Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Hi!
Mimi ni mkristo, tena ni kiongozi kanisani kwetu.
Hili suala la sadaka liko wazi kabisa kimaandiko. Maandiko yameweka wazi tutoe vipi, tutoe wapi na muda gani.
Ila baada ya Taasisi nyingi kuzaliwa kwa mgongo wa ukristo sasa misingi ya sadaka kibiblia imeharibiwa na mwanadamu anayetaka kulijaza tumbo lake.
Mfano: Fungu la kumi liliwekwa kwaajili ya Walawi ambao walikosa mgao wa ardhi kule Israel. Hawa Walawi hawakuruhusiwa kujishughulisha na mambo yao ya kiuchumi.
Leo hii mchungaji na askofu wana fremu Kariakoo lakini bado hawaoni haya kula 10% ambayo ilipaswa iende kwa maskini.
Ibada moja ina inakuwa na sadaka mpaka 5. Wanabadilisha jina tu au makapu.
Kapu la sadaka ya ujenzi linafanya nini katika kanisa lililoisha ujenzi?
Kila siku ya ibada ni kukumbushana ujenzi tu.
Moja ya Sababu itakayonifanya nifungue huduma mpya ni suala la sadaka.
Dhulma ya wazi kabisa inafanyika. Ikitokea kongamano la vijana au wamama wataambiwa wajigharamie huku kanisa wanalotoka jumapili Moja tu millioni zaidi ya 2 zinakusanywa.
Hawa manabii na mitume pamoja na makuhani wa mchongo ndo usiseme. Hao Kila siku ni ibada na machangizo.
Uchungaji si kazi ya waliokosa ajira na mitaji.