Kwetu wakristo watoto wa nje wana haki sawa ya kurithi mali kama watoto wa ndani ya ndoa, Dada wa Arusha awape mali watoto wa Housegirl

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Watoto wote wana haki sawa, maamuzi ya wazazi hayana uzito wa kuwabagua, Mali zipigwe pasu kwa pasu kwa watoto wote bila kujali ni wa ndani ya ndoa au nje.

Nimeshangazwa kusikia kinachoendelea huko Arusha kwamba mke wa marehemu bilionea YTemu anajitetea kwamba walifunga ndoa ya kikristo ya mke mmoja kwahiyo akimaliza kuzika anakusanya mali zote za mumewe baada ya kufungua mirathi.

Hii ni kinyume na ukristo, watoto wote huonekana sawa hakuna ubaguzi, hawahusiki na maamuzi ya wazazi wao kuzaa nje ya ndoa.

Kwa nchi kama za ulaya hii migongano huwezi kuikuta, wakristo wengi wana watoto wa nje, Ikitokea Baba kafariki watoto wa nje na wale wa ndoa hugawana mali pasu kwa pasu maisha yanaendelea.
 
Tatizo la kuzaa nje, ndio maana Mo au bakhresa au baba zao huwezi kuwasikia wamezaa nje.

Angalia ngozi nyeusi zote zilizozaa nje au mke zaidi ya mmoja baada ya kufa ni eidha biashara zimekufa au migogoro isiyoisha

Ukianza kutajirika Linda sana mbegu zako ili kulinda utajiri wako Kwa vizazi vyako
 
Nimeshangazwa kusikia kinachoendelea huko Arusha kwamba mke wa marehemu bilionea YTemu anajitetea kwamba walifunga ndoa ya kikristo ya mke mmoja kwahiyo akimaliza kuzika anakusanya mali zote za mumewe baada ya kufungua mirathi.

Hii ni kinyume na ukristo.

Mali za Marehemu inabidi zigawanywe kwa watoto wote wakiwemo wa nje.
Wacha kudanganya watu na kujidanganya mwenyewe. Labda useme sheria za Tanzania.

Sheria za Kikristo. bilia ipo wazi kabisa, hao hata ufalme wa Mungu hawaurithi mpoaka kizazi cha kumi kipite.

Ukiwa mtoto wa nje ya ndoanhuruhusiwi hata kuingoia kanisanai, mpaka vizazi kumi vipite. Ushahidi:

Kumbukumbu la Torati, Mlango 23

2 Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana.
 
Agano la kale hilo, Kulikuwa na sheria za ziada zikiwemo kuosha dhambi kwa kutoa kafara wanyama.
 
Watoto wote wana haki sawa, maamuzi ya wazazi hayana uzito wa kuwabagua, Mali zipigwe pasu kwa pasu kwa watoto wote bila kujali ni wa ndani ya ndoa au nje.

Nimeshangazwa kusikia kinachoendelea huko Arusha kwamba mke wa marehemu bilionea YTemu anajitetea kwamba walifunga ndoa ya kikristo ya mke mmoja kwahiyo akimaliza kuzika anakusanya mali zote za mumewe baada ya kufungua mirathi.

Hii ni kinyume na ukristo, watoto wote huonekana sawa hakuna ubaguzi, hawahusiki na maamuzi ya wazazi wao kuzaa nje ya ndoa.

Kwa nchi kama za ulaya hii migongano huwezi kuikuta, wakristo wengi wana watoto wa nje, Ikitokea Baba kafariki watoto wa nje na wale wa ndoa hugawana mali pasu kwa pasu maisha yanaendelea.
Ukristu hauzungumzii mambo ya kidunia kama mgawanyo wa mali. Hayo waachie watu wa sharia
 
Back
Top Bottom