LAMINE YAMAL, NAOMBA msikilize walau Ally Nipishe na Fraser, kuhusu wanawake utajifunza kitu, anachomaanisha baba yako

LAMINE YAMAL, NAOMBA msikilize walau Ally Nipishe na Fraser, kuhusu wanawake utajifunza kitu, anachomaanisha baba yako

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
4,686
Reaction score
10,018
Mawazo kina yametawala kichwa changu, ila uwezo Sina kulitawala jicho langu,

Hii ni baadhi ya mistari kutoka Kwa ally nipishe kijana alie wika sana enzi hizo, huyu dogo alipata masala, Iko hivi, baada ya dogo kuwika sana, alipata limama inasemekana ni la kizanzibari, huyo mama akaingia kwenye mahusiano na ally nipishe, dogo hana hili Wala lile mara akahongwa gari nadhani altezza kipindi hicho talk of the town dogo kaisukuma ndinga mwaka mzima akiwa dar, basi bhana siku Moja hana hili Wala lile, kapigwa mkono na watu, paki pale Mzee, akaulizwa hii gari umetoka wapi, ile hajajibu vizuri akaambiwa hii gari ya wizi, kapelekwa polisi kilicho fuata baba yake akaanza kuuza mali ikiwemo mashamba ili kumtoa ally jela.

Fraser huyu ni muigizaji wa the mummy na George of the jungle, alioa mke mzuri TU pesa ilikuwepo na ustar ndo mahala pake Kwa muvi zake hizo, kipindi anaigiza akataka aoneshe uhalisia kuruka kwenye jengo mara paah chini, hoi akavunjika mifupa miaka Saba mfululozo Yuko kitandani kumbe kipindi tunafurahia muvo zake jamaa alikua kitandani kafungiwa kamba za barafu, ice packs, kwenda chooni mpaka abebwe,

Mkewe aka mpeleka mahakamani alidai talaka, avunje ndoa pia akamtaka awe anamlipa child support ya Dola laki tisa Kwa mwaka, kumbuka anaeambiwa alipe hizo pesa yupo kitandani haiwezi, jamaa alienda kulia mahakamani jamani hali yangu si nzuri taweza vipi lipa hizo pesa weee nani hamuelewe, jamaa akaona sio KESI kaanza kuuza mali zake alipe deni la mkewe, wana ita sweetheart my baby, my love Leo hii anamtesa mahakamani, hajamfumania, hawajagombana dah.

Jamaa alikata tamaa ya maisha kazi hana mke kukimbia tena na KESI juu, mali zimekwenda jamaa akataka kujiua.

MUNGU akikupa mtihani hukuchujia baadhi ya marafiki na ndugu nikama Fraser marafiki zake wote walimkimbia Hadi director cjui camera man alio Fanya nao kazi wote nduki, baada ya jamaa kukata tamaa, akapata dili la kuigiza whale kama sikosei filamu iliyo mrudisha kwenye ramani, alipo pewa tuzo za Oscar Fraser alilia kama mtoto akikumbuka panda shuka aliyopitia.

Sasa bhana baba yake mzazi LAMINE YAMAL mwanasoka kinda na tajiri, amepost MTANDAONI akilala Mika kumbe kipindi kile kamshauri LAMINE YAMAL kuhusu kuachana na mbunye dogo anabadili sana mademu aache awekeze kwenye soka ajenge ufalme badae atakula Bata tu , kumbe dogo alichukia, kamblock Mzee amsalimii na pesa hatumii, japo Mzee ana amini hata mama yake LAMINE anachangia kumshawishi mwanae huyo kumchunia na kumdharau.

Anyway, tuyawache. Good morning, ladies and gentlemen; good morning once again.

Screenshot_20260830-060422.jpg
Screenshot_20260830-055306.jpg
Screenshot_20260830-063556.jpg
 
Kwenye maisha usijisahau sana,usitegemee watoto wala mtu yeyote yule,
weka akiba yako ambayo itakusaidia uzeeni mwako,

Dunia inabadilika,vijana wa siku hizi hawashauriki,Dunia imekua na life style nyingine kabisa,huwezi kuwalazimisha hawa vijana wa sasa waishi maisha ambayo sisi tuliyaishi,

Lea familia yako ila usijisahau na wewe mwenyewe.
 
maisha yanaenda shagala bagala leo mtu maisha mazuri kesho magumu au kinyume chake
Acha tyu, huyu jamaa alikua star ghafla akapotea kumbe walipata msala, ally na Fraser wote walifulia, Fraser alikua tajiri mkubwa lakini aliisha mpaka kuanza kurandaranda mtaani akijikongoja, noma sana sikuamini asee maisha haya
 
Kwenye maisha usijisahau sana,usitegemee watoto wala mtu yeyote yule,
weka akiba yako ambayo itakusaidia uzeeni mwako,

Dunia inabadilika,vijana wa siku hizi hawashauriki,Dunia imekua na life style nyingine kabisa,huwezi kuwalazimisha hawa vijana wa sasa waishi maisha ambayo sisi tuliyaishi,

Lea familia yako ila usijisahau na wewe mwenyewe.
Baba yake LAMINE ana haki ya kumkanya mwanae pale anapo kosea ikizingatiwa, dogo bado sana mdogo, sasa kuplay part ya ubaba ndio kosa?
 
