo la ndoa na bado kanisa linaweza kuvunja hiyo ndoa ukakaa kifungoni hata miaka miwili ndo upate kibali cha kuoa tena. .

Ndoa inaweza kuvunjwa pia kama mke na mume mna matatizo ya kimaumbili, mfano penis kubwa sana mwanamke anashindwa kufurahia tendo au vagina ndogo sana mwanaume anashindwa kuingiza uume. Ila kanisa halijaangalia wale wanawake wenye nyuke kubwa na mwanaume kibamia. Ndoa hizi mkipeleka malalamiko basi yatapokelea na mnaweza kuta ikavunjwa baada ya miaka hata mitatu mnapewa muda wa kulikabili tatizo. .

Kama hamtaki kufundishwa na hamkuelewa kwa sababu ya ubishi haina haja ya kureply potezea. Ndoa inatenganishwa kwa kifo tu, hayo mengine ni nadra sana hata mkitengana kanisa linawatambua kuwa nyie ni wanandoa. Ngoja niwaongezee neno moja, katika sakramenti za kanisa nyingi zinakuwa anatoa Padri lakini sakramenti ya ndoa ni maagano mnayofanya wewe na mkeo, Padri hausiki yeye anakaa kuwa shahidi wa maagano mnayowekeana kati ya mume na mke. .
Mada nduri, shukrani sana. .
 
Kwanza huu hujaunukuu full. Ukinukuu kuanzia ulipoanzia utagundua hauhusiani na mada hii!
 
Uasherati unafanywa na watu wasio na ndoa, bali uzinzi ni kwa wale wenye ndoa
 
Uasherati ni neno pana. Linajumlisha uzinzi, puli, ushoga nk nk.
 
Kwasababu dini ya kweli ni moja tu ilokuja na muongozo wake kutoka kwa Muumba

Izo nyengine ni dini za watu ambazo zina mapungufu mengi mnoo

Atakaenipinga aje na facts
Soma dini ya kweli
Muhammad anaulizwa na mtu wake wa karibu kabisa je nikimkuta mke anapigwa machine na mwanaume mwingine je niwape mda mpaka nikatafute mashahidi wa 4, Muhammad akajibu ndio 😂😂😂😂

Hadith
That Sa'd b. 'Ubadah said to the Messenger of Allah (ﷺ) : What do you think if I find with my wife a man ; should I give him some time until I bring four witnesses ?" He said: "Yes". Sunan Abi Dawud 4533
 
Naona ilo bandiko limekubana ww ulolitoa
M sibishani
Hlf ww mgalatia kma zimeruka ivi
 
Naona ilo bandiko limekubana ww ulolitoa
M sibishani
Hlf ww mgalatia kma zimeruka ivi
Limekubana , kumbuka Muhammad kasema bila mashahidi wa4 walioona machine ikipigwa ushahidi haukubaliki , ndio akamwambia huyo jamaa ukimkuta waombe waendelee ukalete mashahidi muwe wa4 🤣 😂

Hadith
That Sa'd b. 'Ubadah said to the Messenger of Allah (ﷺ) : What do you think if I find with my wife a man ; should I give him some time until I bring four witnesses ?" He said: "Yes". Sunan Abi Dawud 4533

Ukimfumania mke, Muhammad anasema waombe waendelee ukatafute mashahidi wafike wa4 😂 🤣
 
Mkuu Biblia ipo wazi kabisa, Ndoa inatenganishwa kwa kifo na sio uasherati, Huo haukuwa mpango wa MUNGU sheria hio iliwekwa na Mussa Tena kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya binadamu.
 
