Laiti Rais samia angeijua historia ya soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Laiti Rais samia angeijua historia ya soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Mama Samia leo asubuhi aliamkia Soko la Karikaoo kuangalia biashara inavyokwenda na kuzumgumza na viongozi wa soko.

Allah ana rehma zake na hutukumbusha mengi kwa njia ambazo mtu huwezi kutegemea.

Hapo aliposimama kwenye gari Rais Mama yetu Samia Soko la Kariakoo alikoelekeza sura yake ni Mtaa wa Swahili na kona ya Tandamti na ameupa mgongo Mtaa wa Swahhili na Mkunguni.

Hapo mbele yake ndipo ilipokuwa Ofisi ya Market Master Abdulwahid Sykes miaka ya 1950 Tanganyika inaanza harakati za kupigania uhuru wake kutoka kwa Waingereza.

Soko la Kariakoo na ofisi hiyo palikuwa moja ya ngome za harakati dhidi ya ukoloni.
Bahati mbaya historia hii haifahamiki ila kwa wachache sana.

Sehemu nyingine ambako vijana wanaharakati walikuwa wakipita kwa hili au lile katika siasa za ukombozi ilikuwa Ilala Welfare Centre ofisi ya Hamza Mwapachu.

Vilevile wanaharati walikuwa wakikutana nyumbani kwa Dossa Aziz Mtaa wa Congo na Mbaruku na nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na nyakati za jioni wakikutana Tanga Club Mtaa wa New Street na Mkunguni.

Ilikuwa hapo sokoni Kariakoo ndipo Julius Nyerere akija kumuona Abdul Sykes ofisini kwake kuanzia mwaka wa 1952 na ndipo alipojuana na wazee mashuhuri wa mji maarufu kupita wote ni Mshume Kiyate.

Mzee Mshume akaunga uhusiano na Nyerere uliopitiliza siasa za TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika akamfanya Nyerere mfano wa mwanae.

Kueleza mchango wa Mzee Mshume katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kutarefusha hii makala.

Hapo sokoni ndipo Mwalimu Nyerere alipofahamiana na Shariff Abdallah Attas kwa karibu sana kiasi safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 mkewe Shariff Attas, Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mmoja wa akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege pamoja na Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee.

Hawa ndiyo walikuwa wanawake pamoja na Bi. Hawa Maftah na Bi. Halima bint Salum kwa kuwataja wachache waliojenga msingi wa akina mama kuipa TANU nguvu za kutisha katika mikutano yake Viwanja Vya Mnazi Mmoja na katika sanduku la kura.

Hii ndiyo iliyokuwa Kariakoo ambayo ile ofisi ya Abdul Sykes pale Kariakoo ilimpa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa.

Itapendeza sana kama CCM itaweka ukumbusho pale sokoni kama kumbukumbu ya wazalendo hawa wake kwa waume.

Vinginevyo tutabaki kuwa taifa lisilo na historia inayoeleweka ya ukombozi wake.

Picha ya Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 Ofisi ya Market Master ni hilo jengo dogo mkono wa kulia.

Picha ya chini kabisa Mshume Kiyate na Julius Nyerere, 1964.

View attachment 1804842

View attachment 1804844

View attachment 1804850
Wapigania uhuru wote huwa hawatajwi na huwa hawana umaarufu Sawa,ni kitu Cha kawaida,
Kuna vijana hata hawamjuhi Steve Biko,kwa kule SA,anayejurikana sana ni Nelson Mandela,lakini wapo waanzilishi wa ANC kabla ya Mandela hajajiunga,na wengi mchango wao huwa hautajwi sana,popote palipokuwa na mapambano ya kudai uhuru,
Tatizo we jamaa,muelekeo wako ni kuwa "waislam"ndio waliopigania uhuru wakati "wakristo"wakila bata na mkoloni,
So biased
 
Mimi ninachojua uislam wakati unaletwa na mwarabu uliwakuta wazee wetu.

