Laana: Usije ingilia ugomvi wa wazazi hata siku moja

Laana: Usije ingilia ugomvi wa wazazi hata siku moja

Ushawahi kuona mzazi ambae haelewek.. unagraduate anachukia.. unaenda kutafuta maisha anachukia.. narud na picha ya graduation nyumban wanaweka chini ya kabati.. wewe ni mtoto wake likija kwny swala la kuwakomoa ndugu zake tu.. ataanza ee mwnanangu amesoma.. mwanangu hv.. jana tu baada ya kunikazia nmehangaika mwnyw nimepata kibarua kwa muhindi.. anakuja ba idea eti ooh nenda jkt sasa.. kuna rafk zangu watakuunganisha ukimaliza course.. kweli kijana wa miaka 27 inaenda 28 unamwambie jkt leo.. alikua kwako toka akiwa na miaka 25 amemaliza degree hakuna alichosaidia zaidi ya kuniuliza najitolea kwny mashirika kwa faida gani.. Sasa huyo nae ni Baba au laana kamili.. mama yangu kafariki nna miaka miwili lakn tokea naanza kupata akili naskia negativity za mama kutoka kwa Baba.. nahajawah kwenda hata kuangalia kaburi.. watu wanapga wazazi wao kwa sababu.. na kuna wazazi wana nuksi sana.. tena sanaa
Pole Mkuu
Huwa inauma sana hasa mzazi aliyekuzaa kushindwa kukupa support hata ya mawazo tu na faraja.
Mimi mwaka saba huu sijapata kazi ila napata support kwa wazazi namshukuru Mungu tena kimawazo na na wakati mwingine kifedha.
Hii inanisaidia sana hasa kunipunguzia stress pale mambo yangu yanapoenda hovyo angalau mzazi anakupa moyo na kukufariji ila usiombe mambo yawe mabaya halafu mzazi naye akugeuke aisee unaweza changanyikiwa.
 
Acha tu.. mshukuru sana Mungu kwa wazazi wako ase.. sisi wengne huku hakuna rangi tunaacha kuiona
 
Kwaiyo Hadi mama yako au Baba yako akiuliwa ndyo uje kumchukia Baba yako kweli vichaa ni wengi
 
Inaonekana mtoa thread ni baba fulani hivi wa hovyo sana kwenye familia yake, hivyo anatafuta huruma ya kuhalalisha upuuzi wake humu....! Hata kama ni mzazi tenda haki kwa familia yako utalipwa haki, jidanganye kunyanyasa familia yako ukijipa moyo eti utawaapa laana wanao wakikukataa, utasubiri saana....! Ukiona mpaka unaingia kwenye mgogoro na mwanao ww mzazi ndio unayeweza kumaliza huo ugomvi, sasa bao lako likuzidi nguvu mpaka ufikie hatua ya kumwekea kinyongo mwanao uliyemleta duniani kwa starehe zako.

Wazazi nao wana wajibu wa kuwaheshimu na kuwapenda watoto..! Na mzazi aliyetimiza wajibu wake kikamilifu hawezi kuingia kwenye ugomvi na familia yake
 
kukwama kimaisha haina maana kuna mzazi mmoja kakukosea, kila unapokwama haina maana kuna mzazi ulimkosea hivyo maisha yanakufanya ukwame sababu ya hiyo laana.

kuna kitu kimoja cha muhimu nikukumbushe kabla haujafika mbali, Africa tumekuwa ni watu wa mila,jadi pamoja na desturi zetu hizi mambo zimekuwepo toka enzi na enzi,
kuna misingi mingi sana iliyomo katika hizi vitu hatuijui sababu yakukulia katika mazingira yasiokuwa rafiki katika kujifunza na kuelewa nini tunapaswa kufanya.
Haya mambo yalitufanya wa africa tuweze kuishi maisha ya kiroho ambayo ndio moja kwa moja yameumana na mifumo ya asili kabisa yanayohusu ulimwengu huu.
Nakudokeza na siri hii sasa jambo la kwanza linalotufelisha katika mafanikio yetu binafsi ni kushindwa kujua namna gani tunaweza kutumia wazazi wetu katika kufanikiwa,
jambo la pili nakudokeza mzazi akikukunjia hakuna mungu wala shetani anayeweza kukusikiliza katika ulimwengu huu na sayari zote kwa ujumla.
huyo mungu mtoa laana uliyemsema angeweza kukulaani moja kwa moja maana yake hata pesa angekupa direct utoboe maisha.

sasa akili yako inajua kuwa kila mwenye maisha magumu anakosana na wazazi kitu ambacho tayari upo kinyume kabisa na wala sijasema hivyo mimi nimeongelea matokea ya hii laana ilivyo.
sio kila ugumu wa maisha unatokana na laana za wazazi hata siku moja ila kuna baadhi ya watu hiki kitu kinakuwa kinawatafuna.
Acha kudanganya watu mkuu hakuna binadamu wa kukukunjia na kuziba riziki zako, kama tu ukiwa mtu wa haki...! Ila kama ni mtu usiyetenda haki sio mzazi tu anayeweza kukuaribia ni mtu yeyote tu uliyemtenda vibaya, tenda haki uishi kwa amani na furaha
 

1:Wazazi wakiafrika hutumia neno laana Kama silaha yao dhidi ya watoto wakati wanapokuwa na mitazamo mikubwa kuwazidi hufunya vizazi vyao kudumaa kimaendeleo na ndio Sababu ya kutokuendelea kumbe ni Sababu ya wazazi wapumbavu

2: kwenye upendo hakuna laana, hivi vitu huendekezwa na familia maskini ambazo hazina umoja katika kujikomboa na umaskini.

Kumbuka: Unapoamua kumlaani mwanao ni bora tu ungetumia kondom wakati wa starehe zako maana unamwamshia giza nene katika safari ya Maisha yake

 
Back
Top Bottom