LATRA mabasi kuondoka saa 9 usiku ni usumbufu na mzigo wa wananchi

Wabongo ni watu wa ajabu ajabu tu.
Kutwa nzima usafiri upo kwani lazima uondoke saa 9?
Kumbuka, Kulala Lodge badala ya home kunaongeza akili, maarifa na kipato kwa mwenye na nchi
 
Lakini hata Kenya yanasafiri usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo ni watu wa ajabu ajabu tu.
Kutwa nzima usafiri upo kwani lazima uondoke saa 9?
Kumbuka, Kulala Lodge badala ya home kunaongeza akili, maarifa na kipato kwa mwenye na nchi
Yeye anataka mabasi ya saa tisa lukwili tu.
 

Kwani hakuna mabasi ya muda unaotaka wewe?
 
Hata ndege zipo za usiku mbona wanafika on time.
 
Jamani kwani kuna shida gani kusafiri hiyo saa? Wale wanaopanda ndege za saa 9, 10 na nane usiku huwa wanafanyaje?
Umeandikiwa reporting time ni saa nane basi tafuta pa kujibana mpaka hiyo saa nane usiku unareport unaingia kwenye basi, unaanza kusinzia basi. Wakati unasubiria unaweza kupata kahawa au chai na chapati kwa mama/baba lishe.
Huo ni ushauri wangu. Watu tubadilike. Siku hazigandi.
 
Mbona iko sawa tu. Fikiria hata ukitoka saa kumi na mbili itakulazimu uamke saa kumi za usiku.
 
Kwani mtu analazimishwa saa9, gari zipo kuanzia saa 9 na kuendelea..
 
Kusafiri usiku raha sana afu uwe na pisi kwenye siti apo unamshawishi konda azime taa tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NAKAZIA HAPO MKUU!.
 
Msafiri halazimishwi, kuna magari ya saa 9, saa 11, na saa 12 asubuhi . Kuna mabus yanatoka mbali mfano Bukoba , Mwanza, Sirari, Tunduma na kshlk, kuondoka mda huo abiria anafika mapema aendako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…