Sasa ni kwanini hao wazee wako unawatambua zaidi kama wazee wa kiislam badala ya wazee wa Mzizima ?
 
Mafiningo,
Udini ikiwa unakusudia Uislam ni shida sana kuuepuka katika historia ya TANU uhuru wa Tanganyika.

Kwa nini?

Wazee wetu waliunda African Association (AA) 1929 ili kujitoa katika mikono ya Father Gibbons wa Minaki Mission ambaye yeye ndiye alikuwa mwakilishi wa Waafrika.

Ndipo wakaunda AA na majority wa hawa waasisi walikuwa Waislam akina Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Kisha hawa wazee wetu wakaunda Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933 pembeni ya AA ili wasipitishe mambo ya Uislam AA lakini viongozi wakiwa ni wale wale waliokuwa wanaongoza AA.

Hawa waasisi wa AA ndiyo waliokuja kuunda TANU na ndiyo wanachama wa mwanzo na viongozi wa mwanzo pia wakiwa watu waliokuwa karibu sana na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hauko peke yako unaetaabishwa na historia hii.

Wengi wangependa kama historia hii ikabadilishwa na tuondoe mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Haiwezekani kuifuta historia.

Huwezi kusomesha historia ya uhuru wa Kenya bila kuwataja Wakikuyu na Mau Mau ukisema kufanya hivyo ni ukabila.

Chuo Cha CCM Kivukoni walijaribu na wakachapa kitabu amacho haya yote unayosoma kutoka kwangu hayapo.

Balaa lake ndilo hili leo wewe unasoma historia ya kweli unateseka.

View attachment 1805557

View attachment 1805558

Vipi mimi leo nisijifaharishe na historia ya wazee wangu hawa anbao wengine niliwaona kwa jicho langu udogoni?
Sitaabishwi na historia bali ni namna unavyoingiza maneno yenye malengo kuwa waislam walionewa.
Naona ni kama kuna kitu ungependa waislam wakidai. Ndipo ninapopata shaka na story nzima na kuhisi umeipindisha.
 
Wapigania uhuru wote huwa hawatajwi na huwa hawana umaarufu Sawa,ni kitu Cha kawaida,
Kuna vijana hata hawamjuhi Steve Biko,kwa kule SA,anayejurikana sana ni Nelson Mandela,lakini wapo waanzilishi wa ANC kabla ya Mandela hajajiunga,na wengi mchango wao huwa hautajwi sana,popote palipokuwa na mapambano ya kudai uhuru,
Tatizo we jamaa,muelekeo wako ni kuwa "waislam"ndio waliopigania uhuru wakati "wakristo"wakila bata na mkoloni,
So biased
Juan...
Hii Steve Biko hajulikani umeitoa wapi?

Naijua vyema historia ya Afrika Kusini nimeisoma kidato cha kwanza 1967 tena nimesomeshwa na mwalimu Muingereza Mrs. Grant St. Joseph's Convent School.

Kitabu kilichoniathiri sana katika historia hii ni "Cry the Beloved Country," cha Alan Paton.

Nimefika Afrika Kusini mara mbili na nimetembelea Apartheid Museum na nimefika Soweto na nyumba ya Mandela ambayo sasa ni kumbukumbu yake.

Nimekisoma kitabu cha Mandela, "Long Walk to Freedom."

Nimeitembelea pia selo yake Roben Island.

Steve Biko ni mmoja wa mashujaa wa Afrika Kusini na hakuna asiyemjua.

Steve Biko ametengenezewa senema ya maisha yake.

Historia za mashujaa wao wote zipo hapo Apartheid Museum mpaka magari ya deraya yaliyokuwa yanatumika dhidi ya wananchi.

Afrika Kusini wamehifadhi historia yao.

Kabla ya kuandika ni vizuri kufanya utafiti.

Sanamu ya Mandela na selo yake Roben Island.

