TANZIA Lala salama Padre Felician V. M. Nkwera

Kwa marehemu mama mwanza ndio EMAUS? Umemuelekeza vizuri, kama hajaelewa mwambie aende nyuma ya iliyokuwa stendi ya mabasi ubungo.
 
Daah! Hii kitu uliyoandika bila shaka umeitoa kichwani kwako.
 
Ni wapi unahisi nimetoa kichwani.
Kanisa Katoriki limezuià hizo huduma Kwa sababu kutakua na Vurugu kanisani wakiruhusu, utakuta Padre ana Karama ya Uponyaji na Askofu wake Hana, itapelekea Padre kuwa na Nguvu Kanisani kuliko Askofu, na baadaye Kanisa litakua na Migogoro.
 
Kanisa Katoriki limezuià hizo huduma Kwa sababu kutakua na Vurugu kanisani wakiruhusu, utakuta Padre ana Karama ya Uponyaji na Askofu wake Hana, itapelekea Padre kuwa na Nguvu Kanisani kuliko Askofu, na baadaye Kanisa litakua na Migogoro.
Huo ndo Ukweli....!
Nakumbuka kipindi hicho namsaidia huduma Padre mwenye Karama ya Uponyaji ambaye pia alikua na Karama ya Unabii, alinambia Usimwambie mtu, Mimi nikaona yule Padre anafanya jambo jema Kwa Nini anasema nisimwambie mtu...!? Kwa Nini iwe Siri....!?

Akanambia Kanisa Katoriki haliruhusu huduma za maombezi, lakini Linao Mapadre wenye Karama za Uponyaji.....! Ni kufifisha kazi za Roho Mtakatifu Kwa Watu wake.

Haya Mimi nimekupa sababu Kwa Nini huduma za Maombezi zimezuiwa Kanisani.....!
Na unahisi siko sahihi, Sasa wewe tuambie Kwa huduma za maombezi zimezuiwa ndani ya Kanisa Katoriki ...!?
 
Alitengwa kwa sababu ya kufanya huduma ya maombezi??
Umeandika kwanba alikuwa na kesi nyingi, unaweza fafanua kiasi kesi zilihusu nini (nimeshangaa padri kuwa na kesi mahakamani, anashtaki ama anashtakiwa ~ kwa nini)
sio mahakamani
 
Makanisa yote ya Roman Catholic DSM yaliweka vibao vya kuzuiya wanamaombi wasiingie kanisani sababu ya father Nkwera. Ni padre aliyesaidia kuanza kwa karismatiki katoliki kama utume kutokana na kanisa kutaka kupunguza pressure ya wanamaombi. Pumzika kwa amani baba
 
Nimesoma mahali kanisa (RC) limesimamia mazishi yake ilhali lilimtenga enzi za uhai wake!

Ina maana alikuwa bado anasali RC?
 
 
Sababu uliyotoa ni ya kijinga! Hii inadhihirisha kwamba viongozi katika Roman ni watu wenye wivu!! Jambo ambalo halipaswi kuwa kwa viongozi wa kidini kama wao! Inadhihirisha kuwa pengine hata hawakuwekwa na Mungu mahali hapo!!! Kwanini wakatae kazi ya Mungu kufanyika Kanisani?
 
Kwenye Ukatoriki, Yeyote anayetamani kuwa Padre anaweza kuwa Padre, wapo Mapadre ambao Wazazi wao waliwalazimisha kwenda Seminari, Kuna wengine wamekua Mapadre Kwa sababu aliona Baba mdogo, Mjomba, n.k Kawa Padre...!

Na katika Mapadre wapo ambao wameitwa kabisa kumtumikia Mungu, na ndiyo hao wanakua na Karama za Uponyaji n.k.....!

Ila ukija Kwa Watumishi wa Mungu Kama kina Mwalimu Mwakasege, kwao Uchungaji haukua chaguo, ila waliitwa wakiwa kwenye Shughuri za zingine, na ilibidi waache Shughuri zao kumtumikia Mungu, na Wachungaji Aina hii hawahitaji kwenda Chuo Cha Biblia kumjua Mungu, hawahitaji kusoma Theology n.k, Mungu mwenyewe huwafundisha watu Hawa Kwa njia tofauti.

Hutokea Kwa Watu kama kina Marehemu Father Nkwera, ule wito ndani Yao, ule Moto ndani Yao unakua unafukuta, Roho wa Mungu anakua amefinywa kufanya kazi yake, ndiyo Wachache wa Aina yake wanaamua liwalo na liwe, na pale uongozi wa Kanisa unapogundua hawana chaguzi nyingine Zaidi ya kuwatenga watu wa Aina hiyo...!

Wanazo sababu zao, KKKT, Wasabato, Anglikana na Makanisa aina hiyo pia Yana sababu kama za Wakatoriki ila wao wamejitofautisha kidogo.

Cha Ajabu wote wawe Mapadre ama Wachungaji wanahubiri kuwa huu ni wakati wa Mwisho, na wengine husema tupo kwenye Dakika za Nyongeza, lakini Kuna Verse za Biblia wanazisoma na ama hawaziamini ama wanazipuuza, Kwa sababu sio wote wamepewa uwezo wa kuponya, wanaona si sawa.

