Laiti Rais samia angeijua historia ya soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Laiti Rais samia angeijua historia ya soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Eyume,
Waliotangulia kufika Pwani ya Afrika ya Mashariki walikuwa Wamishionari na azma yao ilikuwa kulistaarabisha ''The Dark Continent.''

Lakini Krapf alipofika Vuga kwa Chief Kimweri alistaajabu kumkuta Kimweri na wanawe wote wanajua kujua kusoma, kuandika na Hesabu na wakiandika kwa herufi za Kiarabu.

Kwa ufupi hakukuta watu ambao hawakuwa ''washenzi,'' kawakuta watu wenye ustaarabu na wana dini wakimwamini Mungu Mmoja, yaani Uislam.

Ugunduzi huu ulijaza choyo ndani ya hawa Wamishionari na walipokuja kufuatiwa na wakoloni ikawa sasa Wamishionari na Wakoloni ni wamoja katika kuupiga vita Uislam.

Ili waweze kufanikiwa katika njama zao kitu cha kwanza walichofanya ilikuwa ni kupiga marufuku hati za Kiarabu na badala yake wakaweka hati za Kirumi.

Wakawa wanatoa elimu kwa ubaguzi.
Ili mtoto aaandikishwe shule ilikuwa sharti kwanza abatizwe.

Kwa mukhtasari ubaguzi huu ndiyo uliowafanya Waislam wajiunge pamoja kupambana na ukoloni wakijua wakoloni wakianguka Wamishionari watakuwa hawana pa kushika na haki na usawa kwa wote utapatikana.

Hii ndiyo sababu harakati za uhuru zikaongozwa na Waislamu.
Lakini uhuru ukaja na changamoto zake.

Waafrika waliosomeshwa na Kanisa wakawa na hofu na nguvu za Waislam katika siasa na juhudi zao za kujenga taasisi za elimu kujiendeleza.

Ikawa kinachotakiwa ni kuwa hali ile ile iliyokuwako wakati wa ukoloni ya Waislam kubaguliwa katika elimu iendelee.
Huu ndiyo msuguano ambao bado haujatafutiwa dawa hadi sasa zaidi ya miaka 50 nchi ikiwa huru.
🙆🏻‍♀️ Ina maana hadi sasa tz kuna ubaguzi wa dini..... Nilidhani ulikwisha?

Na je awali kabla ya dini wazee wetu waliishi vipi je ni kweli hawakumjua Mungu wa kweli?
 
Ni mpika propoganda mahiri sana wa dini yake.
History nzuri japo imeingia walakini kwa kuingiza udini. Ukiingiza udini sisi ambao hatufahamu tunahisi kuna mahala unapindisha ili uweze kutetea dini yako. Hivyo story inakosa kuaminika kutokana na malengo ya mtoa mada.
Niliichukua vizuri lakini nimeifuta kwa kiasi kikubwa kwani nahisi kuna uongo umedumbukizwa.
Nimechukua Jiografia basi,, imenitosha.
 
Back
Top Bottom