Land cruiser VX V8 ni ndege ya chini aisee! Ndiyo maana viongozi hawataki kuyaachia

Land cruiser VX V8 ni ndege ya chini aisee! Ndiyo maana viongozi hawataki kuyaachia

Land cruiser vx v8 hii gari isikie tu!

Hii ni ndege ya chini!
Ukionja hii gari unaweza ishauri Serikali kuwe na leseni maalum kwa madereva wa hizi gari maana ni ndege ya chini wallah!
Mwenye kufahamu bei halisi ya kumkamata huyu mdudu mkononi ni Tsh ngapi?

Nahisi ndiyo maana ilibatizwa Ushangingi maana ni kweli VXV8 ni shangingi la njia siyo uwongo!

Na ukitaka kuielewa vizuri panda kwenda safari ndefu ndiyo utajua TOYOTA HAPA ALITULIZA KICHWA.

Uraibu wa hii gari ni viongozi wachache sana wakiafrika wanaweza kukubali kuushinda ili waachane kununua magari Haya ya gharama kubwa!

Zote zipo fiti ila hii land cruiser vx v8 2022 ni kiboko yao!

Ni gari bomba sana, very comfort, stable, luxury, High speed tolerance, sensor of crush, music system, massaging seat, sleeping sensor and much more!

Napata ugumu kukuelewesheni hii ya 2022 ilivyo bora na bomba ila kama kuna mtu yuko karibu na Mwigulu Nchemba anayo moja bado mbichi kabisa unaweza kuitizama ni mashine!

Land cruiser vx v8 inasifa moja kuu! INAOMBA NJIA MUDA WOTE!

Tunawalaumu bure viongozi wanavyopita pyuupyuupyuu huko barabarani siyo wao! Bali ni land cruiser vx v8 ndivyo inataka mambo hayo!

Naomba Mungu anijalie na mimi siku nimiliki yangu!

View attachment 2373415
 
Unajua utamu wa gari ni engine perfomance,sasa kwa hizi Vx V8 sio kwamba inazidi zile za europe,ila kwa kweli wamejitahidi kiasi chao,maana kwa wazungu nao ukichukulia machine kama Range Rover sport 2022,kwakweli inabidi Toyota aende shule kwanza...
 
Unajua utamu wa gari ni engine perfomance,sasa kwa hizi Vx V8 sio kwamba inazidi zile za europe,ila kwa kweli wamejitahidi kiasi chao,maana kwa wazungu nao ukichukulia machine kama Range Rover sport 2022,kwakweli inabidi Toyota aende shule kwanza...
Landrover Range Rove ni gari nzuri sana .
Lakini ukikaa nayo miaka 2-3 una bahati, LC200 unakaanayo miaka 10 haisumbui.
Na parts zote zipo.
 
Land Cruiser ni gari aisee...
 

Attachments

  • IMG-20221020-WA0144.jpg
    IMG-20221020-WA0144.jpg
    88.3 KB · Views: 30
  • IMG-20221020-WA0176.jpg
    IMG-20221020-WA0176.jpg
    116.3 KB · Views: 31
Hakuna luxury car ya seat nane 😳
Tofautisha kati ya luxury and expensive car mark x mpya ipo pia kundi la luxury cars
Gari ya dollar laki moja plus unasema ni expensive car....ebu google bei ya Lamborghini Aventador halafu urudi
 
Nilipewa lifti na mshikaji wangu ni Waziri toka Katavi mpaka Dodoma mzee comfortability,standard & speed ya yale magari ni balaa na nusu. Ndio maana wabongo wanalewa uongozi aisee. Hakuna raisi atakuja kupiga stop V8 hawatakubali wajuba wa nchi hii.
 
Ndugu yangu mfano kama hiyo LC 300 AU LC 200 nitalilisha nini ili litembee na huku kazi zenyewe yule kichaa aliondoka nazo? Tupo huku Ibindi Katavi tunasarura vifusi mtu unaweza kuokota hata robo gram[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Upo ibindi mkuu mm nipo kakese
 
Upo ibindi mkuu mm nipo kakese
Karibu sana mkuu na wanapouzia miwa hapa mashine za karasha za mwanzo utanikuta nimetoa macho tu na miwa yangu sina namna huku najianda kwenda Burundi kufuatia agizo la ndugu yangu mmoja hivi kutoka kiomboi🤣🤣🤣🤣
 
Hao waangalia magari ya kina Cr 7 nimeshangaa sana kuona akitetea kitu kwa nguvu kweli..
Hao ndo wanamiliki laxury car...sisi wengine tunamiliki vyombo vya usafiri cha kututoa sahemu moja kutupeleka sehemu nyingine
 
Back
Top Bottom