Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Hizo ni fikra mufu.
Na ndizo zinavyoeleweka na kuaminiwa na wanachi wa kawaida,kwao ni mpambano ni wa Mwakyembe against Mwakipesile+RA+EL, hii ngoma kwa Mwakalinga ni kujiangamiza kifo cha kisiasa moja kwa moja.
 

Fidel,

BAK aliandika kwa ujumla. Mwakalinga na Mwakipesile wapi na wapi? Kumbuka kuwa Mwakalinga na nduguze walihusika kwa karibu sana kumuangusha Mwakipesile kwenye uchaguzi uliopita.

BAK, Mwakalinga anakuja kwa nguvu yake ambayo kaanza kuijenga tangu yuko Secondary. Kwa nini mnafikiri Kyela ni mali ya Mwakyembe? Kama yeye ni Mbunge wa Taifa, si agombee majimbo ya Dar es Salaam? Nina imani itakuwa kwake rahisi kushinda.

Ona Watu walivyomkalia kooni Mwakalinga utafikiri kavunja katiba. Mwakyembe ana haki ya kugombea Kyela. Mwakalinga ana haki ya kugombea Kyela. Let the best WIN. Sasa huu kwa nini watu wanaweweseka na Mwakalinga? Jibu ni moja tu : Mwakalinga ni kama Watusi wa Rwanda. Wale hawaendi vitani kabla hawajajipanga vya kutosha. Ndiyo maana kila vita yao hushinda.

Kama Mwakyembe kaleta maendeleo, watu wanaona. Kama Mwakalinga kaleta maendeleo, watu wanaona. JF haitapiga kura ila ni wananchi. Magazeti wataandika kile wanachokitaka. Manafyale, Kanda2, Mwafrica, Nsesi, Mtindi, Shalom nk nao wataandika wanachokitaka....

BTW: Shalom, kama wewe una RISASI za kummaliza MWAKALINGA, basi wengine pia wanajua MAKOMBORA yalipo ya kummaliza Mwakyembe. Hivyo, usitishe watu kwa vijirisasi vyako. Unajua hizo risasi unaweza zificha wapi.
Unapokuja kwa akina Lowassa na RA, hawa wao sijui wana nini. Ila watakuwa wanafahamu zaidi. Hivyo BAK, Mwakyembe na ushujaa wake, anaishi nyumba ya VIOO, na kibaya ni kuwa alisharusha mawe (Very good 4 Tz) ila na yeye wakianza kumuopolea uchafu wake, asilie MAFISADI.
 

asante Kanda2, ingawa nimekuwa nikitofautiana nawe ktk hoja mbali mbali, lakini leo nakuunga mkono. Mimi simpigii debe Mwakalinga kuwa Mbunge wa Kyela (kwakuwa tayari yupo mpiganaji Mwakyembe at least kwasasa). Bali ninakubaliana nawe ktk mambo haya: -

i) Ni vibaya na ni utovu wa nidhamu kuiweka wazi ID ya mtu pasipo ridhaa yake. Without excuse lazima mods wapitishe rungu japo mvua moja.

ii) Nampongeza sana Ndg. Mwakalinga kuwa moja wa waanzilishi na mfadhili wa JF. Anastahili pongezi kwa kuona mbali na kujitolea ktk mpango mzima wa kutuwezesha kupigania nchi yetu kwa njia ya mijadala na uhamasishaji. Ni ukosefu wa fadhila kumtukana na kumsema vibaya Ndg. Mwakalinga kwa jitihada anazofanya juu ya JF.

iii) WanaJF tuheshimiane na tushauriane pale panapohitaji ushauri siyo kutukanana na kusemana vibaya.

At all JF founders wana-deserve heshma toka kwetu sote.
 

Mwakalinga na Mwakipesile ni damu damu. Ushahidi upo kwenye hiyo story ya uchangiaji pesa wa UVCCM ambao ulibuma baada ya wanakyela kujua the story behind trip ya fisadi Ridhiwani Kikwete.


Mwakalinga amekaliwa kooni kama mwanasiasa yoyote yule Tanzania. Kilichoongeza moto kwenye mafuta (oooppppsss) ni kujihusisha kwake na mafisadi - Lowasa, ROstam na RIdhiwani.