Mmmh
Zipi hizo tunaomba
 
Moja ya Tabia ya MUNGU Ni kusamehe. Na pia wakikristo ninlazima wawe na moyo wa kusamehe , endapo mwezi wako wa maisha amechepuka Basi msamehe, hata Kama alitanga mbali kea miaka kazaa Basi akirudi kwako umusamehe na hivyo hata MUNGU ndivyo alivyo ndio tabia yake hio ya kusamahe.
Kama ikishidikana Basi wakae hivyo hivyo bila kuoa Wala kuolewa Tena.
 
Hapa umepotea sana ndugu, ni vema kutafakari Neno la Mungu na sio kusoma kama hadithi. Mtume Paulo hakuwahi kutoa maoni yake bali alifafanua SHERIA YA MUNGU.

Pia na na swali dogo kwako, hivi unafahamu uhusiano wa torati na Agano Jipya? Jaribu sana kutafakari maandiko (meditate) kwani ndilo agizo.
 
Nimelazimika kujibu hoja yako nzuri sana baada ya kuona kuna upotoshaji mkubwa kwenye majibu ya baadhi ya prominent members. Nitaanza kwa kunukuu andiko uliosimamia:

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani.
² Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.
³ Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?


> Kumwacha mke kwa kila sababu,yaani hata akipika chakula kibichi waweza kumpa talaka, akijibu vibaya, nk. Sababu hizi ni sawa kabisa na kile ulichoandika:



Hebu tusome Yesu Kristo alijibu nini:

⁴ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
⁵ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?


> Yeye aliyewaumba MWANZO, aya huu inarejea uumbaji wa Mwenyezi Mungu kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Mwanzo (Genesis). Mpango wa Mungu ni mume mmoja na mke mmoja, ndio maana aliwaumba mtu mume na mtu mke.

Umeona hapo haikusemwa ATAAMBATANA NA WAKE ZAKE? Mwanamume anakuwa mwili mmoja na mke wake mmoja tu, kama vile Mungu alivyomuumba Adam kisha akachukua ubavu wa Adam kumtengeneza Hawa. Mke ni ubavu wa mume SIO KICHWA, ndio maana kwenye ndoa ya Agano la Mungu mke ni msaidizi wa mume.

⁶ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

> Mume na mke ni muunganiko unaoleta mwili mmoja. Hoja muhimu hapa, ni wakati gani Mungu humuunganisha mume na mke? Mungu ameweka seal ya Agano la ndoa kwenye bikira ya mwanamke. Mwanamke ajitunzaye bikra yake na kulishika neno la Mungu huyo ana sifa ya mke mwema. Ndoa ya Agano haithibitishwi wala kufungwa kanisani, hili hufanywa nyumbani kwa mume pale wanapoingiliana kitandani na ushuhuda wa damu ya bikira kutolewa hadharani. Hiyo ni damu ya Agano la ndoa kwa Mungu. Tuendelee..

⁷ Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
⁸ Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.


>Ona hapo, linapokuja suala la NABII MUSA, Kristo anabadili hoja kutoka MKE na sasa inakuwa WAKE ZENU. Habari ya wake wengi kwenye Agano la Kale ilikuja kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya Waisraeli, tena hapa inathibitisha Musa ndiye aliyeomba ruhusa hii kwa ajili ya wana wa Israeli. Anaposema lakini tangu mwanzo haikuwa hivi anarejea mpangilio wa ndoa ya Adam na Hawa mkewe, mume mmoja na mke mmoja.

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

> Hiyo hapo sheria ya Mungu kuhusu Agano la ndoa,sio sheria mpya bali Kristo anarejesha kusudi la uumbaji wa Mungu. Hii ni sheria ya bustanini Edeni.