Screenshot_20210602-141424_Photos.jpg

Screenshot_20210602-142547_Photos.jpg
 
Sitaabishwi na historia bali ni namna unavyoingiza maneno yenye malengo kuwa waislam walionewa.
Naona ni kama kuna kitu ungependa waislam wakidai. Ndipo ninapopata shaka na story nzima na kuhisi umeipindisha.
Mafiningo,
Ni historia ndefu na inataka ujuzi si kitu kinachowezwa kujadiliwa na yeyote yule.

Kukusaidia kuelewa inabidi wewe mwenyewe kuisoma historia ya Tanganyika hadi kufikia uhuru mwaka wa 1961 na baada ya hapo.

Ukiwa ushasoma na kuelewa historia yote utakuwa katika hali ya kujua.

Anza hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com

Fanya search kwa matukio na majina.
 
Mimi ninachojua uislam wakati unaletwa na mwarabu uliwakuta wazee wetu.

Sasa ni kwanini hao wazee wako unawatambua zaidi kama wazee wa kiislam badala ya wazee wa Mzizima ?
Mkaruka,
Soma kwanza mjadala uelewe.
Utakuwa katika hali nzuri ya kujadili.
 
Lihakanga,
Historia ya Kariakoo nimeieleza katika kitabu cha Abdul Sykes kuanzia mpangilio wa biashara ndani ya soko; wapi paliuzwa tumbuku, wapi matunda, wapi samaki nk.

Nimeeleza hata makabila na biashara walizokuwa wanafanya.
Wanyamwezi waliuza viazi vitamu, Waluguru machungwa, Wamashomvi samaki nk.

Nikaeleza wafanyakazi wake, Shariff Attas alikuwa ''collector,'' wa ushuru wa nafaka, Mshume Kiyate dalali wa samaki wabichi, ng'onda na papa nk, kutoka mbali hadi Mafia.

Abdul Sykes akiuza kadi za TANU Kariakoo hadi siku akavamiwa na Town Clerk Mzungu ofisini na ukazuka ugomvi mkubwa baina yao.

Kwa kuhofu Abdul Sykes atafukuzwa kazi wazee wa sokoni wakamsomea dua na wakachinja mnyama.

Dua ambayo Nyerere alisomewa nyumbani kwa Jumbe Tambaza na Rashid Ali Meli pia akasomewa na hawa wote kwa ajili ya kuwakinga na shari za Waingereza.

Nakushukuru hata hivyo kwa ushauri wako.
ni wapi naweza kusomewa dua hiyo leo hii....? nasikitika sana moja ya vitu tulivyo poteza ni asili yetu na hadi kufika mwaka 2045 apatokuwa na asili yoyote itakayokuwa inaeexit
 
ni wapi naweza kusomewa dua hiyo leo hii....? nasikitika sana moja ya vitu tulivyo poteza ni asili yetu na hadi kufika mwaka 2045 apatokuwa na asili yoyote itakayokuwa inaeexit
Prince...
Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilipofika kwenye TANU imeshaundwa hii ni 1955 moto wa kudai uhuru unazidi kuongeza joto lake.

Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika anauza kadi za TANU misikitini anakodarsisha.

Abdul Sykes anauza kadi za TANU sokoni Kariakoo.

Iko siku Town Clerk Mzungu akamvamia ofisini.

Ugomvi mkubwa ukatokea baina ya huyu Mwingereza na Abdul.

Ikawa wazi Abdul atafukuzwa kazi.

Mpashaji wangu alinieleza kwa yakini nini kilimfika yule Mzungu.

Mimi nilibakia kimya.

Abdul alibakia kazini na TANU ilizidi kupata nguvu.

Dua ya Rashid Ali Meli yeye alifungua sefu ya Dar-es-Salaam Municipal Council alikoajiriwa kama Bwana Fedha akatoa hela akampa Iddi Faiz Mafungo mratibu wa safari ajaze mfuko wa safari ya Nyerere ya kwanza UNO 1955 kisha hela zirudishwe haraka.

