HOJA LATRA toeni vibali kwa daladala, Mwendokasi peke yake haiwezi kukidhi ruti ya Mbagala - Mjini

HOJA LATRA toeni vibali kwa daladala, Mwendokasi peke yake haiwezi kukidhi ruti ya Mbagala - Mjini

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Maeneo ya Mbande, Msongola, Kitonga kumeanza kuwa na shida ya usafiri wa kuelekea katikati ya mji yaani Posta na Kariakoo.

Hii ni kwa sababu gari zote zenye hizo ruti za Stesheni, Posta & Gerezani Kariakoo zimekuwa zikinyimwa vibali za kutoa huduma kwenye hizo ruti.

Ikumbukwe awali mnamo Juni 2026 lilitolewa tangazo la kuzuiwa kwa daladala katika barabara zote zinazofungamana na barabara za DART ikiwemo kutoka Mbagala to Gerezani na Posta - Stesheni lakini baada ya mizozo ya raia wamekuja kulitimiza lile kwa indirect ya LATRA kuzuia vibali kwa daladala.

Kila anayekwenda LATRA kuhuisha kibali cha ruti baada ya kuisha muda wake anabadilishiwa ruti na kwa kuwa gari ni nyingi ruti tunazohamishiwa nazo zimekuwa hazitoshi imesababisha kuundwa kwa ruti mpya za Mbande Tambani to Mbagala Rangi 3.

Mipeko to Mbagara Rangi Tatu ruti ambazo ni hewa kwa sababu ya ubovu wa Barabara za hayo maeneo haya-support kwenda zaidi ya Bajaj.

Tunashauri LATRA iendelee kutoa vibali kwa daladala ili kuondoa hii kero ya usafiri, Mwendokasi peke yake haiwezi hudumia kundi hili lote kwa sababu za kijiografia, kipato cha abiria na miundombinu pia.
 
Daladala zilete watu kwenye feeder ya mwendokasi kutokea hayo maeneo unayopendekeza, kwamba daladala ziendelee kwenda kariakoo hatutatibu tatizo la foleni hata tutanue barabara vipi kutokana na mtindo wa hovyo wa uendeshaji daladala kwenye mji huu wa Dar...foleni nyingi Dar zinasababishwa na uendeshwaji holela wa daladala...zifanye kazi pembezoni huko ziwatoe watu matitu ziwalete rangi tatu lakini sio kwenda kariakoo shule
 
Dsm daladala zimezidiwa watu ruti nyingi tu lakini huwa nawaza mabosi hawaoni kama hizo ni fursa kuongeza daladala
 
Back
Top Bottom