Kila mtu atakayemwacha mkewe.... Hapo hakuna tena mitaala, mke mmoja mume mmoja. Tena iko sababu MOJA tu ambayo Kristo ameruhusu mke aachwe, UASHERATI. Sasa uasherati ni tendo la ndoa pasipo ndoa. Hii ikoje? Ikiwa kijana ametoa posa kwa binti bikira, kisha binti huyo asiwe bikira siku ya kumtwaa rasmi basi alifanya uasherati kwenye nyumba ya baba yake. Binti huyo atapewa talaka na ndoa itavunjika. Hii haitahesabiwa dhambi kwa mwanamume kwani binti alishafunga Agano la ndoa na mwanamume mwingine (damu ya bikira). Labda tunukuu andiko:

Kumbukumbu la Torati 22 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁰ Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;
²¹ na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


>Alama za ubikira ni kifungo cha Agano la ndoa, ndio maana ukisoma zaidi utaona kijana aliyembaka binti atatozwa mahari na atamwoa binti huyo, HANA RUHUSA KUMWACHA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKE.

Mfano mwingine ni ndoa ya Yusufu na Mariamu. Baada ya Yusufu kugundua kuwa Mariamu ni mjamzito alitaka kumtoroka (akiogopa angeripoti kwa Mafarisayo mawe yangemhusu). Alidhani kuwa Mariamu amefanya uasherati kwa vile yeye alikuwa hajamjua bado. Hii ndio maana halisi ya Yesu Kristo kusema ....isipokuwa kwa sababu ya uasherati.

¹⁰ Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
¹¹ Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.


> Kumbuka Mafarisayo ndio waliouliza swali hili la majaribu, lakini jibu la Yesu liliwastua hata wanafunzi wake. Wengine wakaona ni heri kutokuoa (kama vijana wengi humu wanavyolishana huu ujinga) kisa tu, wamenyimwa ruksa ya kutoa talaka. Yesu aliwaambia ukweli, si wote wanaoweza kumudu kudumu kwenye ndoa kama hii isipokuwa WALIOJALIWA. Sasa kama husomi maandiko kwa kutafakari utaacha mambo muhimu zaidi. Waliojaliwa hao ni WANA WA UFALME WA MUNGU. Sio Wakristo, sio wapagani, bali hawakuzaliwa kwa mapenzi ya mwili bali kwa roho. Kuishi kwao ni Kristo na kufa ni faida, hawautumikii mwili bali wanaishi kutenda mapenzi ya Baba.

Ndoa nyingi ingawa zinafungwa makanisani lakini zipo kwenye utawala wa giza, ziko kwenye mamlaka ya shetani!! Unapooa mwanamke mwasherati huoni kuwa umeoa binti ya shetani? Ukioa mwanamke mwenye kiburi mpaka kwa wazazi wake utaanzaje kumlaumu Mungu wakati huyo mwanamke wala hakuwahi kuwepo kwenye ufalme wake? Wewe mwanamke unayeolewa na mwanamume mzinzi, mlevi, mfiraji hujui kama huyo yupo kwenye kambi ya shetani? Unawezaje ewe binti wa Ibrahim kuvutwa na sifa za nje ukaacha sifa kuu ya uchaji wa Mungu? Unafuata mali, uhandsome, perfume? Basi umeingia kwenye kasiri la ibilisi, huko utatendwa sawasawa na kanuni zake. Usitishwe na mtu kuhudhuria kanisani ama kubeba Biblia, hata shetani alinukuu maandiko mbele ya Yesu Kristo mwenyewe!! Hujui kuwa mawakala wa shetani kwa wingi wao na umaarufu wao mkubwa ndio wamesimama madhabahuni leo hii wakiwapoteza yumkini na wateule? AMKA!!

¹² Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Matowashi yaani mahanithi. Wako wa aina tatu:

1. Waliozaliwa hivyo - ili Mungu atukuzwe​

2. Waliofanywa na watu - hawa ni wale walioachwa na wake zao, yaani mojeo akijitenga nawe basi hupaswi kutafuta kipozeo, ishi hivyo hivyo kama hadithi au patana na mkeo upesi!!​

3. Waliojitoa kwa ajili ya ufalme - kama ilivyokuwa kwa Paulo. Hiki ndicho wakifanyacho mapadre wa Kanisa Katoliki pia.​

Maswali?

