Laiti Rais samia angeijua historia ya soko la Kariakoo katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Kwanini walifutwa mkuu?
 
Anasema alimuelezea Mzee Aikael Mbowe kwenye kitabu chake ila huku jamvini mada zake zote hawataji sasa kina mbowe, sio wote wamekisoma kitabu chake.
Ndugu zangu,
Nimewasoma wachangiaji watatu waliopita.

Bahati mbaya sana ni kuwa wameghadhibishwa na historia hii ambayo kwao ni mpya hawakupata kuisikia kabla.

Ibra moja katika historia hii ni kuwa wengi wakisoma na ni chembe tu kutoka kitabu kizima huwa wanapandisha hamaki na huishia kutoa kejeli na zinafuatiwa na lugha nje ya uungwana.

Wengi huishia kunishambulia mimi binafsi.

Katika hali kama hii mimi huona bora nikasimama kuisomesha hii historia hadi wenzangu hasira zao zitakapopungua.

Hii ni tofauti na wenzetu nje ya mipaka yetu Ulaya na Marekani wao maswali huwa mengi sana kwangu wakitaka kujua kwa nini imekuwa hivi au vile nk.

Naomba niwape mfano mmoja uliotokea University of Iowa, Iowa City.

Nilifanya mhadhara hapo kuhusu historia ya Tanganyika na mjadala ulikuwa mkali sana.

Idara ya African History ilikuwa imenialika na mhadhara wangu ulihudhuriwa na wataalamu wa African History kutoka baadhi ya vyuo hapo Marekani.

Nilijitahidi kujibu kila swali walilonitupia.

Mwisho wa mhadhara sikutoka pale kichwa chini bali kichwa changu kilikuwa juu.

Hapo hapo Jonathan Glassman profesa wa African History akanipa mwaliko bila hata ya kunipa barua akaniomba nikazungumze chuoni kwake Northwestern University, Evanston, Chicago.

Hiki chuo kinaongoza ulimwenguni katika African History.

Nilikubali mwaliko ule na nilikwenda kuzungumza.

Hakuna hapo kughadhibika wala kejeli.

Wao ni swali juu ya swali.

Hawatukani wala hawamshambulii mtoa mada.

Hii ndiyo tofauti kubwa baina yao na nyie hapa.



Prof. Michael Lofchie, University of Iowa, Iowa City.
 
Huyu mzee anajifanya anamjua Mwl Nyerere kuliko mama Maria Nyerere!!

Bahati nzuri ajenda zake watu wengi sasa wameishaanza kumstukia!

Huyu mzee anajifanya anamjua Mwl Nyerere kuliko mama Maria Nyerere!!

Bahati nzuri ajenda zake watu wengi sasa wameishaanza kumstukia!
Mzizi,
Sina sababu ya kujifanya namjua Julius Nyerere.

Ila nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Ndani ya historia hii nimemtaja Nyerere kwa mapana na marefu yake.

Nyerere alipokelewa na wazee wangu 1952 na waliishi pamoja na yeye hadi uhuru ulipopatikana 1961.

Kupitia hawa ndiyo nimeweza kumweleza Mwalimu vyema hadi sigara aliyokuwa akivuta.

Jopo la Prof. Issa Shivji lililoandika kitabu cha maisha ya Nyerere walinihoji kama mmoja wa watu wanaomjua Mwalimu.

Na waliniambia kuwa katika watu waliowahoji mimi nina mengi kuhusu Nyerere.

Kitabu kilipozinduliwa nilitunukiwa nakala kwa mchango wangu katika utafiti.

Soma hapo chini kile walichosema kuhusu mimi:




 
taandika, ''Mzee Mohamed...''
Huyu ni karibu ya tusi.
kwa hili pole sisi wengine kiswahili kinaweza kuwa kinatupiga chenga binafsi sikuona tusi hata kidogo pole sana nimejifunza kitu.
lakini kwa umri wako ushakuwa babu hivyo wajukuu wakikwita huyu usiumie sana japo mimi sio mmoja wapo.
 
kwa hili pole sisi wengine kiswahili kinaweza kuwa kinatupiga chenga binafsi sikuona tusi hata kidogo pole sana nimejifunza kitu.
lakini kwa umri wako ushakuwa babu hivyo wajukuu wakikwita huyu usiumie sana japo mimi sio mmoja wapo.
Chiwa,
Hakika ni babu sasa namshukuru Allah kanijaalia wajukuu lakini bado wadogo sana umri wa chekechea.