Siku ya pili wakaguzi wakaingia ofisini kwake.

Wanejuaje kuwa hela zimetoka?
Kisa kirefu.

Special Branch walikuwa na pandikizi lao ndani ya TANU.

Rashid Ali Meli akawaeleza viongozi wa juu wa TANU yaliyotokea ofisini kwake.

Bahati nzuri wakaguzi hawakugusa sefu siku ile.

Usiku ule ikapigwa dhikr nzito usiku kucha wanaomba Allah amnusuru ndugu yao Rashid Ali Meli.

Siku walipofungua sefu hela zote wamezikuta kamili.

Nimeinamisha kichwa nataka mpashaji wangu anieleze vipi fedha zilirudi kwenye sefu?

Hii ndiyo TANU iliyokuwa ikifungua mikutano yake kwa kusoma dua.

Yako mengi.

Mengine sikuweza kuyaandika kwani nilitaka ithibati ya taarifa.
 
Father...
Sikudandia.

Pale aliposimama Mama Samia kwangu kunanikumbusha mengi katika historia ya Kariakoo.
Kwanza na hili sikueleza.

Hapo nyuma ya Ofisi ya Market Master, babu yangu Shariff Muhammad alikuwa na matundu ya njiwa hiyo ndiyo ilikuwa biashara yake.

Hivi ninavyoandika ni kama vile namuona kasimama mbele ya matundu yake na chini pametapakaa mtama aliokuwa akiwalisha njiwa wake.

Mimi sijapatapo kusema kuwa wazee wangu ndiyo walostahili kuongoza Tanganyika.

Labda nikueleza kidogo historia ya hawa wazee.

Mkutano wa kumwingiza Nyerere katika uongozi wa TAA ulifanyika Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes alisafiri na Ali Mwinyi Tambwe, Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya kwenda Nansio kupata kauli ya Mwapachu kuhusu Nyerere.

Ushauri wa Mwapachu ulikuwa Abdul ampishe Nyerere na amsaidie kushinda uchaguzi wa TAA 1953 na mwaka unaofuata, 1954 TANU iundwe.

Na Hamza Mwapachu alitoa sababu zake.

Kisa kirefu.

Mimi nayajua haya yote.

Sasa ikiwa huu ndiyo ukweli wa historia ya uhuru vipi mimi nitatamani kuwa historia iwe vinginevyo?

Mimi nimefaidika sana kwa kuandika historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kubwa ni kuondoa dukuduku lililosonga moyo wangu kwa kuona kuwa wazee wangu waliofutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimeweza kuwaandikia kitabu kizima na kikapata umaarufu katika vyuo vikuu duniani vinavyosomesha African History.

Sijachoka na wanafunzi wangu hawajachoka kama wewe ulivyokuwa hujachoka unashindwa kustahamili unaniandikia na mimi kama nifanyavyo kwa wenzako sijachoka kuisomesha historia hii.

Kama nafsi yako inaumizwa na ukweli wa historia hii ni bahati mbaya sana kwako.

Sikudandia.

Mama Samia kanikumbusha mengi kwa kusimama pale aliposimama katika soko la Kariakoo.

Pale mbele yakeilikuwa Ofisi ya Market Master, Brian Hodges Mwingereza na alipoacha kazi ndiyo akaingia Abdulwahid Sykes na akabadili historia nzima ya soko lile kuwa moja ya ngome dhidi ya ukoloni.

Father...
Nahitimisha.

Sikujua kuwa kuwafuta Waislam katika historia ya uhuru wa Tanganyika ni kuondoa sumu.

Umenisaidia pakubwa.
Japo hukunielewa, sina ugomvi nawe kukumbuka zama zako hasa marhum mzee wako. Wote tunawapenda sana waliotutengeneza kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Pia hakuna sehemu yoyote nimegusia kuwafuta hao waislam wako. Kwani Kawawa, Karume, Kaluta, Bi Titi na wengine walikuwa matwahuti? Huwa mie si mtu wa udini hata kidogo. Wote mu watoto wangu.
 
