Kwenye vijiwe vya kahawa, kashata kachori na pweza hivi sasa stori kubwa ni Rais Samia

Kwenye vijiwe vya kahawa, kashata kachori na pweza hivi sasa stori kubwa ni Rais Samia

umekuja kupuma nakijiwe hiki wanasemaje?
hali ni shwari sana uelekeo ni mzuri sana, hakuna hata moja anae mtaja kibaraka wa mabwenyenye ni aibu,

Pamoja njaa kali lakini naona wengi uelekeo ni moja tu 2025 ni kwa Dr.Samia Suluhu Hassan
 
nikiwa kiraia zaidi, nimejumuika na wananzengo vijiwe vya kahawa, kashata, kachori na pweza. Stori na hadithi nyingi zimetekwa na jina la Rais, Dr Samia Suluhu Hassan.
Kwamba huyu mama ni hodari, anajali sana, ana bidii mno ya kazi, anaskiza sana maoni ya wananchi, ni mahiri na makini sana kwenye kuchukua maamuzi magumu na hatua za kuwaletea wananchi uhuru, haki na maendeleo.

Wanadai mama amefungua nchi, fursa zipo na zinaonekana saivi na pesa inapatikana kwa wenye kuchapa kazi kwa bidii na inaonekana.

Ubora wa maisha na urahisi wake, unapanda na kuongezeka siku hadi siku.
Wangwana na watafutaji hawa wasiochoka wala kukata tamaa, kwakweli wanafurahia na kunufaika kwa jitihada na hatua mbalimbali za kiuchumi anazochukua Raisi.

Wadau wanafunguka zaidi kwamba nchi ni tulivu mno, haijawahi kutokea. Ulinzi na usalama wa mipaka, mali na raia ni wa uhakika sana nchini.
Amani imetawala pote Tanzania.

Hii ni sehemu ndogo tu ya makundi mengi sana wanaofurahia na kunufaika na mipango ya serikali ya Dr Samia mthalani bodabodas, mabajaji, madaladala nk.

Wanadai 2025 kama huyu muMama atagombea, basi uhakika wa kura zao ni asilimia 100%.
Wanashauri watoa taarifa na wengineneo bora wakafanye mambo mengine lakini sio uongozi wa nchi hii wakati huu.

Kiufupi huyu muMama anapendwa sana na anakubalika mno vijiweni.

Kupambana na huyu mama ni kupoteza muda.....

Wacha tusubiri,
Time Will tell.....
Labda vijiwe vya dubai na oman
 
kwahio huyumama atahudumu kwamiaka 20?
Hapana ni awamu mbili tu, then atawaachia wengine wa endelee.
Hawezi ongeza hata nukta moja baada ya ngwe inayo anzia Oct 2025 kutamatika...
 
Vijiwe vya kipuuzi unategemea kiongelewe cha maana kweli!?
🤣😂
yaan wauza kahawa, kashata, kachori na pweza ni wapuuzwe?

kuweni waungwana tafadhali, watu wanalisha familia na kusomesha watoto shule unawadharau namna hiyo?

wacha Dr SSH ang'ang'ane nao tu tutakua kwa debe 2025.
 
Sijasema wao, mie nimezungumzia vijiwe vyao, vijiwe vyao vina upuuzo upuuzi, hivyo si ajabu kukaa wanamsifia samia.

Muuza kahawa anaweza kuwa na akili zake saafi kabisa, ila hawezi zuia hizo mada za kipuuzi sababu ndio zinamletea wateja biashara yake inaenda.
 
Pole na samahan kukuelewa vibaya, but it's okay.
Yes sometimes kupo ivo.

sometimes Usimba vs Uyanga sanaaaaa

sometimes Dr Samia Suluhu Hassan sanaaaaa...

sometimes ni hizo vitu zingine makhalakhancha sanaa utacheka ufeee 🤣
 
Back
Top Bottom