Na ndio maana mimi naweka wazi hapa kuwa Mwakalinga aachane na mafisadi ambao wanafadhili kampeni zake ili awaache wana kyela wachague mtu wanayempenda. Wewe unasemaje?

BTW: Shalom, kama wewe una RISASI za kummaliza MWAKALINGA, basi wengine pia wanajua MAKOMBORA yalipo ya kummaliza Mwakyembe. Hivyo, usitishe watu kwa vijirisasi vyako. Unajua hizo risasi unaweza zificha wapi.

Sikonge, negative kampeni ziko kila mara. Marekani sasa hivi kuna watu wanadai kuwa Obama anataka kuuuwa vizee vikongwe na wanaaminiwa. Chochote kambi ya Mwakalinga itakachokuja nacho sio kipya kwenye lingo la siasa.


Ya Lowasa na RA, Mwakalinga ndiye aliyaleta mwenyewe kwa kwenda monduli kupata baraka za fisadi Lowasa. Hayo mengine ni ya kwako mkuu.
 
Najua unajua unachokifanya Msauzi,ndio hawa ooh ukiniona mimi tu umeshamaliza kata hii...,na hii... na hii...., duh....Msauzi endeleeni kumpiga mwenzenu changa la macho na hii financial crisis........,akili ku mukichwa!!!
 

Hizi tunaita ni pumba Mwakalinga hahusiki kabisa na uanzishaji wa JF msimpe sifa zisizo zake, nyie wapambe wake mnaharibu mataniao ya kisiasa ya Mtanzania kule Kyela

Kwa kukusaidia

Hii nimeitoa kwenye wikipedia

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Tanzania[/ame]
 
Haha haaa ,


Kwa hiyo sasa hii ndio new spin ambayo inatoka kwa fisadi Mwakalinga. Anajaribu kutafuta huruma ya wanabodi kwa vile tu alifiwa na mdogo wake?

Na hiyo ya kumleta Ridhiwani mtasemaje? alikuwa anakuja kutoa pole?

Mie nimekuandikia alifiwa na kaka yake. Wee kwanza UNACHEKA. Halafu mwisho unasema MDOGO WAKE. Duuu, mikono inaanguka. Yaani mtu anachekelea kusikia mwenzake alifiwa na kaka yake?

Hayo ya RIDHIWAN wee shambulia. Huko mie sijasema hata neno moja.

Ila hili la kucheka jamaa kafiwa na kaka yake, tena jamaa alikuwa masomoni URUSI? Na hii habari waweza ithibitisha kwani UBALOZI/Wizara ilishughulikia kuuleta mwili Tanzania na yeye akawa amepewa jukumu la kusafiri na mwili wa Marehemu Tanzania kwa Mazishi. Kama hili unaona ni SPIN, basi nenda wizarani na uulize kama kuna mwanafunzi alifariki Urusi miaka ya 90. Ukipata jibu, njoo NIKUOMBE msahama kwa ku-SPIN kifo ya kaka yake Mwakalinga.
Siku ukifiwa, ukiona watu wanakucheka, kumbuka wee kicheko chako cha leo. Na uzuri wa dunia yetu, Mungu si Athman. Kila la kheri.
 

Sikonge,

Huwa nakuona kama analyst mzuri sana wa mambo ya kisiasa hapa JF (kwa vipimo vyangu). Kitu kimoja naomba nikukumbushe, kifo kwenye familia sio silaha nzuri kwenye mpambano wa kisiasa.

MImi nimefiwa na ndugu zangu wengi tu lakini sitahitaji huruma ya mtu siku nikiingia kwenye siasa. Life ya Mwakalinga sasa hivi ni fair game kwa vile ameingia kwenye siasa. Hayo ya kufiwa umeyaleta wewe na sidhani kama yana sababu za kutosha za kunizuia nisicheke au kuchambua ufisadi wa Mwakalinga.

Asante
 

Asante Masanilo,

Kumbe huyu Mwakalinga sio mwanzilishi wa JF?! Wakome na walegee wale waliokuwa wanajaribu kuipaka hii forum matope kwa maneno yao ya uongo na kizushi kuwa Mwakalinga ni mwanzilishi wa JF.
 


OK,

Kumbe mambo ni kama SIASA za USA siyo?

OK, nilifikiri watu wanaelewashana kumbe ni KUFURAHISHA GENGE?
 