Father,
Labda kama ikiwa ndiyo leo unanisoma mie kama wewe si mtu wa kuparurana.

Mimi sina Waislam wangu hao ni waja wa Allah aliyewaumba na kuwajaalia kuwa Uislam ndiyo dini yao.

Wala mie si mtu wa udini kama ulivyo wewe kwani ukiwa hivyo utawadhulumu wale ambao si wa dini yako na Allah kawaasa Waislam wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa.

Ndiyo maana kwa kufuata mafunzo hayo wazee wangu walimpokea Julius Nyerere Mkatoliki wakampa uongozi na wakamhami kwa kila hali.

Ikutoshe tu kuwa Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliomfikisha kumjulisha kwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Ilikuwa Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo walikwenda Zanzibar na Nyerere kumtambulisha kwa Karume.

Ikutoshe pia ilikuwa Iddi Faiz Mafungo na Iddi Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere kumtambulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo.

Hapa ndipo niliposimama mie na kuandika kitabu kusahihisha historia ambayo haikuwa historia ya TANU.

Sihitaji kueleza upya kwa nini nimeikataa historia ya TANU ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Naikataa vilevile historia ya TANU kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Julius Nyerere.

Mimi sikudandia historia hii.

Hii historia mimi inanihusu kwa nasaba na ndiyo ikawa najua hadi vitu vidogo vidogo ambavyo wengi wanavisikia kwangu kwa mara ya kwanza.

Leo ile historia iliyofutwa sasa imehifadhiwa na atakae anaisoma.

Sasa kwangu mimi chochote utakachoandika liwe jina au jambo basi nitakuwa na historia yake.

Iwe umemtaja Bi. Titi au Karume au Nyerere mwenyewe.

Mimi nina miaka 69 sasa na ili mimi niwe umri wa kuwa mwanao wewe utakuwa mtu mzima sana.
 
Mbona kwenye uzi wako hujamtaja John Rupia ?
Uzalendo...
Umoja ulidumu kwa kipindi kile cha kudai uhuru.

Baada ya uhuru misuguano ndani ya TANU ikaanza.

Mwaka wa 1963 ndani Kamati Kuu ya TANU ulizuka mzozo baina ya Rajab Diwani, Selemani Kitundu, Julius Nyerere na Bi. Titi Mohamed.

Bi. Titi na Nyerere kauli zikapishana.

Mwaka huo huo Bukoba katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wagombea wa TANU Waislam walipingwa kwa sababu kuwa hawana elimu na Kanisa likaweka wagombea wake wenye elimu.

Mjini Tabora Regional Commissioner Richard Wambura akapambana na Bilal Rehani Waikela kwenye mkutano wa hadhara.

Mwaka huo huo 1963 Baraza la Wazee wa TANU likavunjwa kwa kuchanganya dini na siasa.

Kufikia mwaka wa 1964 hali ilikuwa si shwari.

Uhuru ukawa umekuja na changamoto kubwa.

Bi. Titi Mohamed na Tewa Said Tewa wakawekewa mkakati wasishinde ubunge uchaguzi wa mwaka 1965 na kweli wakashindwa.

Yako mengi.

Kilele mwaka wa 1993 kwa mara ya kwanza Waislam wakapambana na askari waliokuja kutawanya maandamano ya kukamatwa masheikh kuhusu mabucha y nguruwe.

Yaliyofuatia baada ya hapo sote tunayajua.
 
