Kwenye sakata la Mchungaji Kimaro, nasimama na Kiongozi wangu Askofu Malasusa

Kwenye sakata la Mchungaji Kimaro, nasimama na Kiongozi wangu Askofu Malasusa

Dah! Kama Kanisa la Anglikana, kuna maeneo unaweza ukadhani ni Kanisa la Kilokole! Yaani ni full sebene. Wanaita sijui low church! Tofauti kabisa na Kanisa la Anglikana la Tanga.

Hakika misingi ya Kanisa lazima izingatiwe. Mambo ya kuligeuza Kanisa kama mali yako, unaendesha ibada zilizo kinyume na tamaduni za Kanisa; si sawa hata kidogo.
Ulishasema low church. Hivyo ndivyo linapaswa kuwa sasa
 
Je tunawakumbuka
Yatima
Wajane
Wagonjwa
Wenye uhitaji mwingine?
hayo mambo huwezi kuyaleta kanisani,ila kanisani utahubiriwa kuwajali watu hao, kwa hiyo nijambo la mtu binafsi na uelewa wake wa neno la mungu. la sivyo tukilibebesha kanisa mzigo huo duuh, bahasha/vikapu vitakuwa vingi sana mwisho wa siku naamini unajua kitakachotoke
 
Ulichoandika hakieleweki. Kama anataka kufikisha injili kwa mataifa kama unavyotaka iwe ajitoe KKKT, akawe huru kuhubiri bila kufungwa na tamaduni hizi, simple.
Wewe ndo huelewi nilichoandika, rudia tena kusoma vizuri...
 
Wewe ndo huelewi nilichoandika, rudia tena kusoma vizuri...
Usijitoe ufahamu wewe unayemtegemea binadamu ambaye anaweza kuwepo leo na kesho asiwepo. Anayemtegemea Mungu ni yule aliye tayari kumpokea mtumishi yoyote atakayetumwa kuhudumu katika usharika wake. Vinginevyo ni ukosefu wa utii kwa viongozi wa kanisa waliowekwa wakfu. Na hilo ni chukizo kwa Bwana.
 
Ndiyo maana ya huduma na dini safi
Dini safi siyo kumneemesha Mchungaji
dini ni kitu tofauti na kanisa, dini inafundisha tuyatende hayo sisi kama jamii, lakini haielekezi makanisa yafanye hivyo!!!!. ningefurahi kujua wewe kama una bajeti ya kufanya hayo kwa makundi yote uliyoyataja, kama unafanya basi dini na mungu umewaelewa na kuwashika vizuri, hukulitii kanisa, umemtii mungu na dini yako
 
Nilichukiwa sana na ninaendelea kuchukiwa sana na kiongozi pamoja na wenzangu kanisani ninapouliza jambo hili
Huo utaratibu umeletwa ili kuwafanya watu watoe sadaka kwa woga. Kwamba nikitoa kiasi kidogo nitadhalilika. Ndio yale yale ya wenye 5000 walete niwabariki, kisha wenye 10000 walete niwabariki, mara wenye 100,000. Yaani ni kama baraka inauzwa na zina makundi.
 
Umenena
 
ningefurahi kujua wewe kama una bajeti ya kufanya hayo kwa makundi yote uliyoyataja, kama unafanya basi dini na mungu umewaelewa na kuwashika vizuri, hukulitii kanisa, umemtii mungu na dini yako
Kiukweli nasema, natumia sehemu ya kipato changu kusaidia wajane, wagonjwa, yatima na wengineo wenye shida mbalimbali
 
Kiukweli nasema, natumia sehemu ya kipato changu kusaidia wajane, wagonjwa, yatima na wengineo wenye shida mbalimbali
guud kabisa na ubarikiwe, kwa moyo huohuo jitahidi kuwashawishi na wengine utembee nao pamoja kwenye njia hiyo. pia tumia kanisa kutoa ushuhuda wa jambo unalolifanya naamini kuna watu wataguswa na kukuiga. pengine mnaweza kujikuta ndani ya kanisa mna kikundi chenu kwa ajili ya jambo hilo. UBARIKIWE SANA
 
Usijitoe ufahamu wewe unayemtegemea binadamu ambaye anaweza kuwepo leo na kesho asiwepo. Anayemtegemea Mungu ni yule aliye tayari kumpokea mtumishi yoyote atakayetumwa kuhudumu katika usharika wake. Vinginevyo ni ukosefu wa utii kwa viongozi wa kanisa waliowekwa wakfu. Na hilo ni chukizo kwa Bwana.
Kwa hiyo Mtume Paulo alimchukiza bwana kwa kutokutii taratibu za dini ya kiyahudi na kujikita kumhubiri Yesu Kristo kinyume na mafundisho ya dini ya kiyahudi, si ndiyo?
 
