Laana: Usije ingilia ugomvi wa wazazi hata siku moja

Pole Mkuu
Huwa inauma sana hasa mzazi aliyekuzaa kushindwa kukupa support hata ya mawazo tu na faraja.
Mimi mwaka saba huu sijapata kazi ila napata support kwa wazazi namshukuru Mungu tena kimawazo na na wakati mwingine kifedha.
Hii inanisaidia sana hasa kunipunguzia stress pale mambo yangu yanapoenda hovyo angalau mzazi anakupa moyo na kukufariji ila usiombe mambo yawe mabaya halafu mzazi naye akugeuke aisee unaweza changanyikiwa.
 
Acha tu.. mshukuru sana Mungu kwa wazazi wako ase.. sisi wengne huku hakuna rangi tunaacha kuiona
 
Kwaiyo Hadi mama yako au Baba yako akiuliwa ndyo uje kumchukia Baba yako kweli vichaa ni wengi
 
Inaonekana mtoa thread ni baba fulani hivi wa hovyo sana kwenye familia yake, hivyo anatafuta huruma ya kuhalalisha upuuzi wake humu....! Hata kama ni mzazi tenda haki kwa familia yako utalipwa haki, jidanganye kunyanyasa familia yako ukijipa moyo eti utawaapa laana wanao wakikukataa, utasubiri saana....! Ukiona mpaka unaingia kwenye mgogoro na mwanao ww mzazi ndio unayeweza kumaliza huo ugomvi, sasa bao lako likuzidi nguvu mpaka ufikie hatua ya kumwekea kinyongo mwanao uliyemleta duniani kwa starehe zako.

Wazazi nao wana wajibu wa kuwaheshimu na kuwapenda watoto..! Na mzazi aliyetimiza wajibu wake kikamilifu hawezi kuingia kwenye ugomvi na familia yake
 
Acha kudanganya watu mkuu hakuna binadamu wa kukukunjia na kuziba riziki zako, kama tu ukiwa mtu wa haki...! Ila kama ni mtu usiyetenda haki sio mzazi tu anayeweza kukuaribia ni mtu yeyote tu uliyemtenda vibaya, tenda haki uishi kwa amani na furaha
 

1:Wazazi wakiafrika hutumia neno laana Kama silaha yao dhidi ya watoto wakati wanapokuwa na mitazamo mikubwa kuwazidi hufunya vizazi vyao kudumaa kimaendeleo na ndio Sababu ya kutokuendelea kumbe ni Sababu ya wazazi wapumbavu

2: kwenye upendo hakuna laana, hivi vitu huendekezwa na familia maskini ambazo hazina umoja katika kujikomboa na umaskini.

Kumbuka: Unapoamua kumlaani mwanao ni bora tu ungetumia kondom wakati wa starehe zako maana unamwamshia giza nene katika safari ya Maisha yake

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…