KijanaHuru
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,822
- 2,320
- Thread starter
- #41
sahihi sana ulichokisema ndugu umezungumza ukweli mtupu kabisa,Unaingilia ugomvi kusuluhisha. hapo hauna laana. Kwa mfano mzee akikuambia uende ukaibe, ukigoma akakuambia atakulaani, utaenda kuiba? Baba anampiga mama nisingiilie kuwaamua kisa nitalaaniwa. Haiwezekani.
Je, ni sahihi wewe kumpiga mkeo au kumtukana hata kama amekukosea? Je, maandiko ya vitabu vya dini vinasemaje?
Tumekuwa na hofu na dhana potofu kuwa ni sahihi kutoingilia ugomvi wa wazazi kwasababu tutalaaniwa ndiyo maana familia za kiafrika zimejaa umasikini, chuki na kiburi.
Baba anatelekeza familia, anaenda kusokojulikana tena akifika huko anaoa. Anawasahau, inapita miaka mingi. Hajui mnakula nini wala mnavaa nini.
Baadae baada ya kukua na kufanikiwa anakuja kwasabb mila za kiafrika hurusiwi kumhoji wala kumkataa mzazi. Anaanza kukupangia kumhudumia. Hapana aisee kupata laana ni pale unapokiuka matendo ya haki (matendo mema) ya mzazi.
Watu wengi wanafikiri kupata laana ni kutoka kwa wazazi ila laana unaweza kuipata kwa mtu yoyote na kutenda matendo machafu. Wewe unamwingilia mwanamke kinyume cha maumbile, ushoga, unampiga mkeo na kunyanyasa watoto wako hizo zote ni laana.
ila kumbuka hili kazi ya moyo haiwezi kufanywa na miguu hata siku moja,
baba kukutuma kuiba na kukataa hilo sio ugomzi wa wazazi,
baba anampiga mama mbele yako suluhisho la kwanza kaite majirani ndio waje kuamulia suluhisho la pili amulia ugomvi lakini usije ukaingia sehemu yoyote ya kujua huyu ana haki au hana haki, usije ukamchukia mzazi akikushushia pamoja nawe hicho kipigo.
kuna siri kubwa ya wazazi katika ulimwengu wa kiroho na kimamla na kiutawala ambayo watu huwa hatuijui kabisa na usipoijua unaweza ona ni haki kabisa,
rudi katika kauli yangu usiingilie ugomvi wa wazazi hata kama unaona kabisa nani anamakosa ugomvi wa wazazi watoto hauwahusu hata siku moja,
baba kutelekeza familia hilo linahitaji busara yako na hekima yako kwa kufuata umelelewa vipi mazingira yamekukuzaje na jamii yako imekufunda namna gani na shida ya kufanya familia ikatelekezwa.
point yangu nikukumbusha tu kutokuingia ugomvi wa wazazi hakuna sababu yoyote ya mtoto inayokubalika kwa namna yoyote ile kumfanya akaingilia ugomvi wa wazazi,
nadhani sheria huwa unazijua mkuu