Kweli maana hajamtaja John Rupia !
History nzuri japo imeingia walakini kwa kuingiza udini. Ukiingiza udini sisi ambao hatufahamu tunahisi kuna mahala unapindisha ili uweze kutetea dini yako. Hivyo story inakosa kuaminika kutokana na malengo ya mtoa mada.
Niliichukua vizuri lakini nimeifuta kwa kiasi kikubwa kwani nahisi kuna uongo umedumbukizwa.
Nimechukua Jiografia basi,, imenitosha.
 
huyu mzee anamaumivu ya ndani nafsi yake haijakubali kwanini waswahili (waislamu) hawakutambuliwa kama wapigania uhuru kitu ambacho sio kweli sana sema yeye hiyo line hakuwemo au waliona anadadisi sana wakamtema.
haya yalishapita ukombozi wa tanganyika haukuhusisha Dar es salaam tu bali nchi nzima ya Tanganyika sasa si kweli watu watafanana.
mwisho bado siku chache kwa kizazi kijacho hakitahitaji kujua yote haya bali yale yatakayosaidia wao kuondokana na umaskini na pia kuwa na nguvu ya kutawala Dunia
 
Mama Samia leo asubuhi aliamkia Soko la Karikaoo kuangalia biashara inavyokwenda na kuzumgumza na viongozi wa soko.

Allah ana rehma zake na hutukumbusha mengi kwa njia ambazo mtu huwezi kutegemea.

Hapo aliposimama kwenye gari Rais Mama yetu Samia Soko la Kariakoo alikoelekeza sura yake ni Mtaa wa Swahili na kona ya Tandamti na ameupa mgongo Mtaa wa Swahhili na Mkunguni.

Hapo mbele yake ndipo ilipokuwa Ofisi ya Market Master Abdulwahid Sykes miaka ya 1950 Tanganyika inaanza harakati za kupigania uhuru wake kutoka kwa Waingereza.

Soko la Kariakoo na ofisi hiyo palikuwa moja ya ngome za harakati dhidi ya ukoloni.
Bahati mbaya historia hii haifahamiki ila kwa wachache sana.

Sehemu nyingine ambako vijana wanaharakati walikuwa wakipita kwa hili au lile katika siasa za ukombozi ilikuwa Ilala Welfare Centre ofisi ya Hamza Mwapachu.

Vilevile wanaharati walikuwa wakikutana nyumbani kwa Dossa Aziz Mtaa wa Congo na Mbaruku na nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na nyakati za jioni wakikutana Tanga Club Mtaa wa New Street na Mkunguni.

Ilikuwa hapo sokoni Kariakoo ndipo Julius Nyerere akija kumuona Abdul Sykes ofisini kwake kuanzia mwaka wa 1952 na ndipo alipojuana na wazee mashuhuri wa mji maarufu kupita wote ni Mshume Kiyate.

Mzee Mshume akaunga uhusiano na Nyerere uliopitiliza siasa za TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika akamfanya Nyerere mfano wa mwanae.

Kueleza mchango wa Mzee Mshume katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kutarefusha hii makala.

Hapo sokoni ndipo Mwalimu Nyerere alipofahamiana na Shariff Abdallah Attas kwa karibu sana kiasi safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 mkewe Shariff Attas, Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mmoja wa akina mama waliomsindikiza uwanja wa ndege pamoja na Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee.

Hawa ndiyo walikuwa wanawake pamoja na Bi. Hawa Maftah na Bi. Halima bint Salum kwa kuwataja wachache waliojenga msingi wa akina mama kuipa TANU nguvu za kutisha katika mikutano yake Viwanja Vya Mnazi Mmoja na katika sanduku la kura.

Hii ndiyo iliyokuwa Kariakoo ambayo ile ofisi ya Abdul Sykes pale Kariakoo ilimpa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa.

Itapendeza sana kama CCM itaweka ukumbusho pale sokoni kama kumbukumbu ya wazalendo hawa wake kwa waume.

Vinginevyo tutabaki kuwa taifa lisilo na historia inayoeleweka ya ukombozi wake.

Picha ya Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 Ofisi ya Market Master ni hilo jengo dogo mkono wa kulia.

Picha ya chini kabisa Mshume Kiyate na Julius Nyerere, 1964.