OK,

Kumbe mambo ni kama SIASA za USA siyo?

OK, nilifikiri watu wanaelewashana kumbe ni KUFURAHISHA GENGE?

Ekzaktli -- hivyo ndivyo nilivyohitiimisha uliposema kuwa kambi ya Mwakalinga ina mambo mengi sana ya Mwakyembe (ninayaita negative campaign) itakayoyaleta wakati wa uchaguzi.

Katika hili, wao wayalete tu kwani hawatakuwa wa kwanza kufanya hivyo na wala hawatakuwa wanafurahisha genge lolote lile - zaidi ya genge la mafisadi - EL, RA na Mwakipesile.
 
Kuna ban zaidi ya 20 zinakuja tokana na name calling katika topic hii.

Sheria hii imezingatiwa katika kufanya maamuzi haya:

2 - Profanity:
Profanity is not tolerated in the board, some words will be censored, also there is to be no name calling, doing so will give you a warning, and then a ban if you continue.

Nasikitika kwa watakaoathirika na mamauzi haya.

Atakayeendelea kukiuka atapata Server ban and that will be a permanent one.
 

Masanilo,
Sijui umeandika kwa kutaka kujua au unatania. Maadamu wee ndugu yangu na hatuna utani basi nitakueleza. Kwa sasa jamaa anafanya kazi kampuni moja kubwa sana la electronics na mambo ya simu. Mapema kabla ya hapo alikuwa Lucent. Sasa basi hizi kazi zao mara nyingi unaweza kuwa UK ila unashughulika na mitambo ya simu ya Australia, Argentina, Russia, German nk. Kutokana na uzoefu wake kikazi, amekuwa akipelekwa nchi tofauti za Ulaya ili kwenda kuchukua VIZA, hasa hii viza ya SCHENGEN. Mwezi wa tano aliniambia alikuwa anatakiwa kwenda kuchukua tena VIZA. Hivyo wakati Lowassa yupo German, tayari alikuwa na viza ya mwaka mzima. Huwa wanampatia ya muda mrefu kutoka na safari zake za mara kwa mara ndani na nje ya Europe.

Pia kwa Mtu mkali wa IT, hivi anahitaji kwenda hadi Monduli ili kumuona Lowassa? Kumbuka Lowassa sasa anajenga sijui TV? Inamshinda Laptop moja na Internet ya high speed ili aongee na Mwakalinga? Kama ni pesa si wangelienda kuchukua wapambe? Au Lowasa angelikwenda kumuona UK.

Na wee Mwafrika, acha ushama wako. Nenda kwa Michuzi, utaona picha ya Lowassa akiwa German kwa matibabu. Alienda na kurudi salama. Nani ampige mawe Richmonduli?
 
Nimesema Nsesi aka mwakyembe kwanini anamlaumu mwezake kupiga siasa jf ilihiali yeye anapiga hapa siasa.?
....naona mboko haram keshakula chake....
 

SIkonge,

Chenge anabrag sana kuwa kasoma Havard. Ufisadi haujali elimu wala uzoefu wa kuishi nje ya nchi. Kama kambi ya Mwakalinga inataka kutumia haya kama kigezo cha kushinda ubunge basi inabidi wajipange upya.


Tatizo halikuwa kwa Mwakalinga .... h aha haha ... Tatizo lilikuwa kwa fisadi Lowasa ambaye hana clue ya mambo ya IT.

Na wee Mwafrika, acha ushama wako. Nenda kwa Michuzi, utaona picha ya Lowassa akiwa German kwa matibabu. Alienda na kurudi salama. Nani ampige mawe Richmonduli?

Natumaini hapo ulitaka kumaanisha ushamba? Suala la Lowasa kuwa German kwa matibabu lingezuia wapopoaji (wa mawe) wasitimize azma yao maana hata wajerumani wasingefurahi kuona mtu mwenye mvi na mgonjwa akipipopolewa mawe.

Kupitia Monduli ndiyo ilikuwa njia pekee kwa Mwakalinga na Lowasa kukutana bila hofu wala shaka yoyote.
 
Hivi hamjui Mwakyembe ni BABA SUKARI? Hebu oneni hapa.

(TANGAZO LA BIASHARA).

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=dp4_Xdsl050"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…