Baba yake LAMINE ana haki ya kumkanya mwanae pale anapo kosea ikizingatiwa, dogo bado sana mdogo, sasa kuplay part ya ubaba ndio kosa?
Jifunze kusoma na kuelewa,

Kuna sehemu yeyote ile ambayo mimi nimesema kua Baba wa Lamine kumkanya mwanae ni kosa?
Kuna sehemu yeyote ile mimi nimesema kua Baba wa Lamini hana haki ya kumkanya mwanae?

Comment yangu imejikita zaidi kwenye issue ya ''Hata hela hamtumii'' ndio nikakumbusha kua tusijisahau kujiwekea akiba,
Usinilishe maneno ambayo sijayasema.
 
Acha tyu, huyu jamaa alikua star ghafla akapotea kumbe walipata msala, ally na Fraser wote walifulia, Fraser alikua tajiri mkubwa lakini aliisha mpaka kuanza kurandaranda mtaani akijikongoja, noma sana sikuamini asee maisha haya
hivi kuna wanawake wanaopitiaga mambo kama haya anakuwa tajiri kwa juhudi zake anakuja kupoteza kila kitu?
 
Mzee wa Lamine Yamal anakosea sana kulia-lia mtandaoni kuhusu mtoto wake kum-block. Mtoto ana miaka 19, anachezea klabu kubwa duniani na anamiliki mamilioni ya Euro. Huwezi ku-deal na mtu wa namna hiyo kwa amri na maneno ya shombo.

Huyo mzee anatumia mbinu za malezi za miaka ya 1990 kwa kijana wa Gen Z anayejilisha mwenyewe na kulisha ukoo mzima. Akili kubwa ilitakiwa itumike hapa, sio kelele za mitandaoni.
 
Dogo kama anafanya hayo kwa mshua wake basi ajiandae, Wakati wa Makuzi Uko niliwahi kupishana na Mzee lakini influence kubwa ilikuwa ni mama,

Vijana wawe makini Sana mana Mtu pekee wakiume Anae wish ufanikiwe zaidi na Umzidi mafanikio ni Baba yako

Huyu Mzee pia aache kutumia mitandao kumuanika Mwanae, kama mtoto amekuwa inaccessible basi atulie Tu akili ikimrudi mbona atamtafuta tuu
 
Hivi kuna reliable source yoyote ile imeandika hii habari ya Baba wa Lamine kulalamika hivyo?
Isije ikawa tunamlaumu Baba wa Lamine kwa habari za Unaambiwa,nasikia,inasemekana.
 
Jifunze kusoma na kuelewa,

Kuna sehemu yeyote ile ambayo mimi nimesema kua Baba wa Lamine kumkanya mwanae ni kosa?
Kuna sehemu yeyote ile mimi nimesema kua Baba wa Lamini hana haki ya kumkanya mwanae?

Comment yangu imejikita zaidi kwenye issue ya ''Hata hela hamtumii'' ndio nikakumbusha kua tusijisahau kujiwekea akiba,
Usinilishe maneno ambayo sijayasema.
Hujamuelewa jamaa!
 
Dogo kama anafanya hayo kwa mshua wake basi ajiandae, Wakati wa Makuzi Uko niliwahi kupishana na Mzee lakini influence kubwa ilikuwa ni mama,

Vijana wawe makini Sana mana Mtu pekee wakiume Anae wish ufanikiwe zaidi na Umzidi mafanikio ni Baba yako

Huyu Mzee pia aache kutumia mitandao kumuanika Mwanae, kama mtoto amekuwa inaccessible basi atulie Tu akili ikimrudi mbona atamtafuta tuu
Mara nyingi ukiwa huna mahusiano mazuri na mkeo, atatafuta mbinu zote ahakikishe mmekosana na kijana wako wa kiume. Uanaume ni kuwa makini na jinsi unavyohusiana na kijana wako. Pili ni kosa kubwa kutegemea mtoto akutunze. Imagine mama wa kijana wako ni Lamomy wangu Mtiti huo ni wa kiwango gani
 
G mbona unajimilikisha mali na huduma hakuna? Sikuelewi ujue 😹😹
 
Back
Top Bottom