View attachment 1804842

View attachment 1804844

View attachment 1804850
wewe nimtu mwema, umeeaelezea MATAGA vizuri maana wao wanalaumu na kuasifia tu
 
wewe nimtu mwema, umeeaelezea MATAGA vizuri maana wao wanalaumu na kuasifia tu
Jaji...
Hili neno MATAGA hulisoma kwingi lakini sijui maana yake na kwa kuwa sikuwa nona linanihusu sikutaabika kuuliza.

Nifahamishe maana ya neno hili tafadhali.
 
Jaji...
Hili neno MATAGA hulisoma kwingi lakini sijui maana yake na kwa kuwa sikuwa nona linanihusu sikutaabika kuuliza.

Nifahamishe maana ya neno hili tafadhali.

..mataga maana yake ni " make tanzania great again. "

..hili ni kundi mahususi la kumtukuza Magufuli na kumtetea kwa kila jambo.

..lengo lingine la mataga ni kutukana na kumdhalilisha yeyote asiyekubalina na Magufuli.

..kwa sasa hivi kundi la mataga limehamisha nguvu zake ktk kumkosoa, kumtukana, na kumdhalilisha, Rais Samia kwasababu wanaamini mafanikio yake yatamfunika mwendazake na kumfanya asahauliwe na Watanzania.
 
huyu mzee anamaumivu ya ndani nafsi yake haijakubali kwanini waswahili (waislamu) hawakutambuliwa kama wapigania uhuru kitu ambacho sio kweli sana sema yeye hiyo line hakuwemo au waliona anadadisi sana wakamtema.
haya yalishapita ukombozi wa tanganyika haukuhusisha Dar es salaam tu bali nchi nzima ya Tanganyika sasa si kweli watu watafanana.
mwisho bado siku chache kwa kizazi kijacho hakitahitaji kujua yote haya bali yale yatakayosaidia wao kuondokana na umaskini na pia kuwa na nguvu ya kutawala Dunia
Chiwa,
Kwa kawaida inapoandikwa. ''Huyu Mzee,'' basi jua maneno yatakuwa kidogo makali.
Mwandishi anakuwa kaghadhibika kwani kama mtu anataka kuonyesha staha na heshima kwa mtu aliyemzidi umri hawezi kumwita, ''Huyu.''

Ataandika, ''Mzee Mohamed...''
Huyu ni karibu ya tusi.

Mimi sikuwemo katika kundi la kupigania uhuru ila babu yangu Salum Abdallah alikuwamo toka 1920s wanaanza African Association.

Baba yangu kaiona TANU inaasisiwa Dar es Salaam mwaka wa 1954 mimi ni mtoto wa miaka 2.

Kwa hiyo hayo yote uliyosema kuwa mimi nina uchungu sikupata cheo baada ya uhuru ni maneno hayana maana yeyote.

Hiyo picha hapo chini ni mimi wakati TANU inaasisiwa.

Aliyenipiga picha hii ni Mzee Shebe yeye alikuja kuwa mpiga picha wa TANU na kaacha hazina kubwa za kumbukumbu ya miaka ya mwanzo ya TANU.

Ninazo picha zake alizopiga miaka hiyo hadi uhuru na mbele yake katika Maktaba yangu.

1622738436992.png
 
huyu mzee anamaumivu ya ndani nafsi yake haijakubali kwanini waswahili (waislamu) hawakutambuliwa kama wapigania uhuru kitu ambacho sio kweli sana sema yeye hiyo line hakuwemo au waliona anadadisi sana wakamtema.
haya yalishapita ukombozi wa tanganyika haukuhusisha Dar es salaam tu bali nchi nzima ya Tanganyika sasa si kweli watu watafanana.
mwisho bado siku chache kwa kizazi kijacho hakitahitaji kujua yote haya bali yale yatakayosaidia wao kuondokana na umaskini na pia kuwa na nguvu ya kutawala Dunia
Huyu mzee anajifanya anamjua Mwl Nyerere kuliko mama Maria Nyerere!!

Bahati nzuri ajenda zake watu wengi sasa wameishaanza kumstukia!
 
Back
Top Bottom