Wanasahau
Matendo ya Mitume 2 : 17-21 inasema Nini....!!!
 
we nawe akili yako unaijua mwenyewe, ukweli wako umeutia chumvi nyingi ukaongezea na uwongo juu yake,

1. Tangu lini uti ikasababishwa na kutembea peku? labda ungesingizia gonjwa lingine, lakini sio uti, huu ni uwongo. Na tuseme ulimaanisha uti inasababishwa kwa ku share vyoo, hivi makanisani, misikitini mashuleni na kadhalika kila mtu ana choo chake??? au hukuenda shuleni? na kanisani jee? au wewe popote unapoenda umejengewa na unatumia choo chako mwenyewe??
Kuhusu viongozi wa dini kua na vyoo vyao, wewe shuleni ulitumia choo kimoja na mwalimu wako?, si kuna vyoo vya walimu na vya wanafunzi? yaani nyumbani kwako uwe na choo chako mwenyewe na kwa watu i.e shuleni, kanisani,msikitini napo utake choo chako mwenyewe, ni akili gani hizi?
Please acha kutafuta visingizio kwa vitu visivyo na maana.
 
2. Kusema kua father "alisema" anawaponya wagonjwa sio kweli, hapo umetia chumvi, father pamoja na viongozi wengine wa dini waliopewa karama ya uponyaji na Mungu, wao watakuombea na kukuweka katika njia sahihi, ni Mungu na ni MUNGU tu ndio atakaekuponya kupitia msaada na maombezi yao, ndio maana hata kituo chake pale kinaitwa "kituo cha sala na huduma za maombezi" hapo uliposema kua "amesema anaponya" sio kweli, ni akili finyu za binadamu kutotambua kua ni Mungu anakuponya kupitia maombezi ya watumishi wake, watu wanaoponywa kupitia viongozi hawa ni Mungu anawaponya na sio kiongozi fulani aliekuombea ulijue hilo. Hamna kiongozi wa dini yoyote anaetumia nguvu zake za kibinadamu kumponya mtu, ni Mungu tu ndio anaeponya, labda hukulielewa hilo.

Na unakosea sana, tena sana pale unapowalalamikia viongozi wa dini na hata kuwaita waongo pale shida zako zisipo tatuliwa, kama nilivyokuelezea ni Mungu tu ndio atakaekuponya sio padre, yeye anakuombea tu na kukuweka kwenye njia sahihi. Hujiulizi kwanini wengine wanaponywa na sio wewe? na je watu wote hao walioponywa na kusaidiwa wanasema uwongo?

Uache kuwalalamikia bila sababu za msingi, na pia ujue shida za watu zinatofautiana tena sana, na unakuta wengine shida wanazopata ni kwasababu ya makosa waliofanya, wengine siku zao za hapa duniani zimeisha. Mungu hana formular ya lini na wakati gani atamponya au kumsaidia mtu, na ana makusudio yake ambayo sisi binadamu hatuyajui na hatuwezi jua ndio maana inatupasa kuendelea kumuomba bila kuchoka na pia kubadilika na kuacha maisha ya dhambi. Kuna watu wanaponywa hapo hapo wakishaombewa, kuna wengine wanaponywa baada ya masaa, wengine baada ya masiku miezi na hata miaka.

Shida watu mnapenda mambo marahisi, unataka uombewe siku moja tu upone, wengine hawataki kubadilika na kuacha maisha ya dhambi na katika hali hiyo wanataka waombewe hivo hivo wapone lasivyo kiongozi anaitwa muongo
 
Hivi unaweza kuwaambia waumini wako waende chooni peku kwa kuwa kumesafishwa na maji ya Baraka? Hivyo vyoo wanatumia wakubwa kwa wadogo. We nawe huelewi, huko shuleni na misikitini mnaingia chooni peku?
 
Kumbe unajua kuwa ni Mungu pekee ndie mponyaji, ushuhuda wangu ni huu, mtoto anaumwa, mzazi anampigia simu father, father anamwambia mlete mtoto kanisani tumuombee atapona, mlete kwenye mkesha apate na maji ya Baraka, mtoto anakufa hapo kwenye kituo cha maombezi sababu hakupelekwa hospitali au hakupata huduma sahihi, wewe kama mdogo wako anakufa kwenye hayo mazingira ungesemaje? Si hilo tu kuumwa wote tunaumwa hata marehemu ameumwa akaenda hospitali, iweje wengine awaambie akawaombee na si kwenda hospitali? Kuomba ama kuombewa kupo lakini si kuacha kupata huduma sahihi. Hakuna mgonjwa asiyeamini kama Mungu atamponya mbona wasiende hospitali kuwaponya?
 
Umeongea vyema sana mkuu, tunahitaji sana kusikia vitu kama hvyo ili tuondokane na mambo km aliyofanyiwa Padri Nkwera
 
nimekulia river saidi nimecheza sana mule ndani kwenye kituo chake cha maombezi!!! Ila ukweli usemwe ukishaanza kuwa muumini wa lile kanisa kuna mawili usipo kuwa zezeta basi utaanza kutembea kwa kuchechemeea!!! Mnisamehe ntakao wakwaza
 
Hivi unaweza kuwaambia waumini wako waende chooni peku kwa kuwa kumesafishwa na maji ya Baraka? Hivyo vyoo wanatumia wakubwa kwa wadogo. We nawe huelewi, huko shuleni na misikitini mnaingia chooni peku?
Unaweza kudhibitisha maji yanayotumika kusafishia vyoo ni maji ya baraka??
No research no comment, (kama hujafanya uchunguzi wa kina usitoe maoni kuepuka kusema uwongo, ni dhambi)
 
Ndio maana nimekwambia ufanye research kwanza, lile sio kanisa ni KITUO CHA HUDUMA ZA MAOMBEZI.

Pili, una mgonjwa mahututi kilichokufanya umpigie simu Father kwanza badala ya kumpigia simu daktari ni nini??

Tatu, na je ungemkimbiza hospitalini akafia mikononi mwa daktari nae ungemlaumu??

swala la kuombewa na kupona linahitaji IMANI, hata wakati wa Bwana Yesu hawakuponywa wote na walioponywa waliambiwa, "ENENDA ZAKO IMANI YAKO IMEKUPONYA."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…