Land cruiser VX V8 ni ndege ya chini aisee! Ndiyo maana viongozi hawataki kuyaachia

Land cruiser VX V8 ni ndege ya chini aisee! Ndiyo maana viongozi hawataki kuyaachia

Mimi na IST huwa natembea hadi 150 usiku. Nikwa nasafiri napenda kutembea usiku kwa vile hakuna 50.
Kwa jinsi mziki wa IST ulivyo mtamu, sioni haja ya gari nyingine ya gharama kubwa.
Wengi wana magari mazuri but driving skills ni ndogo. Ni mwendo wa kuwatesa na magari yao huko bara barani. Wengine wanaojichanganya kuleta ligi, huwa wanaishia kuaibika.
Acha uongo wewe, kila gari inauwezo wake, huwezi kuweka ligi na gari za maana ukiwa na ist yako, labda ukute yupo mmama anaendesha tena hataki ligi na mtu. tunao tembea barabarani tunajua hali za gari zote ,iwe milori au hizi za kawaida,
 
Haha! airbags za japan ni simple sana kutengeneza kuliko za mzungu , discovery, range ,bmw, benz busta zikizingua kweli unaweza kupaki gari,
Japan ametumia tech rahisi sana kwenye air bags ndo maana hata watu wa costa zikizingua siku hizi wanatengeneza za local .
Unahitaji air supply, na kitu kinaitwa mzani , baas!!! Gari inarudi kwenye mneso wa busta !!! You ll loose abs support ,,na vikolombwezo kadhaa lakini sio mneso
Sasa kwanini prado j120 nyingi zinakuja na Air suspension, ila nyingi ukizikuta kwa mswahili zina coils?
 
2021 kuendelea Toyota wametoa tolea jipya la 300 series ambayo sio V8 ni V6

Edit bango lako ufafanue ni Aina gani ya land cruiser uliopanda pamoja na model ya engine yake

Hiyo picha ni ya landcruiser 300 series , ambayo technically ni v6 na si v8
Kibongobongo lc kuanzia 2015 kuja juu zote zinaitwa v8 😃 ni kama vituo vya mafuta vinavyoitwa shell
 
Hiyo naijua na nishawekaga Uzi wake humu, lakini haina mwrndo kama land cruiser vx v8! Dar Dom 5:30hrs
VX V8 Dar Dom km 460 massa 5:30 dereva mzembe. Moro Mbeya km 650 chuma inatembea massa 4:00 tu mnaondoka saa 12 asubuhi mnawahi kikao saa 4 mpaka saa 7 mchana baada ya Lunch chuma inarudi by saa 12 jioni mpo Moro
 
Mwamba uyu apa kama umepewa lift ya mkoa unaweza kulilia usishuke[emoji1787][emoji1787] kuna ndege ya ardhini alafu kuna hii Jet fighter LEXUS L570View attachment 2373572
Hii niliwahi panda na boss tunawahi kikao, ilikua akikanyaga ni sawa na ndege iko kwenye runway inataka iachane na ardhi, afu huhisichochote, nikamwambia boss usikimbie sana. mana dizaini unahisi bandama na figo vinataka vitokee mgongoni.
 
Mwezi wa sita nilikuwa Babati... Katika shughuli zangu nikawa naelekea Arusha... Mimi nina gari ya kawaida sana... Lakini sehemu kama imenyooka naweza jikuta 160 au zaidi kidogo.. Ila sio muda mrefu...

Kuna sehemu imenyooka kama rula maeneo ya Magugu kabla ya Minjingu... nilipitwa na machine hiyo v8 sijui series L300 ... Yaani niko 160 ...nikaongeza mpaka 170 ...sikuiona hiyo gari...
Hiyo machine v8 L300 series akikupita.. Usishindane nae unaweza ukakata timing belt.. Nilijaribu nikaogopa
Ni LC200 V8 au LC300 V6.
 
Mwezi wa sita nilikuwa Babati... Katika shughuli zangu nikawa naelekea Arusha... Mimi nina gari ya kawaida sana... Lakini sehemu kama imenyooka naweza jikuta 160 au zaidi kidogo.. Ila sio muda mrefu...

Kuna sehemu imenyooka kama rula maeneo ya Magugu kabla ya Minjingu... nilipitwa na machine hiyo v8 sijui series L300 ... Yaani niko 160 ...nikaongeza mpaka 170 ...sikuiona hiyo gari...
Hiyo machine v8 L300 series akikupita.. Usishindane nae unaweza ukakata timing belt.. Nilijaribu nikaogopa
Mkuu hizi gari zisikie tu.
Zina power mpaka 300HP na turbocharger mbili.
Hivyo ziki overtake power gain ni kali sana.
Ninayo moja LC200 nami naelekea Dom.
Kuna Brevis akaona nakuja nyuma yake, akakanyaga mafuta.
Hakujua LC200 ukikanyaga mafuta turbochargers zote zinafunguka, nilimpita akiwa 180km/r.
 
Mkuu hixi gari zisikie tu.
Zina power mpaja 300HP na turbocharger mbili.
Hivyo zikiovertake power gain ni kali sana.
Ninayo moja LC200 nami naelekea Dom.
Kuna Brevis akaona nakuja akakanyaga.
Hakujua LC200 ukikanya turbichargers zote zinafunuka, nilimpita akiwa 180km/r
Wacha weee!

Kwahiyo ukajisikia raha?
 
Back
Top Bottom