Mnyama Q
 

Mtu yeyote anayefafanua sheria za Mungu hayo huitwa maoni yake binafsi.
Sheria za Mungu hazifafanuliwi. Zinajieleza zenyewe.
Mungy karuhusu talaka na katoa sheria zake alafu mtu anakuja kufafanua alichomaanisha Mungu Kwa misingi ipi.
Huyo Paulo Hana tofauti na Mimi na Wewe, au kina Mwamposa.
Atakachosema chochote kufafanua amri za Mungu ni maoni yake.
Lakini akisema kama ilivyoandikwa tunasema hapo anazungumza maneno ya Mungu
 
umeupiga nwingi sana, kwa hio ilivyotakiwa ni kwamba ukioa mwanamke asie na bikra unaweza mwacha mda wowote ?
 
excellent!! hata Yesu alikuja kukamilisha wala hakuja kubadili
 
umeupiga nwingi sana, kwa hio ilivyotakiwa ni kwamba ukioa mwanamke asie na bikra unaweza mwacha mda wowote ?
Siku ya kwanza kabisa, Yesu Kristo mwenyewe amesisitiza hilo. Wanawake wanachukulia poa, lakini mke wa ndoa ni mchakato, hutunzwa toka udogo wake
 
Kipi alichopotosha au unachofikiri ni maoni yake tukusaidie? Kuelezea sheria ya Mungu kwa maneno tofauti sio kuikiuka, ndivyo walivyofanya manabii na Mitume. Nio yes he wapi Paulo aliye kama wewe na mimi aliposema maoni yake nami nijifunze neno.
 
Kipi alichopotosha au unachofikiri ni maoni yake tukusaidie? Kuelezea sheria ya Mungu kwa maneno tofauti sio kuikiuka, ndivyo walivyofanya manabii na Mitume. Nio yes he wapi Paulo aliye kama wewe na mimi aliposema maoni yake nami nijifunze neno.

Paulo wa Tarso ni Mtume WA kimataifa, aliyeinjilsha Maeneo ya ugiriki(korinto, Efeso, Galatia,) warumi, Uturuki n.k.
Akiwa nje ya uyahudi alikuwa akitumia zaidi maoni yake kuliko sheria ili awapate watu wa mataifa.
Mfano, Alipokuwa na Warumi wala-nguruwe aliwaambia mtu asiwahukumu Kwa vyakula vyenu, au kutokushika sabato kwenu(hao warumi) kwani walikuwa hawaabudu siku ya sabato
Paulo ni Kama hawa kina Masanja au Mwamposa sio ajabu wakimtumia zaidi katika Aya zao Kwa lengo la kuvuta watu wasiomjua Kristo.

Embu tumsome hapa;
1 Wakorintho 9:20
Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.
1 Wakorintho 9:21
Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
1 Wakorintho 9:22
Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
1 Wakorintho 9:23
Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

Aya ya 9:23 inaeleza kusudio la Paulo ni kupata wafuasi WA Injili na sio Wafuasi WA Mungu.

Alichofanya Paulo ni Kama mhubiri ambaye ameenda Kwa Mtu Malaya au mlevi alafu akamuambia mtu huyo asijali kuhusu umalaya wake, wala mtu asimhukumu Kwa umalaya wake, sio kwamba kahalalisha umalaya Ila anajaribu kumfanya Malaya ajione kuwa amekosea Ila ana -second option ya kutibu.

Lakini kwenye ishu ya Talaka Paulo anakiuka amri ya Mungu inayompa mwanaume ruhusa ya kutoa Talaka Kwa mkewe.
Pia Paulo kwenye amri ya ndoa anatoa maoni yake kuwataka watu Kama wataweza wasioe Jambo ambalo linakiuka sheria kuu ya mungu ya Mwanaume kuoa na kuzaa ili kutekeleza amri ya kuijaza dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…