Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mama Samia leo asubuhi aliamkia Soko la Karikaoo kuangalia biashara inavyokwenda na kuzumgumza na viongozi wa soko.
Allah ana rehma zake na hutukumbusha mengi kwa njia ambazo mtu huwezi kutegemea.
Hapo aliposimama kwenye gari Rais Mama yetu Samia Soko la Kariakoo alikoelekeza sura yake ni Mtaa wa Swahili na kona ya Tandamti na ameupa mgongo Mtaa wa Swahhili na Mkunguni.
Hapo mbele yake ndipo ilipokuwa Ofisi ya Market Master Abdulwahid Sykes miaka ya 1950 Tanganyika inaanza harakati za kupigania uhuru wake kutoka kwa Waingereza.
Soko la Kariakoo na ofisi hiyo palikuwa moja ya ngome za harakati dhidi ya ukoloni.
Bahati mbaya historia hii haifahamiki ila kwa wachache sana.
Sehemu nyingine ambako vijana wanaharakati walikuwa wakipita kwa hili au lile katika siasa za ukombozi ilikuwa Ilala Welfare Centre ofisi ya Hamza Mwapachu.
Vilevile wanaharati walikuwa wakikutana nyumbani kwa Dossa Aziz Mtaa wa Congo na Mbaruku na nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na nyakati za jioni wakikutana Tanga Club Mtaa wa New Street na Mkunguni.
Ilikuwa hapo sokoni Kariakoo ndipo Julius Nyerere akija kumuona Abdul Sykes ofisini kwake kuanzia mwaka wa 1952 na ndipo alipojuana na wazee mashuhuri wa mji maarufu kupita wote ni Mshume Kiyate.
Mzee Mshume akaunga uhusiano na Nyerere uliopitiliza siasa za TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika akamfanya Nyerere mfano wa mwanae.
Kueleza mchango wa Mzee Mshume katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kutarefusha hii makala.
Hapo sokoni ndipo Mwalimu Nyerere alipofahamiana na Shariff Abdallah Attas kwa karibu sana kiasi safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 mkewe Shariff Attas, Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mmoja wa akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege pamoja na Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee.
Hawa ndiyo walikuwa wanawake pamoja na Bi. Hawa Maftah na Bi. Halima bint Salum kwa kuwataja wachache waliojenga msingi wa akina mama kuipa TANU nguvu za kutisha katika mikutano yake Viwanja Vya Mnazi Mmoja na katika sanduku la kura.
Hii ndiyo iliyokuwa Kariakoo ambayo ile ofisi ya Abdul Sykes pale Kariakoo ilimpa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa Tanganyika.
Itapendeza sana kama CCM itaweka ukumbusho pale sokoni kama kumbukumbu ya wazalendo hawa wake kwa waume.
Vinginevyo tutabaki kuwa taifa lisilo na historia inayoeleweka ya ukombozi wake.
Picha ya Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 Ofisi ya Market Master ni hilo jengo dogo mkono wa kulia.
Picha ya chini kabisa Mshume Kiyate na Julius Nyerere, 1964.