Kwa hiyo Mtume Paulo alimchukiza bwana kwa kutokutii taratibu za dini ya kiyahudi na kujikita kumhubiri Yesu Kristo kinyume na mafundisho ya dini ya kiyahudi, si ndiyo?
Acha mbwembwe, kama hatii taratibu za kanisa zinazolifanya liwe hapo lilipo leo aondolewe tu. Utapamba kwa kila mbwembwe, lakini kutokutii ni dalili ya kiburi kinachokemewa sana kwenye Biblia.
 
Acha mbwembwe, kama hatii taratibu za kanisa zinazolifanya liwe hapo lilipo leo aondolewe tu. Utapamba kwa kila mbwembwe, lakini kutokutii ni dalili ya kiburi kinachokemewa sana kwenye Biblia.
Kwa hiyo Mtume Paulo alikuwa mtu wa kibri?
 
Kiufupi kkkt sasa hivi wako kibmaslahi zaidi macho yanawatoka sana kwenye pesa imagine unaenda kanisani unakutana na sadaka hadi ya shukrani ya krismasi wakati hapo hapo kuna shukrani ya wiki 😂😂😂😂😂 inamaana krisimasi ipo nje ya wiki husika inayotolewa shukrani
 
Makanisa yakijitenga na siasa basi watamhubiri Mungu wa kweli
So far makanisa yamepoteza mwelekeo
Malasusa mmm sio kabsaaa
Tuombee majumbani Mungu anasikia
 
Huko Kaskazini huwa wana utaratibu wa kuendesha ibada zao kwa lugha zao za kikabila, (kama umewahi kwenda huko Moshi hata kwa msiba utakuwa unajua) sasa unataka Mmakonde akawe mchungaji huko Moshi au Mbeya atahudumia vipi usharika wake?
Hata kule kwetu Bukoba kwa wacatholic ni ngumu sana padri au askofu ukute ni kabila jingine maana ibada nyingi kule mpaka bible imeandikwa kwa kihaya! Kwanza ukija ukajofanya wewe kiswahili kingi waumini kwenye Misa/ibada zako hutowaona
 
Kwani mkuu umelazimishwa kutoa michNgo Yao wew nenda kanisani bhna kamuabudu mungu ,watu na michango Yao achanao kwani hawalazimishi na Kama umebarikiwa wape mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Usipotoa michango siku ukikata moto hawaji kukuzika. Ndo vitisho vyao hivyo. Na watu wana hamu ya kuzikwa na kwaya na mahubiri ya mapasta na maaskofu utafikiri inawasaidia cho chote. Sad!
 
Umeshindwa tu kuelewa maandiko, wewe ndio hutakiwi kutangaza sadaka yako, itoe kwa Siri, Ila yanayoendelea baada ya wewe kutoa si juu yako. Yule mjane alitoa sadaka kwa Siri, Ila Yesu aliitangaza hadharani, kumbuka Yesu alisimama kwenye chombo Cha sadaka, akiangalia kila anaetoa, na Katia sh ngapi!!!!! Na sijui nani alimpa kazi hiyo!!!!!!! Naam hata leo Yuko Mbele ya chombo Cha sadaka, anaangalia umetoa sh ngapi.
Mkuu kuna watu wagumu kuelewa! Kipindi cha Musa Mungu alitoa kiwango cha sadaka kwenye kila hitaji, mfano kila mwisho wa mwezi njoo na mbuzi Jike na njiwa au ukitaka kufanya kitubio cha dhambi njoo na ng'ombe wawili. Kama ingekuwa sasa angesema njoo na laki 3 ili upate ondoleo la dhambi; sasa nashangaa mtu akipewa bahasha aweke elfu 5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ibada anaona ni jambo geni kumbe tatizo ni yeye hasomi andiko.

Chukulia mahekalu kama ya RC bila kuwa na michango fixed ukaacha kila mtu atoe buku na jero utayajenga lini? Hata wakati wa Suleiman anajenga hekalu la Bwana wana wa Israel walipewa bahasha kila mtu achangie kiasi fulani ili waweza kulijenga siyo kumtegemea mtu mmoja.

Wakristo tukiwa wavivu wa kutoa kwa ajili ya maendeleo ya makanisa yetu tukamtegemea mtu mmoja aje atufanyie tutakuwa kama wenzetu wanaojengewa nyumba za ibada na tajiri mmoja kisa wanazibatiza majina ya wale matajiri. Muhimu ni uzalendo kwa wakusanya michango iende kwenye kulijenga kanisa siyo kupelekea watoto wao kwenye shule za ughaibuni
 
Back
Top Bottom