Walioko hapa jamvini ni umri wa wanangu kwa hiyo hawa mimi ni baba yao si babu yao.

Kwa ajili hii basi hawawezi kunifanya mtani wao.

Hizi ndizo mila zetu.
 
teh..te...teh.. tukishindwa kabisa tutakutafutia timu ili mradi tutafute ni kwa jinsi gani tunaweza kutafuta furaha.
natumaini ulinielewa ndugu na tuko sawa sasa.
 
teh..te...teh.. tukishindwa kabisa tutakutafutia timu ili mradi tutafute ni kwa jinsi gani tunaweza kutafuta furaha.
natumaini ulinielewa ndugu na tuko sawa sasa.
China,
Tuko pamoja.
 
Kwa kuhofu Abdul Sykes atafukuzwa kazi wazee wa sokoni wakamsomea dua na wakachinja mnyama.



Dua ambayo Nyerere alisomewa nyumbani kwa Jumbe Tambaza na Rashid Ali Meli pia akasomewa na hawa wote kwa ajili ya kuwakinga na shari za Waingereza.

Mzee Mohammed

Nini kingetokea bila ya hao 2 kusomewa dua?!
 
Uzalendo...
Dua inafuta qadar yaani inafuta lile baya ambalo lilikuwa likufike.

Allah akiombwa anakunusuru.
 
Kwanini Msiombe Dua Dhidi Ya Mayahudi "Waliokalia" Ardhi Ya Wapalestina Huku " Wakiwanyanyasa"?
Uzalendo...
Hii si maudhui tunayojadili hapa.

Ikiwa unataka mjadala huo ninacho cha kuzungumza.

Nimepata kualikwa State University of Zanzibar (SUZA) na Centre for Foreign Relations, Kurasini Dar es Salaam na nimetoa mada.

Fungua uzi mpya.
 
Asante sana nimejifunza vitu nahisi hapo mimi ni kajukuu kako
 
Uzalendo...
Hii si maudhui tunayojadili hapa.

Ikiwa unataka mjadala huo ninacho cha kuzungumza.

Nimepata kualikwa State University of Zanzibar (SUZA) na Centre for Foreign Relations, Kurasini Dar es Salaam na nimetoa mada.

Fungua uzi mpya.

Kwa hiyo zamani baada ya uhuru ama hata kabla walikua na ubaguzi wa dini?
 
Kwa hiyo zamani baada ya uhuru ama hata kabla walikua na ubaguzi wa dini?
Eyume,
Waliotangulia kufika Pwani ya Afrika ya Mashariki walikuwa Wamishionari na azma yao ilikuwa kulistaarabisha ''The Dark Continent.''

Lakini Krapf alipofika Vuga kwa Chief Kimweri alistaajabu kumkuta Kimweri na wanawe wote wanajua kujua kusoma, kuandika na Hesabu na wakiandika kwa herufi za Kiarabu.

Kwa ufupi hakukuta watu ambao hawakuwa ''washenzi,'' kawakuta watu wenye ustaarabu na wana dini wakimwamini Mungu Mmoja, yaani Uislam.

Ugunduzi huu ulijaza choyo ndani ya hawa Wamishionari na walipokuja kufuatiwa na wakoloni ikawa sasa Wamishionari na Wakoloni ni wamoja katika kuupiga vita Uislam.

Ili waweze kufanikiwa katika njama zao kitu cha kwanza walichofanya ilikuwa ni kupiga marufuku hati za Kiarabu na badala yake wakaweka hati za Kirumi.

Wakawa wanatoa elimu kwa ubaguzi.
Ili mtoto aaandikishwe shule ilikuwa sharti kwanza abatizwe.

Kwa mukhtasari ubaguzi huu ndiyo uliowafanya Waislam wajiunge pamoja kupambana na ukoloni wakijua wakoloni wakianguka Wamishionari watakuwa hawana pa kushika na haki na usawa kwa wote utapatikana.

Hii ndiyo sababu harakati za uhuru zikaongozwa na Waislamu.
Lakini uhuru ukaja na changamoto zake.

Waafrika waliosomeshwa na Kanisa wakawa na hofu na nguvu za Waislam katika siasa na juhudi zao za kujenga taasisi za elimu kujiendeleza.

Ikawa kinachotakiwa ni kuwa hali ile ile iliyokuwako wakati wa ukoloni ya Waislam kubaguliwa katika elimu iendelee.
Huu ndiyo msuguano ambao bado haujatafutiwa dawa hadi sasa zaidi ya miaka 50 nchi ikiwa huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…