Anaufadhili mtandao huu?
Waliochangia kwa mwaka huu wanapatikana hapa:
Hakuna mfadhili zaidi ya hao! Wengine wamechangia miaka ya 2007 nao hakuna alochangia zaidi ya $200!
Haya maneno ya ati ni mfadhili wa JF au mwanzilishi sijui yanatoka wapi! Labda kama yumo kwenye list hiyo.
Invisible nashukuru kwa maelezo lakini inasemekana kuwa huyu jamaa anaufadhili mtandao huu,imeandikwa kwenye magazeti yanayoheshimika sana hapa nchini (like Mwananchi la jumatatu).
Nadhani si mimi tu peke yangu niliyenazo habari hizi nawe umezisikia mahali pengine. Habari hii ilivyoandikwa inaonesha kama ufadhili wake ni wa kipekee tofauti na uchangiaji wa hao uliowataja.
Pia jamaa anavyozungumziwa humu JF ni kama vile ni mtu maarufu sana hapa ndani kama akina Mwanakijiji na hiyo inaleta hisia kwamba labda huyu mtu kweli ni kama magazeti na vyanzo vyetu vingine visemavyo.
Nina imani na JF,sitaki kuamini kuwa tunataka kuchukua nafasi ya kuuza wagombea,lakini tuwe makini. Wachangiaji wa fedha wawe wazi na wawekwe wazi ili tuondoe "
conflict of interest". JF inaheshimika sana,kama mtu akisoma habari jinsi ilivyoandikwa kwenye gazeti na akaona jinsi Mwakalinga anavyouzwa humu JF ataamini kuwa mtandao huu umegeuka kama sehemu ya kampeni za baadhi ya wagombea.
JF ina members wengi sana na hata wanasiasa wanaweza kuitarget kama sehemu ya kujiuzia. Pia JF ni chanzo cha habari nyingi sana kwani mabo mengi yanatoka hapa ndiyo tunayaona magazetini. Kama mgombea akiweza kuteka JF ana weza kuteka magazeti mengi yanayochukua habari zake hapa.
Suala la Mwakalinga lilikuwa closed topic,iweje lirudishwe kama new post wakati lilishaongelewa na kufungwa. Mwakalinga ni nani mpaka akapewa publicity kubwa kiasi hiki katika JF? Hili linanipa mashaka kwa nafasi ya huyu bwana katika JF. Tunaomba ukweli wa jambo hili kama inawezekana.
JAMII FORUMS Where We Dare to Talk Openly!