Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hali ni shwari sana uelekeo ni mzuri sana, hakuna hata moja anae mtaja kibaraka wa mabwenyenye ni aibu,umekuja kupuma nakijiwe hiki wanasemaje?
Labda vijiwe vya dubai na omannikiwa kiraia zaidi, nimejumuika na wananzengo vijiwe vya kahawa, kashata, kachori na pweza. Stori na hadithi nyingi zimetekwa na jina la Rais, Dr Samia Suluhu Hassan.
Kwamba huyu mama ni hodari, anajali sana, ana bidii mno ya kazi, anaskiza sana maoni ya wananchi, ni mahiri na makini sana kwenye kuchukua maamuzi magumu na hatua za kuwaletea wananchi uhuru, haki na maendeleo.
Wanadai mama amefungua nchi, fursa zipo na zinaonekana saivi na pesa inapatikana kwa wenye kuchapa kazi kwa bidii na inaonekana.
Ubora wa maisha na urahisi wake, unapanda na kuongezeka siku hadi siku.
Wangwana na watafutaji hawa wasiochoka wala kukata tamaa, kwakweli wanafurahia na kunufaika kwa jitihada na hatua mbalimbali za kiuchumi anazochukua Raisi.
Wadau wanafunguka zaidi kwamba nchi ni tulivu mno, haijawahi kutokea. Ulinzi na usalama wa mipaka, mali na raia ni wa uhakika sana nchini.
Amani imetawala pote Tanzania.
Hii ni sehemu ndogo tu ya makundi mengi sana wanaofurahia na kunufaika na mipango ya serikali ya Dr Samia mthalani bodabodas, mabajaji, madaladala nk.
Wanadai 2025 kama huyu muMama atagombea, basi uhakika wa kura zao ni asilimia 100%.
Wanashauri watoa taarifa na wengineneo bora wakafanye mambo mengine lakini sio uongozi wa nchi hii wakati huu.
Kiufupi huyu muMama anapendwa sana na anakubalika mno vijiweni.
Kupambana na huyu mama ni kupoteza muda.....
Wacha tusubiri,
Time Will tell.....
yaan wauza kahawa, kashata, kachori na pweza ni wapuuzwe?Vijiwe vya kipuuzi unategemea kiongelewe cha maana kweli!?
🤣😂
Sijasema wao, mie nimezungumzia vijiwe vyao, vijiwe vyao vina upuuzo upuuzi, hivyo si ajabu kukaa wanamsifia samia.yaan wauza kahawa, kashata, kachori na pweza ni wapuuzwe?
kuweni waungwana tafadhali, watu wanalisha familia na kusomesha watoto shule unawadharau namna hiyo?
wacha Dr SSH ang'ang'ane nao tu tutakua kwa debe 2025.
Ulijiunga na hivyo vijiwe vya ccm baada ya kupewa kofia na t-shirt 😂😂nimejumuika na wananzengo vijiwe vya kahawa, kashata, kachori na pweza.
Pole na samahan kukuelewa vibaya, but it's okay.Sijasema wao, mie nimezungumzia vijiwe vyao, vijiwe vyao vina upuuzo upuuzi, hivyo si ajabu kukaa wanamsifia samia.
Muuza kahawa anaweza kuwa na akili zake saafi kabisa, ila hawezi zuia hizo mada za kipuuzi sababu ndio zinamletea wateja biashara yake inaenda.
Karume ya magomeni au mangamba?Yes,
Leo mguu kwa mguu vijiweni vya kahawa nipo karume saivi hebu pitia apa kwanza kama upo jirani